SALAMU ZANGU ZA LEO

BWANA YESU KRISTO ATUKUZWE SANA....

Ni matumaini yangu, kuwa unaendelea vyema katika kukua na kumjua Christo.
N amtukuza MUNGU kwa ajiliyako, pia kwa nafasi hii ambayoamenipa ya msingi. Napenda kushirikishana nawe na kukuhimiza zaidi juu ya safari hii ya Imani tuliyo nayo juu ya mabo kadhaa muhimu kama ifuatavyo;

  (01)1petro 2:9, Moja kati ya nafasi muhimu ambayokila Mwana wa MUNGU anapaswa kuifahamu, ni Ukuhani wa Kifalme.

-Kuhani maana yake kiongozi wa taratibu za kiibada au ni mtu ambaye anawaongoza watu wadumu  katika mambo yamuhusuyo MUNGU. Ebrania 5:1
-Mfalme ni kiongozi aneyetawala  kwa njia ya/au kulingana na sheria ,kanuni, na taratibu za nchi au jamii fulani ya watu au mahali husika.
-Siri hiinapenda uifahamu maana kanisa limekosa kuifahamu na linashindwa  kuishi maisha ya ushindi. Ndugu katika BWAN, napenda kwanzia leo ufahamu wajibu huu na siri hii, ISHI KAMA KUHANI PIA KAMA MFALME, katika eneo lolote ulipo.

 (02)Zaburi 82:6 Sisi ni miungu na wana wake aliye juu. Miungu kwamaana ya wingi-hivyo mimi na wewe tu miungu na watoto wa MUNGU. Hii inamaana kuwa sisi tumeubwa na ndani yetu kuna nguvu y MUNGU, ambayo kama tukijitambua na kusimama katika nafasi zetu, tumepewa uwezo wa kufanya mambo kama Mungu, au kufanya mambo makubwa sana na yaajabu sana yenye utukufu kwa MUNGU wetu, kulingana sawasawa na nguvu ya MUNGU, iliyopo ndani yetu. Hivyo jambo la muhimu ni kwamba, ifahamu Ibada, na Ibada simaanishi tu kwenda maisha ya kwenda kanisani, bali Ibada ni jumla ya mambo yote ya maisha ya ya mwanadamu na nimfumo mzima  wamaisha ya mwanadamu ambayo, jinsi ambavyo anahusiana na MUNGU. Chunguza MUNGU anakazi gani, na kwa kuwa wewe usehemu  yake na umfano wake ili kukamilisha na kutimiza kile anataka kukifanya hapa duniani...hivyo simama na kushirikiana naye kikamilifu ili mapenzi ya Muumba wako yatimie, ili kukamilisha ufalme wake na kuujenga hata kuwa imara san ahapa duniani kama kule mbinguni.

SIFA ZA KUHANI NA MFALME
-Kufanya upatanisho kati y awanadamu na MUNGU, au kati ya mtu na mtu. (walawi 4:20,12:8)
-Amejaa Imani, yaani uhakika wa mambo na Neno la matumaini na ni jasiri si,ku zote. ana Imani  kubwa juu mambo yate kwa MUNGU anayemtumikia. (kumbukumbu la torati 20:2-4)
-Amejaa hekima na maarifa ya kuwaelekeza wengine katika njia ya KRISTO. (kumbukumbu la torati 24:8)
-Ni mtu mwaminifu ambaye yupo tayari kufanya mambo yote sawasawa na nia y aMUNGU. (1samweli 2:35)
-Hukaa patakatifu pa  MUNGU,pia hushusha/huachilia UTENDAJI WA NGUVU ZA MUNGU na uwepo wa MUNGU (1falme8:10 "Ikawa makuhani walipotoka katika patakatifu nyumba ya BWANA, ikajaa wingu.......")
-Anaruhusiwa kuingia nyumbani nyumbani mwa BWANA,hata wakati wengine hawaruhusiwi kuingia (hawaruhusiwi kwa sababu mbalimbali yawezekana uchafu wao au kujihusisha na mambo ya mashetani na miungu kinyume na mapenzi ya MUNGU.) Kwa sababu kuhani ni mtu ambaye ametakasa na Mungu, na ni mtakatifu. (2nyakati 23:6)
-Siraha kubwa na kitendea kazi kikubwa ambacho kinampa kuhani kibali mbele za MUNGU, toka zamani hata sasa ni DAMU, huu ni utaratibu wa MUNGU toka zamani hata sasa. Na kwa sasa tunatumia damu ya YESU KRISTO, hii ndiyo damu bora sana kuliko damu za wanyama wengine wote nabe vyote.

 (03)Ebrania 2:18 "Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojalibiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa."
Napendaufahamu ya kuwa majaribu yapo, shida zipo, ila yupo yeye tunaye mwamini BABA YETU, AISHIE MBINGUNI, aliye mkuu ambaye nu mkuu na mwenye uweza juu ya mambo yote, ambaye alimtoa mwana wake wa pekee ili atushindie taabu na kutuokoa na shida zote, na kuonesha msaad na mfano kwetu, kuwa hata sisi tunaweza shinda, na tena zaidi yeye ataweza kutusaidia na yupo tayari kutusaidia wakati wowote ule tumwitwpo na tuwapo katika majaribu na katika shida za namna zote. JAMBO HII amelisisitiza sana ya kuwa kila saa na kila wakati yatupasa kumwamini na kumwangalia YEYE MUNGU WETU,NA KUAMINI UKOMBOZI NA WOKOWO WA MUNGU KWA NJIA YA YESU KRISTO,MWANA PEKEE WA MUNGU,MPATANISHI NA MKOMBOZI WA MAIOSHA YETU.

TAMBUA KUWA NAKUPENDA SANA, NA NAKUOMBEA SANA NA KUKUBARIKI SANA KWA JINA LA YESU KRISTO. BARIKIWA SANA ZIDI USOMAPO SALAMU HIZI, KWA JINA LA YESU KRISTO NEEMA NA REHEMA ZA MUNGU ZIWE NAWE DAIMA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO.
(2wakorintho 9:8) 
Ni mimi Elisha Ndumizi, 0654501879

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

UWEZA WA MUNGU JUU YA MAGONJWA NA VYANZO VYAKE

UMUHIMU WA IBADA

IJUE IBADA-SEHEMU YA KWANZA