UWEZA WA MUNGU JUU YA MAGONJWA NA VYANZO VYAKE

 SEMINA YA NENO LA MUNGU-DODOMA UWANJA WA BARAFU*

*MWL.CHRISTOPHER MWAKASEGE*
*SOMO: UWEZO WA MUNGU JUU YA MAGONJWA NA VYANZO VYAKE.*
*TAREHE  06 MAY, 2018*
*SIKU YA KWANZA*
*👉 NAMBA ZA SADAKA* https://goo.gl/Z3ozYB
*👉LINK YA SEMINA YA LEO YOUTUBE* https://youtu.be/ZU8Q2qbvqPE
*👉NAMNA YA KUPATA CD&DVD BONYEZA HAPA* https://goo.gl/tgwoub
Hili somo tutaenda nalo kwa siku 8 vile Mungu atakavyotufundisha hatua kwa hatua na tutapata nafasi ya maombi kila siku kadri Mungu anavyotuongoza kwa kadri ya kile Mungu anataka kufanya kila siku.
Leo katika kuweka msingi nataka tujibu swali ya _*kwanini MUNGU anataka tujue ya kuwa kuna sehemu ya uweza wake alioutenga mahususi kwa ajili ya kuponya magonjwa na vyanzo vyake?*_
Tutaangalia mistari mitatu na kujibu hili swali kama ifuatavyo:-
*Luka 5:17, Luka 4:18 na Matendo 10:38*
*Luka 5:17*
_“Ikawa siku zile mojawapo alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waalimu wa torati walikuwa wameketi hapo, waliotoka katika kila kijiji cha Galilaya, na Yudea, na Yerusalemu; na uweza wa Bwana ulikuwapo apate kuponya.”_
Nimekupa huu mstari ambao unaeleza huduma ambazo Yesu alikuwa nazo alipokuwa hapa duniani kwa jinsi ya mwili akizunguka na anapotuambia hapa anasema kulikuwa na mafarisayo na waalimu wa torati walikuwa wameketi hapo, na watu toka maeneo mbalimbali.
Kwa wale wanajua ramani ya Israeli ilivyo au umepata nafasi ya kwenda Israeli au unanisikiliza ukiwa Israeli unaweza ukaelewa maana ya kukusanya watu kutoka kila kijiji cha Galilaya na Uyahudi na Yerusalemu. Inamaanisha kulikuwa na kundi kubwa ambalo lilikuwa limekuja kumsikiliza na Yesu alikuwa pale.
Lakini mwandishi aliekuwa anaandika alikuwa chini ya uvuvio wa Roho Mtakatifu, aliandika kipengele ambacho usingewaza kuwaza kwamba kilikuwa kina umuhimu kwa maana alisema _na uweza wa Bwana ulikuwapo apate kuponya._ Huyu ni Yesu alikuwa pale na kulikuwa na sababu nyingine ya kutuambia ya kwamba Yesu yupo, lakini kuna uweza wa Bwana uko mahali hapo ili apate kuponya.
Biblia inazungumzia habari za Yesu kuwa alikuwa anaponya lakini Biblia hiyo hiyo inataka tujue ya kwamba kulikuwa na uweza ambao ulikuwa unamsaidia Yesu kuponya (Uweza wa Bwana ulikuwapo apate kuponya)
Twende kwenye
*Luka 4:18*
_“Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini Habari Njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,”_
Huyu ni Yesu kwa jinsi ya utaratibu ulivyowekwa yalikuwa ni mahubiri yake ya mara ya kwanza (kwa lugha ya kawaida alikuwa kanisani kwa maana alikuwa kwenye Sinagogi) na hatujajua alichaguliwaje kwamba asome yeye kwa maana kwa desturi kulikuwa kuna neno linasomwa inawezekana wale viongozi walikuwepo pale walisema Sabato hii nani asome. Sabato ile Yesu alikuwepo alipewa yeye kitabu (chuo cha nabii Isaya). Alipopewa alienda moja kwa moja mahali palipoandikwa hiyo Luka 4:18.
Na Ukisoma mistari inayofuata
*Luka 4:19‭-‬21*
_“Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.  Akakifunga kitabu, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.”_
Kwa lugha ya nyingine unaweza ukasema huyu aliekuwa anasemwa na Isaya ni mimi. Unaweza ukaelewa yeye alikuwa mwanadamu kama sisi alitembea kama sisi, amevaa nguo kama wengine, ameenda Sinagogi kusali kama Wayahudi wengine. Walikuwa wanamfahamu kabisa ambao wanajua malaika Gabrieli alivyomtokea Mariamu na baba yake Yusufu na mamake ni Mariamu na ndugu zake walikuwepo hapo na wanamjua kabisa kukua kwake na maisha yake na ufahamu wake juu ya mistari ya vyuo mbalimbali vya Biblia kwa jinsi sisi tunavyoizungumza kwa sasa.
Wakati ule hakukuwa na Biblia, walikuwa wanapewa chuo cha Isaya na vitabu vingine vilikuwepo wakati ule. Walikuwa wanamtazama kwa mtazamo ule wa kusema sasa hivi naenda kanisani utakuta kuna mtu na anampenda Mungu na mistari ya Biblia.
Nakumbukuka nilipokuwa na kiu ya kumtumikia MUNGU nilikuwa naenda jumamosi kanisani namtafuta mchungaji wa zamu au kiongozi wa zamu ya kuongoza ibada namuuliza kama kuna kazi yoyote anayoweza kunipa hata tu kusoma mstari wa Biblia. Walinishangaa sana lakini nilikuwa na kiu ambayo haielezeki na namshukuru MUNGU kwa wale wachungaji walionielewa maana kwangu ilikuwa ni zoezi kubwa sana maana kipindi hicho sikujua kabisa kama ni mwalimu au mhubiri. Sasa nakupa hii picha ili uweze kuelewa ya kwamba hakikuwa kitu cha kushangaza kumuona YESU akipewa chuo cha nabii Isaya kusoma bali kilichoshangaza ni pale aliposema yale maneno yananihusu mimi.
Kwa lugha nyingine anawaambia msinitazame kama mlivyozoea kuna kitu nimebeba, maana anasema roho wa BWANA yu juu yangu kwa maana amenitia mafuta, ndiko neno la upako lilikotoka kwamba amenipata/amenitia mafuta. Mafuta maana yake ni nguvu za MUNGU zilizoko ndani ya ROHO MTAKATIFU. ROHO MTAKATIFU ni mmoja lakini nguvu za MUNGU zilizopo ndani yake zimegawanyika tofauti tofauti kufuatana na majukumu ambayo MUNGU anataka yafanyike.
SWALI KUBWA: *Kwanini alitaka wale watu wajue?* Maana angeweza akanyamaza tu lakini akaamua kusema.
Sasa tumesoma ile *Luka 5* Kwa hiyo Luka anapoandika hapa anataka sisi tujue tunaosoma kwamba kulikuwa na uwezo wa BWANA ili kila ajuaye apate kuponywa na si wote walijua kipindi kile. Sasa anataka sisi tujue, sisi tunaosoma kwa sababu mstari wa namna hii huwezi kuupata mara kwa mara sehemu nyingi ya Biblia ambako YESU alikuwa anaponya.
*Matendo ya Mitume 10:38*
_“habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.”_
Biblia inatueleza Petro alipokuwa anahubiri anaeleza habari za YESU anazungumza na kusema “habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta” na yale mafuta alipoyapata Biblia imetenga kabisa kwa ROHO MTAKATIFU na nguvu, imetengenanisha ROHO MTAKATIFU na nguvu kwa sababu ROHO MTAKATIFU siyo nguvu za nguvu bali ROHO MTAKATIFU anazo nguvu za MUNGU, ROHO MTAKATIFU siyo upako ila anaweza akakupaka upako.
Biblia inataka tujue na Petro alikuwa anawaambia hawa watu wapate kujua ya kwamba YESU alikuwepo lakini kulikuwa na kitu kilichokuwa kinamsadia kwa ajili ya kuponya wagonjwa na alipokuwa anaponya wagonjwa hakuwa tu anaponya ugonjwa lakini alikuwa anashughulika na vyanzo vyake pia.
*MFANO:* Angalia huu mstari wa *Matendo ya Mitume 10:38* anasema _“na kuponya wote walioonewa na Ibilisi;”_ Walioonewa maana yake haikuwa halali yao/haki yao kuugua lakini wameonewa. Kwa hiyo si tu kwamba anaponya walioonewa bali anaponya na kile kilichosababisha wakaonewa
*Luka 5:17-20*
_“Ikawa siku zile mojawapo alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waalimu wa torati walikuwa wameketi hapo, waliotoka katika kila kijiji cha Galilaya, na Yudea, na Yerusalemu; na uweza wa Bwana ulikuwapo apate kuponya. Na tazama, wakaja watu wanamchukua kitandani mtu mwenye kupooza; wakataka kumpeleka ndani na kumweka mbele yake. Hata walipokosa nafasi ya kumpeleka ndani kwa ajili ya lile kundi la watu, walipanda juu ya dari wakampisha katika matofali ya juu, wakamshusha yeye na kitanda chake katikati mbele ya Yesu. Naye alipoiona imani yao, alimwambia, Ee rafiki, umesamehewa dhambi zako.”_
Hawa watu walimpelekea mgonjwa amepooza sasa hiki cha dhambi kimetoka wapi? Kwa hiyo YESU alikuwa anashughulika si tu kwa kupooza kwake bali pia chanzo cha kupooza kwake.
Kadri tunavyozidi kwenda mbele nitakuonyesha kuwa kuna wafungwa halali na kuna wafungwa walioonewa. Vivyo hivyo kuna wagonjwa halali na kuna wagonjwa walioonewa.
Kwa hiyo uweza wa MUNGU ambao upo kwa ajili ya kuponya haushughuliki tu na ugonjwa bali unashughulika pia na chanzo chake. Kwa sababu kwa MUNGU pale msalabani hakuchukua tu madhaifu na magonjwa yetu ili tupokee uponyaji alichukua madhaifu na magonjwa yetu kwa kupigwa kwa YESU tunapokea uponyaji lakini haiishii hapo anataka tuishi katika afya. Maana kuna tofauti ya uponyaji na afya, ile tu kwamba hauna ugonjwa haina maana una afya.
Msalaba haujaja tu kwa ajili ya kukuponya magonjwa yako msalaba umekuja baada ya kutuponya ukusaidie namna ya kuishi katika afya na ili uweze kuishi katika afya ni lazima ushughulike na chanzo cha ugonjwa, swali tunalotaka tujue hapa kwanini kuna sehemu ya uweza wake alioutenga mahususi kwa ajili ya kuponya magonjwa na vyanzo vyake? Ukisoma hii habari ya *Luka 5:17-27* inakupa sababu NNE kubwa.
Ni jibu la Mungu juu ya ugonjwa na madhara yake.
Tujue ya kuwa anataka na yuko tayari kutuponya magonjwa tuliyonayo.
Tujue ya kuwa anataka na yuko tayari kuponya alionao ndugu yako au rafiki yako
Anataka tujue ya kuwa tupo kwenye mazingira ya kiroho yaliyobeba uponyaji wa magonjwa ili apate kuponya magonjwa
Anatufahamisha ya kwamba upo uweza wake alioutenga kwa ajili ya kushughulika na magonjwa na vyanzo vyake sababu mojawapo akisha kufahamisha juu ya hilo na sababu mojawapo niliyokuonyesha ambayo ni ya 4 kuwa tupo kwenye mazingira ya kiroho yaliyobeba uponyaji wa magonjwa ili apate kuponya magonjwa
Na sababu zote nne zipo kwenye hii habari ya Luka 5:17-27, Biblia inazungumza Yesu alipokuwa mahali pale pamoja na kwamba sura ya nne ameeleza upako uliokuwa juu yake na majukumu yake ulikuwa na kazi ya kuhubiri, ina kazi ya kuwatangazia wafungwa msamaha, ina kazi ya kuponya, ina kazi ya kuwaacha huru waliosetwa, kutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika, ameeleza kwa uchache upo upako juu yangu ambao una majukumu mabali mabali unaona sura ya tano Biblia inaeleza hapo alikuwa akifundisha na unaona mafarisayo na waalimu wa torati walikuwa pale lakini kilichomkalisha kwenye ile nyumba sio kuponya magonjwa bali ulikuwa ni watu wanataka kusikiliza mafundisho lakini pamoja na kufundisha alikuwa amebeba upako kwa ajili ya uponyaji, waliokuwa na maswali kwenye Biblia juu ya upako wa Yesu kufundisha ulikuwa jibu kwao, kwa hiyo walipokuwa wanaenda kwa Yesu walikuwa wanatafuta jibu la maswali yao wapate kuelewa torati. Biblia inasema wakatokea watu waliokuwa wamembeba mtu aliyepooza, ingezungumzwa kwa mazingira ya sasa hivi hata Biblia hawakuwa nayo wamebeba mtu aliyepooza hawakuja kusikiliza wamekuja kutafuta jibu la ugonjwa kwa sababu walishasikia kitu ambacho Yesu alisema sura ya nne na kitu alichokifanya kipindi hicho kabla ya kufikia sura ya tano Biblia inatueleza mambo yaliyofanyika hapo inawezekana wale wanne huyu mtu aliyekuwa amepooza kwa sababu ya mazingira aliyokuwa nayo au alikuwa amesikia akajikatia tamaa kwamba labda anaponya watu wengine lakini sio mimi, au alikuwa hajasikia kabisa habari za Yesu kufuatana na mazingira aliyokuwa anaishi maana alikuwa amepooza lazima mtu ampe taarifa ndio maana nimekupa yale majibu manne kwa wakati moja ili uweze kwenda vizuri
Kwa sababu ile kwamba una upako ameutenga kwa ajili ya uponyaji wa magonjwa hiyo inakupa kujua ya kwamba Mungu analo jibu la ugonjwa ulionao. Ukishajua analojibu na saa nyingine ukasikia ya kwamba kuna mtu mwingine ambae na yeye amepokea. Lile neno la ushuhuda linaimarisha kitu ndani yako. Mnawakumbuka kwenye Biblia akina Mariam mama yake na Yesu na Elizabeth mama yake na Yohana, alietangulia kupata ujauzito ni Elizabeth, na miezi sita baadae Malaika akaenda kwa Mariam na kumueleza juu ya kubeba ujauzito wa Yesu. Elizabeth alikuwa tasa, Mariam alikuwa hamjui mume, lakini Mungu akapita na uweza wake akamsaidia Elizabeth akapata mimba kwa mume wake kwa hiyo ilipofika kwa Mariam, Mariam akasema “mimi simjui mume” akamueleza juu ya uweza wa Mungu utakavyomfunika na kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu. Akaelewa mambo mengi sana pale lakini Mariam akasema na iwe kwangu kama ulivyosema, maana yake niko tayari kubeba kwa jinsi ya kibinadamu ni ngumu sana kuamini.
Baada ya malaika kuondoka Mariamu alinyanyuka mpaka kwa akina Elizabeth, “kama Mungu amefanya kwa Elizabeth ambae alikuwa tasa basi muujiza wangu upo” alikuwa anaenda kutazama ushuhuda, kwa sababu malaika alimwambia tazama hata aliekuwa tasa Mungu amemuondolea aibu yake na amemponya.
Lakini si hilo tu kwamba Mungu analo jibu na anataka kuponya, ndio maana kwenye ile sura ya tano 5 ;17 (na uweza wa Bwana ulikuwapo ili apate kuponya) maana yake ni kwamba anataka kuonyesha utayari aliokuwa nao wa kuponya.Unaweza kwenda hospitali unaumwa ukamkuta Daktari yupo hapo na ana dawa zako nzuri na ana elimu yake nzuri, lakini hana utayari wa kukutibu na anaweza kuwa na sababu nzuri tu  anaumwa au ana kikao, kwa hiyo kutatokea kila aina ya sababu lakini ule utayari wa kukutibu haupo.
Lakini pia inawezekana pia sio wewe unaeumwa una ndugu yako anaumwa, Biblia inasema *hawa watu waliokuwa wamembeba sio tu kwamba walimbeba kwa mikono yao bali walimbeba kwa imani yao* na hiyo imani ndio iliyowapa wepesi wa kumbeba na haikukatishwa tamaa na mazingira yaliyokuweko, kwa sababu palikuwa pamejaa watu ambao walikuwa wanasikiliza mafundisho ya Yesu walipoona hamna sehemu ya kupita, na ndio maana unahitaji kuangalia ile sababu ya nne niliyokwambia kuwa “kipi kiliwafanya mpaka watoboe” ni kwa sababu kulikuwa na uweza wa Bwana lakini uko kwenye eneo fulani.
Upako unapimika, *Roho Mtakatifu yuko kila mahali lakini nguvu zake haziko kila mahali* na nguvu za uponyaji ziko kwa namna hiyo hiyo, maana na wao walitoboa dari mpaka mahali Yesu alipokuwa na Biblia inasema “Yesu alipoiona imani yao” hakuona imani ya mgonjwa, inawezekana alikuwa ameshakata tamaa, alipoona imani yao akasema “eeh rafiki umesamehewa dhambi zako” alikuwa anashughulika na chanzo cha ugonjwa ili iwe rahisi kushughulika na ugonjwa, kwa namna ya kudumu na aliposema namna hiyo yakaanza mazungumzo ya kitheolojia ya kwamba “huyu amepata wapi mamlaka ya kusamehe dhambi” alafu akasema kipengele cha pili “jitwike godoro lako uende” alipojitwika godoro wakapisha njia wakati anaingia hawakupisha njia, kitu gani kimetokea? Mahubiri yote na mafundisho yote yameharibika ukisoma ule msitari wa
*Luka. 5:26-27*
_Ushangao ukawashika wote, wakamtukuza Mungu; wakajaa hofu, wakisema, Leo tumeona mambo ya ajabu.Baada ya hayo akatoka, akaona mtoza ushuru, jina lake Lawi, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate._
Hatuambiwi alifundisha kwa dakika ngapi? Kama alianza kufundisha kwa itifaki biblia inasema alikuwa anafundisha, hii inatuonesha kuwa kilicho kuwa kinasukumwa pale ni sio kile kinachofundishwa  pale bali ni kitu cha uponyaji. Maana alipogundua kuna angalau mmoja amepata kile alichokua anatafuta hana sababu ya kuendelea kukaa pale akanyanyuka akaondoka.
Kama unanisikiliza na kama unaumwa na Mungu akakushuhudia moyoni kuwa hapa kuna nguvu ya uponyaji, usije ukafikiri kila mtu anajua. Biblia inasema imani huja kwa kusikia  wepesi wako wa kwenda kupokea  uponyaji utakuwa tofauti na mtu mwingine.  Biblia inasema tukiomba sawa sawa na  mapenzi yake tuna uhakika ya kwamba anatusikia na kama anatusikia tunazo zile haja tulizo mwomba.
Kama unajua mjini wanagawa unga na hutakuwa na shida kuondoka nyumbani na bakuli kwa sababu unaenda kuchukua unga na unajua utapewa. Ndio maana ukisoma biblia inasema walikwenda  kuponywa magonjwa yao, na haisemi walienda kuombewa magonjwa yao maana yake  walibeba na bakuli kutoka nyumbani maana wanajua aliyekuja amekuja mahususi amebeba uponyaji na yuko tayari kunipa uponyaji, akirudi nao huko alikotoka ina maana hatuhitaji na ndio maana biblia inasema waliponywa waliokuwa na haja ya kuponywa, yeye alikuwa na haja ya kutuponya. Yeye hawezi kukulazisha unga wakati wewe huhitaji unga,  labda unahitaji mchele. Wale waliokuwa Mafarisayo pale walikuwa wanatafuta mafundisho na hawa watu waliokuwa na mgonjwa walitafuta uponyaji.
Wale watumishi wa Mungu wanajua kitu ninachosema,  vitu vingine imani za namna hii zikianza kufanya kazi unabaki unashangaa.  Tulienda mkoa mmoja ambao  waliletwa vijana wa shule.  Wakati wa maombi ya mwanzoni wakati sijaanza kufundisha, mapepo yalilipuka kweli kweli.  Watoto wa shule kama 20 hivi walianguka saa hiyo,  lakini pia walikuja wamebebwa na basi maana walikuwa na shida ya kutembea.Wanatembea kama vile hapa hamna kitu  wanaenda hivi..,ilikuwa ni shule ya wasichana. Tuliomba na akawa anafunguka mmoja baada ya mwingine,  kwa hiyo nikawaachia wenzangu na nikaanza kufundisha na nilifundisha hadi nikamaliza.  Na kumbe mwishoni alibaki msichana mmoja ambaye hajapona, wenzie wote wamepona isipokuwa yeye. Kwa hiyo  walikaa pale wanawaza wakasema tunafanyaje sasa. Mwalimu mmoja alisema hivi “Haiwezekani Mwakasege ameondoka na upako wote uwanjani”, wenzake wakamtazama na wanafunzi wanamsikiliza. Alisema pale kwenye madhabahu lazima kuna upako umebaki pale. Alisema nisaidieni tumbebe huyu msichana, lile pepo likaanza kupiga kelele kuwa msinipeleke hapo wakambeba. Na giza lilikuwa tayari limeingia, wakaja wakamleta madhabahuni. Pepo likalipuka na pepo lilimwachia  akasimama kama watu wengine alikuwa ni mzima.
Sasa hiyo tulisimuliwa kesho yake. Sasa nakueleza kitu cha namna hiyo ili ujue kuwa uwanja ulikuwa mkubwa na watu wengine walikuwa wanasikia wakati tunaomba.  Sasa kitu gani kilimsukuma  yule Mwalimu ku kumleta hapa, ndipo utajua kitu gani kiliwasukuma wale watu watoboe dari. Katika ulimwengu wa roho ile nguvu iliyopo ya uponyaji si tu kwamba inaponya lakini inatengeneza mazingira ya kiroho ambayo katika hilo eneo ni rahisi sana kupokea uponyaji kwa sababu yake mazingira yapo. Yamesha tengenezwa tayari na roho Mtakatifu aliyepo pale.
Ndio maana unapofika kwenye mikutano ya namna hii au semina za namna hii  wakati nguvu za Mungu zinapita usitazame mwenzako wa kulia au kushoto kwa sababu hujui kitu kilichomleta. Mwingine ni mahali pa kukutana na girl friend  si unajua kuwa anaweza asikupate mahali popote pale ila anajua uwanjani unakuja.  Anajua unaambatana na baba au mama au shangazi au mjomba lakini atapita hapo kuja kukusalimia. Anachotafuta sio neno  bali anamtafuta girl friend.  Kwani hujajua kama watu huwa wanaulizana kuwa kwani kesho utaingia ibada ya saa ngapi?
Kasome kwenye biblia  maana inatuambia ya kuwa  kuna mafarisayo ambao walikuwa wanaenda ili wamtege kwa maneno. Kwa hiyo usifikiri kila anayekuja anakuja na nia nzuri wengine  wanakuja kupeleleza uhuru tulionao wa kusema neno. Usije ukafikri natania, nilienda mahali fulani nafundisha, walikuja watu kama 30 hivi, na walikuwa viongozi wa makanisa tofauti tofauti na wakristo  kawaida.  Baada ya lisaa limoja  akaja Askofu mmoja akanifuata sasa ni marehemu tuliwahi hubiri nae wakati fulani. Akasema Bwana  mdogo umeenda vizuri.  Nikasema kitu gani baba, akasema nilikuwa nacheki mahali  utakapokosea theolojia. Kwa hiyo mimi nimehubiri saa nzima yeye anacheki na anasahihisha kama mwalimu.
Alichopata kwenye yale mahubiri ni kuwa sijakosea theolojia, wakati kuna wengine wametoka wameokoka, na  wengine wametoka na vitu vingine lakini yeye ametoka na kusahihisha mtihani wangu wakuhubiri bila kukosea theolojia. Wengine hapa Dodoma tuliokaa nao muda mrefu mna kumbuka wakati fulani tulipokuwa na mkutano kwenye viwanja vya railway, Dada mmoja aliyekuwa ameugua muda mrefu sana. Walimpika wakadhani ana ukimwi kumbe hana lakini anaugua,  na anaumwa tu. Tulikuwa semina   pale watu wakawa wanamwambia kuwa hujasikia hapa mjini watu wanaenda kwenye semina wanapona. Akatoka mbio kuja kwenye semina alipofika hakutukuta, na tulikuwa tumefunga semina. Akarudi nyumbani anasikitika akalala alipoamka, ugonjwa wake haupo.  Kitu gani kimefanyika ni kuwa alikanyaga kwenye uwanja. Kwanini Mungu alimponya kwa namna ile hata  mimi sijui. Kuna mazingira yaliyotengenezwa, unaweza ukavuta uponyaji wako, haijalishi  watu wengine  wanamsonga songa Yesu kiasi gani maana kuna wengine hawamgusi kwa imani . Wewe gusa pindo vuta muujiza wako.
Usije ukafikiri wale watu waliokuwa wanamkaribia Yesu walikuwa wanataka kupona kuna wengine walikuwa wanataka kuangalia tu nguo yake kama imenyooshwa. Haleluyaaaa..
Kuna wamama hapa wana uvimbe. …
TEMBELEA YOUTUBE KUSIKILIZA MAOMBI UPOKEE UPONYAJI KWA LINK PALE JUU..☝☝
Tuonane tena Kesho ✋✋✋✋✋✋
[09:26, 09/05/2018] Filix Bwanji: *2⃣SEMINA YA NENO LA MUNGU-DODOMA UWANJA WA BARAFU*

*MWL.CHRISTOPHER MWAKASEGE*
*SOMO: UWEZO WA MUNGU JUU YA MAGONJWA NA VYANZO VYAKE.*
*TAREHE  07 MAY, 2018*
*SIKU YA PILI*
*👉 NAMBA ZA SADAKA* https://goo.gl/Z3ozYB
*👉LINK YA SEMINA YA LEO YOUTUBE* https://youtu.be/gsOR6TBasaA
*👉NAMNA YA KUPATA CD&DVD BONYEZA HAPA* https://goo.gl/tgwoub
*Luka 5:17*
_“Ikawa siku zile mojawapo alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waalimu wa torati walikuwa wameketi hapo, waliotoka katika kila kijiji cha Galilaya, na Yudea, na Yerusalemu; na uweza wa Bwana ulikuwapo apate kuponya.”_
Jana tulikuwa tunajibu hilo swali _*“kwanini MUNGU anataka tujue ya kwamba uweza wake upo, siyo kwamba Yesu tu yupo lakini pia uweza wake upo”*_ na tuliangalia sababu kadha wa kadha.
Leo kwa kuongezea sababu nyingine ya Mungu kutaka ujue ya kwamba uwepo wake upo ni:-
*IMANI YAKO IPATE KUONGEZEKA, SI TU JUU YA YESU PIA JUU YA UWEZA WAKE.*
Inawezekana unamwamini Yesu ila huamini ipasavyo juu ya uweza wake na kwa sababu hiyo Biblia inataka tujue uweza wake unakuwepo. Imani inapoongezeka juu ya uweza ambao Yesu anao, inakuwa rahisi sana kwako kwenda kwake kupokea kitu ambacho uweza wake unakabidhi kwako.
Mfano:
Kwa wale wanaofuatilia simu za mkononi, huangalia uweza wake, haitoshi tu kuamini simu atataka kujua na uweza wake. Kwa hiyo wale wanaouza hawatangazi tu wanauza simu bali na uweza uliopo kwenye simu ili mnunuzi aweke imani yake kwenye uweza uliopo ndani ya simu, ili unaponunua ujue utakachopata kuhusiana na uwezo uliopo wa kufanya kazi hasa kamera yake.
Na kwa sababu hiyo ile tu unamwamini Yesu haitoshi lazima utuambie Yesu kabeba nini, amekuja na nini, damu yake ikoje na jina lake ikoje, Roho Mtakatifu aliembeba yukoje, neno lake likoje ili kusudi imani yako kwa Yesu pia uweke kwenye Neno, Damu, Jina lake na kwenye uwepo wa Mungu ambao unatembea pamoja naye; ambao yeye mwenyewe alisema _“Roho wa Bwana yu juu yangu amenitia mafuta kuwahubiri na kutangaza na kuweka huru na kuponya”._
Kama hujui uweza uliopo ndani ya chochote unachohitaji unauliza uweza uliopo ndani (sio vibaya kufahamu) kama tunavyouliza kuhusu simu na kwenye Biblia ni hivyo hivyo tafuta wanaojua kutumia Biblia watakuonyesha uweza wa Yesu.
Leo tuzungumzie kidogo katika *UHUSIANO WA NEEMA, IMANI NA REHEMA JUU YA UWEZA WA UPONYAJI WA MUNGU*
*Waefeso 2:8*
_“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;”_
👉Neema inatoa, imani Inapokea.
👉Neema inaachilia kitu, imani inachukua kilichoachiliwa na neema.
👉Neema inaachilia wokovu, imani inachukua wokovu.
Sasa ukienda kwenye Biblia kuangalia jinsi Neema ilivyotumika, imetumika kwa style tofauti tofauti lakini ukiona neema ina maana za jumla unahitaji kujua.
👉Neema maana yake ni kuwekewa kitu ambacho unahitaji bila ya wewe kushiriki kukiandaa. Biblia imeita neema kipawa/zawadi ya Mungu
👉Neema maana yake ni kupewa kitu unachohitaji wakati ulikuwa hustahili kupewa. Neema inakuwepo (available) kwa ajili yako, hustahili lakini imewekwa kwa ajili yako.
👉Neema ni kupewa kitu ambacho si haki yako kupewa.
Na ndani ya Biblia utakuta kuna tafsiri/maana tofauti tofauti juu ya neema, na ndiyo maana ukisoma utaanza kuelewa kwanini Biblia imezungumza juu ya kuitwa kwetu/wito wetu ni kwa NEEMA.
Akishasema ni kwa neema maana yake hatukustahili/haikuwa haki yako, lakini neema yake ndiyo imeita na imani yako ndiyo inatakiwa ipokee wito. Msalaba unaachilia Neema lakini huwezi ukalazimishwa kuchukua.
Neema ya Mungu ikiachiliwa inafundisha pia, lakini huwezi kulazimishwa au kulazimika kuchukua yale mafundisho.
Na Neema ya Mungu iliachilia uponyaji pale msalabani, imani inachukua. Imani ni mkono/kiungio.
Unaposoma kwenye Biblia na kuanza kuangalia/kutazama neno Imani lilivyotumika kwenye Uponyaji (maana limetuma kwenye maeneo mengi Mf: Biblia inasema mwenye haki wangu ataishi kwa Imani na hata kuishi kwetu  maisha yetu yote tunatakiwa kuishi kwa Imani)
Kwa hiyo inapofika kwenye masuala ya uponyaji tafsiri ya Imani ambayo inaweza kuwa kuwa ni rahisi sana maana yake ni hii:-
*TAFSIRI YA KWANZA*
Imani ni uhakika wa kuwepo kitu kile unachokitarajia unaokufanya uende kukichukua.
*Waebrania 11:1*
_“Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.”_
Maana yake sasa unakuwa na uhakika na kitu unachokitarajia. Kukitarajia maana yake hakipo saa hiyo ndiyo maana unakitarajia, na unapata uhakika saa hiyo hicho unachokihitaji kipo, na kwa sababu kipo ndiyo maana Biblia inasema ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Na kwa sababu hiyo Imani ule uhakika unatengenezea picha, unaona ndani ya moyo wako kile unachokihitaji. Kwa hiyo kama unahitaji uponyaji imani inakuponyesha uponyaji ndani ya moyo wako kabla hujaona uponyaji ndani ya mwili wako.
Kwa hiyo huo uhakika unakusukuma kuchukua hatua ya kwenda kuchukua hicho unachokitarajia, na ndiyo maana Biblia inasema Imani isipokuwa na matendo haizai/imekufa nafsini mwake.
*TAFSIRI YA PILI*
Imani maana yake ni uhakika unaoupata kutoka katika NENO la Biblia juu ya kuwepo kile unachokihitaji. Huo uhakika unakusukuma kuchukua hatua ya kwenda kukichukua kile unachokihitaji.
Huwezi kuwa na uhakika na usichukue hatua. Ukiwa na uhakika na usichukue hatua inamaanisha kuna kitu bado unahitaji kufuatilia, maana ule uhakika lazima ufike mahali na kuondoka, kile aina ya tashwishwi ndani yako na ndiyo maana Biblia inasema yoyote myaombayo mkisali aminini ya kwamba mnayapokea nayo yatakuwa yenu, na inaongezea kusema yeyote atakaye uambia mlima huu ng’oka ukatupwe baharini wala asione shaka moyoni mwake (maana yake awe na uhakika)
Uhakika huu unaoitwa imani unaondoa:-
-nia mbili ndani yako,
-kusita,
-hofu,
-aibu,
-unavunjwa mipaka ambayo ingekukwamisha.
Biblia inasema hakuna lisilowezekana kwake yeye aaminiye, ni sentensi nzito kimatendo lakini hiyo imani ikiisha kaa ndani yako (sasa ondoka hilo neno imani weka uhakika=yaani huo uhakika ukiisha kaa ndani yako), ndani yako utasukumwa kuanza kuchukua hatua kwa sababu neema imeshaachilia kitu kipo.
Ukiachilia Imani upande huu/mwingine kwa ajili ya kupata kile kilichokitarajiwa upande huu/mwingine uweza wa MUNGU unaingilia kati kuhakikisha ya kwamba unavuta kitu kilichopo upande mmoja ili kiweze kutokea upande mwingine, maana imani inasukuma hicho kitu kutokea.
*Warumi 10:17*
_“Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.”_
Nimekusomea neno hilo la warumi kwa sababu wakati wenzetu wanatembelewa na YESU kwenye miji yao na vijiji vyao hawakuwa na Biblia maana baadhi ya masinagogi yalikuwa na chuo cha Nabii Isaya , sinagogi lingine unakuta wana kitabu kingine (Mf; Kitabu cha Wafalme) hawakuwahi kuwa na Biblia kamili kama tuliyonayo sisi. Kwa hiyo walikuwa wanategemea NENO LA MUNGU lililokuwa linatoka kwenye vinywa vya watumishi wakiamini ya kwamba ni NENO LA MUNGU.
Na lile NENO lilipokuwa linashuka likuwa linaachilia kitu kinachoitwa Imani. Walikuwa wanategemea neno la ushuhuda ambalo lilikuwa linashuhudia matendo makuu ya MUNGU, na ndiyo maana Daudi anasema shuhuda zako ndizo ninazo zitafakari kitandani mwangu. Shuhuda kazi yake ni kuinua imani yako ili uweze kuona kile unachokitafakari ni MUNGU kafanya hajabadilika ni yeye yule jana na leo hata milele anaweza akakufanyia na wewe.
Ndivyo walivyokuwa wanaenda wakati ule. Lakini wakati huu tuna cha zaidi maana tuna maandiko. Unaweza usisikie mahali popote mtu amepona ugonjwa ulionao au unaweza usisikie MUNGU kamfanyia mtu mwingine yeyote lakini ukaenda kwenye Biblia ukaona kuna NENO linalosemwa juu ya jambo hilo endelea kutafakari hilo NENO mpaka litengeneze ndani yako uhakika, maana yake linakutengenezea kujua ya kwamba hicho ni cha kwako.
Ukiokoka lazima uwe na uhakika wa mambo mawili au vitu viwili
Msamaha
Wokovu uliopokea
Usipokuwa na uhakika utayumbishwa. Kama umeenda kwa MUNGU kutubu lazima uwe na uhakika ndani yako ya kwamba umesamehewa dhambi zako na pia uwe na uhakika wa kile ulichopokea moyoni mwako ulipomkaribisha YESU. Ukishakuwa na uhakika  wa namna hiyo ile imani inakusimamisha mahali kiasi ambacho mtu kesho akikuambia hujaokoka unamshangaa, kwa sababu hawezi kubadilisha ulicho nacho.
Na kwa sababu hiyo nitatembea na uhakika kwa hiyo mtu hawezi kuja na mafundisho yake akaniambia ukitaka kuokoka sawa sawa, unamuuliza kuokoka sawa sawa maana yake nini? Sasa kama huna Neno la kutosha ndani yako itakusumbua usiku na mchana ningeweza kukuonesha mistari mingi sana  ‘Biblia inasema
*Warumi 5:1-2*
_Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na muwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu._
Kitu gani ninachotaka uone  tukisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani na muwe na amani, Imani ilipo na amani ipo, uhakika unapokuja ndani yako unapata utulivu ambao hauna namna ya kumueleza mtu mwingine unakusukuma kuchukua hatua ambayo mtu mwingine hawezi kuelewa,   unasikia uhakika kwamba Mungu amekuita kwa ajili ya kuhubiri haijalishi una kigugumizi utatafuta Biblia, utatafuta madhabahu wanakuambia hujui kuongea unawambia najua sijui kuongea lakini huku ndani nina uhakika Mungu amesema niongee watasema utajuaje, unawaambia mimi sijui nipeni madhabahu ukisimama unakuta kile kigugumizi kimepotea nimeona watu wa namna hiyo ambao najua wana kigugumizi lakini Mungu kamwekea wito huku ndani ambao hawezi kunyamaza nao akivuka kile kizingiti akavuka hatua kwa sababu ya uhakika aliokuwa nao akichukua Biblia akifungua kinywa kigugumizi hakipo .
Sasa ngoja nikupe maana ya Rehema halafu nikupe shuhuda chache.
*Rehema maana yake* ni  _Mungu kukusaidia kupata kilichotolewa na neema bila imani ya mtu kutumika_
Kwa hiyo Mungu anametengeneza namna ambayo huna imani iko rehema kwa sababu neema imeshaachiliwa imani ina umuhimu wake kwa sababu ukipokea kwa imani unatunza kwa imani lakini kama huna imani kabisa na hakuna mtu mwingine jirani ambaye wanaweza akasimama kwa imani pamoja na wewe au kwa niaba yako kuna rehema za Mungu.
*Luke 5:17-25* inazungumza Yesu alikuwa akifundisha mahali na uwepo wa Bwana ulikuwepo pale ili apate kuponya mpaka yule mtu aliyepooza alipokuja hakukuwepo na mtu aliyehitaji uponyaji lakini wale watu walikuwa na imani maana yake kile tulichokuwa tunakitafuta kwa ajili ya ndugu yetu kupona kiko hapa. Biblia inazungumza kile ambacho Yesu alikisema katika ule mstari wa 20 *Naye alipoona imani yao*  kilichosukuma Yesu kutumia ule uweza uliokuwa nao kwa ajili ya uponyaji na msamaha kwa Yule mtu ni imani aliyoiona kwanza kwa Wenzake, imani maana yake nini, cheki tulikotoka ni kuwa na uhakika ya kwamba kile unachokitarajia kipo na ndicho kilichowasukuma kumleta huyo mtu ndio maana nilikuambia kama kipo hapa haijalishi hata kama kuna kizuizi gani huwezi kuondoka utatoboa tu kwa sababu una uhakika unachokihitaji kipo hapo. Wale watu walikuwa na uhakika wakimteremsha huyo mtu hapo apokee uponyaji atapokea walimbeba tokea nyumbani hawakuja kwa kubahatisha walikuwa na uhakika, walikuwa na uhakika na uponyaji, hatua zao na matendo yao yalikuwa yanaonesha imani waliyonayo ndio maana Biblia inasema alipoiona imani yao! Akaenda kushughulika moja kwa moja na chanzo cha ugonjwa rafiki umesamehewa dhambi zako! Wakaanza kupata shida waliokuwa wanamsikiliza wameshasahau mafundisho mazuri aliyokuwa akiwafundisha. Sasa baada ya kushughulikia hayo mabishano walikuwa nayo juu ya uweza wake kusamehe dhambi ule mstari wa 24
_Lakini, mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (alimwambia yule mwenye kupooza). Nakuambia, Ondoka, ujitwike kitanda chako, ukaende zako nyumbani kwako.Mara hiyo akasimama mbele yao, akajitwika kile alichokilalia, akaenda zake nyumbani kwake, huku akimtukuza Mungu._
Huyu ni mtu ambaye amekuja amebebwa kwa misingi ya kibinadamu na kibiologia hawezi kutembea, kateremshwa na godoro lake kule, kilichosukuma Yesu kuingia kazini ni ile imani alioiona kwa wenzake maana angeweza kushughulika na imani aliyokuwa nayo huyu kwanza lakini Biblia inasema aliiona imani ya wale wengine labda huyu mwingine alikuwa amechoka, hawezi kwenda anaona usumbufu lakini wale wenzake wakasema hujui kitu tulichoona alipofika pale Yale mazingira yalikuwa charged na uhakika wa uponyaji yalikuwa mazingira ya imani ndio maana Biblia inasema alishangaa sana alipoenda kwao anaponya wagonjwa wachache na hakufanya muujiza wowote kule akashangaa sana kwa kutokuamini kwao, maana yake mazingira yaliyokuwepo yalimzuia kufanya vitu vingi lakini Yale mazingira yaliyokuwa kwenye ile nyumba yalikuwa charged na imani na ndio maana wanapokuja watu ambao wanauhakika na kitu wanachoenda kufanya ghafla ulimwengu wa Roho unaachilia mvuto ambao wanavuta na kuachilia uponyaji ndio maana huyu mwingine aliyekuwa amebebwa ndani yake kapata uhakika ambao kwa jinsi ya kibinadamu hana namna ya kueleza maana aliambiwa ondoka uende jitwike godoro lako uende! Biblia inasema mara hiyo, hakufikiri mara mbili hakusema nimeugua mda mrefu hakusema nina x-ray zinaonyesha mifupa yangu haiwezi kufanya kazi, hakusema nina vipimo vya M.R.I, misuli yangu haifanyi kazi lakini alikuwa na uhakika ndani huyu mtu aliyeniambia nyanyuka ana uhakika na kitu anachosema kwa hiyo akanyanyuka na alipochukua tu hatua nguvu za Mungu zikaingia kazini.
Ndicho ambacho akina Petro walikifanya kwa mtu ambaye alikuwa kiwete tangu kuzaliwa kwake, Biblia inasema hatuna pesa wala dhahabu lakini tukupacho ndicho tulichonacho simama uende! Kwa jina la Yesu akamshika na vifundo vyake vikatiwa nguvu akanyanyuka hapo mara moja Imani yao ilionekana katika matendo yao.
*Mathayo 8:5-13*
_Na alipoingia Kapernaumu, afisa mmoja alimjia,  akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana. Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye. Yule afisa akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona. Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya. Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa yeyote katika Israeli. Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Abrahamu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni; bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. *Naye Yesu akamwambia yule afisa, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini.* Mtumishi wake akapona wakati ule ule._
Ule mfano mwingine wa Luka sura ya 5 na wao walikuwa na mtu mwingine wakambeba, wakampeleka kwa Yesu, huyu akida na yeye alikuwa na mtu aliepooza nyumbani hakumbeba akaenda yeye na alipopewa ile taarifa Yesu akasema nitakuja nimponye, yule akida akasema
_“Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona. Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya”_  angalia ule msitari wa 13._*Naye Yesu akamwambia yule afisa, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini.*_
Haikuwa imani ya Yesu,Yesu alikuwa pale kwa ajili ya kutumia nafasi aliyokuwa na neema iliyokuwa juu yake na uwepo wa Bwana uliokuwa mahali pale, sasa kitu gani kilichotofautisha IMANI walizopokea. Kitu gani kilichowasukuma watu wale waliombeba hawakuwa hata na gari, Biblia haituambii kama walitumia usafiri lakini walimbeba na akapokea uponyaji na huyu mwingine alikuwa ni askari  angeweza kuwatuma maaskari wamsaidie kumbeba lakini imani aliyokuwa nayo ndio iliyomsukuma. Alikuwa na uhakika katika ngazi nyingine ya amri na mamlaka na nafasi ambayo Yesu alikuwa nayo maana yake  ni kwamba YESU alikuwa tayari kukatisha safari zake aende nae nyumbani.
Lakini unajua ni kitu cha ajabu sana maana inataka kupokea kwa jinsi ilivyoamini kwa hiyo wakati Yesu anataka kuja nyumbani inasema “nilichokuletea hapo sio kwenda kumtafuta Yesu aje aende kwako bali kumwambia aseme neno tu na mtumishi wangu atapona” kwa sababu kuna mamlaka ya neno na ya nafasi. Yesu akashangaa sana akasema “sijawahi ona imani kubwa namna hiyo” sasa sikia, hata kwa wale wengine alisema hivyo maana aliiona kwenye matendo kwa huyu ameiona imani kwenye maneno.
Huwezi kujua nguvu za maneno zinavyokuwa, ambayo unaachilia kati kati ya imani. Na wakati yule akida anakata kona tu kurudi kwake na yule mtoto wake alipona wakati ule ule, *Imani inaua muda na inaua umbali kwa sababu IMANI ni,yaani sasa kile ambacho unakitarajia kesho imani inasema uwe na uhakika sasa* unapoanza kuweka kwenye matendo ni kwa ajili ya kufuatilia kupokea. Yule akida alipopokea yeye maana alisimama kama muombaji, kwa hiyo imani yake ilimsaidia mgonjwa kupona.
Maana unaweza kuonyesha imani yako kwa Mungu, Maana hata yule mama aliyekuwa anatokwa na damu miaka mingi alikuwa amezungukwa na watu wa dini na alisema moyoni mwake “nikigusa tu pindo la vazi lake tu” kwa sababu waliokuwa wanatokwa na damu kwa staili hiyo walikuwa najisi hawaruhusiwi kukaa na watu na mali zake ziliisha kwa sababu ya kuhangaika na waganga wa kienyeji kila mtu alijua pale mjini  juu yake na alitengwa na jamii miaka 12, aliposikia habari za Yesu imani yake ilinyanyuka na akasema moyoni mwake “nikigusa tu pindo la vazi lake nitapona” sasa aliposema namna hiyo ghafla imani yake ikanyanyuka ikawa na uhakika kwa hiyo ilimbidi afuatilie kwenda kupokea kwa hiyo ilikuwa ni lazima atoke nyumbani mpaka kwa Yesu. Maana alimsikia Yesu juu ya habari zake. Usije ukafikiri kilikuwa ni kitu chepesi kufuatilia vazi la kikuhani na namna ya kupenye mpaka kumfikia Yesu na alipogusa namna hiyo ghafla kitoto kichanga kikaruka ndani  yake, na alipogusa tu nguvu za Yesu zikatoka mpaka ndani yake na zikakausha damu saa hiyo hiyo na ile imani  ilikuwa na nguvu kiasi ambacho Yesu alisikia akasema “nani amenigusa” wanafunzi wake wakasema “wanakugusa watu wengi namna hii” akasema kuna mguso tofauti uliotoka na kitu” na yule mama alipojieleza alijieleza akijua kuwa viongozi wake wa dini wanasikia, wangeweza mpiga mawe saa hiyo  na angerudi kanisani wangeweza mtenga, lakini alisema nimepata basi, kama watanitenga sawa, hata kama wakinipiga kwa mawe nina ushuhuda wa dakika mbili. Usije ukafikiri kilikuwa ni kitu chepesi maana hujui dini zinavyofanya kazi, akaishia kusema ushuhuda wake wote akitetemea.
Kasome biblia  yako alieleza ushuhuda wake akitetemeka, Yesu alimwambia enenda zako kwa amani maana alikuwa na imani lakini alikuwa hana amani kwa sababu ya dini yake itasemaje. Mungu aliamua kumpa mara mbili, akampa uponyaji na amani juu. Ukienda kwenye biblia  ukitafuta mifano tofauti tofauti utapata.
*Mathayo 8:14-17*
_Hata Yesu alipofika nyumbani kwa Petro, akamwona mkwe wa Petro, mamaye mkewe, amelala kitandani hawezi homa. Akamgusa mkono, homa ikamwacha; naye akaondoka, akawatumikia. Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi, ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu._
Nataka uone rehema, huoni hapa Yesu akisema mama mkwe wa Petro kuwa imani yako imekuponya au hamwambii Petro kuwa sawa sawa na imani yako juu ya uponyaji wa imani yako sawa sawa na mama mkwe wako upokee. Biblia inasema alikaribishwa tu hapo nyumbani Kapernaum maana Petro ndio alikuwa na nyumba yake hapo  labda ilikuwa apumzike kidogo na hakusema kama anataka kuombewa au Yesu kumuuliza Petro kuwa kwanini hujaniambia kuwa mama mkwe wako anaumwa,  lakini alimgusa na homa ikamwacha, hamna imani inayohusika kwa jinsi hii, sasa utajiuliza kitu gani kilikuwa kazini,  ni rehema.
Biblia inasema kutokea hapo walimletea watu waliokuwa na mapepo na magonjwa wote akawaponya. Sio kwamba walikuwa na imani hapana,  ni ili litimie neno  kwake lililonenwa na  nabii ya kwamba alichukua madhaifu yetu na magonjwa yetu, ina maana anaachilia. Kuna saa nyingine mtu anatafuta Rehema wakati Mungu anadai imani. Wale vipofu waliokuwa wanamkimbilia Yesu alikuwa anasema ee mwana wa Adam uturehemu akasema mnaamini kuwa ninaweza kufanya haya,?. Wao walikuwa wanatafuta rehema wakati Yesu anatafuta imani.  Sasa waliposema kuwa tunaamini Yesu akawaambia kuwa kwa kadri ya imani yenu mpokee. Tunakwenda sawa sawa?
Usipate shida sana  kuwa kuna mtu wala hajali wala haombi lakini anakuja kwenye mkutano anapona. Wewe umekuja na unakazana  kufunga na kuomba lakini unaondoka na ugonjwa wako, na unasema lazima Mungu anaupendeleo. Nilitaka nikuonyeshe kidogo.  Nguvu za Mungu hizo hizo zinachilia neema na kuweka uponyaji, lakini uponyaji upo na ndio maana uponyaji huwezi kununua. Sasa usije shangaa na kuanza kusema kuwa nimetoa na sadaka zangu lakini nashangaa siponi, sasa ulikuwa unataka  kununua uponyaji kwa sadaka?.
Saa nyingine Mungu ananyamaza makusudi ili usije ukasema sadaka yangu  ikanisaidia nikapona. Sasa wasio na sadaka wataponea wapi? Sadaka ina sehemu yake, lakini mtu yeyote asikuambie kuwa kitu chochote kilichotolewa msalabani kuwa kinaweza nunuliwa kwa sadaka.  Neema ya Mungu imeachiliwa na huwezi nunua wokovu kwa sadaka yako. Kornelio alitoa sadaka lakini aliambiwa akamtafute  Petro. Hakuwa ananunua  wokovu maana ile sadaka ilikuwa inapeleka ujumbe kwa Bwana, sadaka inapeleka moyo wako kwa Bwana. Lakini haiwezi kununua kitu ambacho neema ya Bwana imeweka mezani.
Huwa tunawaambia watu usije ukaiga imani ya mtu, wacha ijengeke ya kwako, na nimekueleza kuwa unaweza simama kwa niaba ya mtu mwingine na Mungu akamponya kama nilivyokuonesha. Tulikuwa  shinyanga nikaita watu waliokuwa na shida ya masikio. Watu walijipanga mbele, na akaja kijana mmoja,  akasimama akanyosha mkono.  Nikamuuliza una shida gani akasema  mimi nimesimama kwa niaba ya mama yangu. Nikamuuliza yuko wapi akasema yuko Tabora.  Akasema hasikii sikio moja, nikamwambia  shika sikio lako ambalo ndio mama yako linamsumbua. Baada ya maombi pale maana tuliombea na watu wengine.  Sasa nikamwambia cheki na mama yako, kesho alirudi kutuambia na alitueleza jinsi alivyompigia mama yake simu. Mama yake alipokea na sikio lile ambalo ndio alijua anasikia lakini yule kijana akamwambia kuwa nilikuwa uwanjani leo kwenye maombi na nikashika sikio kwa niaba yako na nina imani kuwa Mungu amekuponya. Sasa weka simu kwenye sikio ambalo lilikuwa halisikii basi, akaweka na alipoongea nae akawa anasikia kabisa. Imani inaua umbali kabisa.  Ndio maana usijaribu kuiga imani ya mwenzako.
Kuna mmoja alikuwa na ukimwi na alikuwa anakuja Arusha ili kututafuta kwa ajili ya maombi  na alipofika mkoa fulani  mahali, nguvu zilimuishia  akatafuta  baadhi ya ndugu ambao wako mahali hapo akapumzika. Sasa alipokuwa amelala kitandani alisikia kuwa tunaenda na semina mkoa ule, lakini ilikuwa iko mbali kidogo,na alitusimulia saa hiyo ni mzima anasema nilikuwa nasubiri niwape ushuhuda niondoke.  Akatazama gazeti moja  na lilikuwa na Tangazo na picha ya kwetu. Akachukua picha akakata akaitisha chai ya rangi, katumbukiza karatasi iliyokuwa na picha ya kwetu, akakakoroga mpaka ikalainika yote akanywa, ghafla baada ya  muda akapata nguvu saa tunakutana nae alisema alikuwa anasubiri atupe ushuhuda. Sihitaji tena uponyaji,  Bwana Yesu  ameniponya.. sasa huhitaji kutafuta picha za kwetu kila  mahali, ndio maana usiige, lasivyo ni sawa sawa na kumwambia Yesu kuwa kila kipofu amkorogee matope ateme mate. Alafu asilibe. Nakueleza jinsi Mungu anavyotengeza imani ndani ya mtu. Na mtu akipata uhakika,anapokea.
Nenda YOU TUBE sikiliza maombi  ili upokee uponyaji wako. … Bonyeza link pale juu..
[08:41, 10/05/2018] Filix Bwanji: *3⃣SEMINA YA NENO LA MUNGU-DODOMA UWANJA WA BARAFU*
*MWL.CHRISTOPHER MWAKASEGE*
*SOMO: UWEZO WA MUNGU JUU YA MAGONJWA NA VYANZO VYAKE.*
*TAREHE  08 MAY, 2018*
*SIKU YA TATU*
*👉LINK YA SEMINA YA LEO YOUTUBE* https://youtu.be/3Ddu2ZavFww
*👉 NAMBA ZA SADAKA* https://goo.gl/Z3ozYB
*👉NAMNA YA KUPATA CD&DVD BONYEZA HAPA* https://goo.gl/tgwoub
Leo ikiwa ni siku ya tatu tuangalie
*UWEZA WA MUNGU JUU YA MAGONJWA AMBAYO CHANZO CHAKE NI MAPEPO*
Na somo hili kwa leo tuangalie kwa mtiririko ufuatao kwa ngazi yoyote uliyonayo ya uelewa wa Biblia ili uweze kupokea.
*JAMBO LA KWANZA*
1.SI KILA UGONJWA CHANZO CHAKE NI MAPEPO.
Marko 1:32‭-‬34
Hata kulipokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa, walikuwa wakimletea wote waliokuwa wagonjwa, na wenye pepo. Na mji wote ulikuwa umekusanyika mlangoni. Akaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua.
Mahali pengine Biblia inasema walimpelekea waliokuwa hawawezi maana yake walikuwa wagonjwa lakini pia walimpelekea waliokuwa na mapepo. Biblia inazungumzia juu ya uponyaji kwa wale ambao walikuwa wana magonjwa mbalimbali lakini pia wale wenye mapepo walitolewa mapepo.
Nakueleza hii kwa sababu saa nyingine unapokutana na shida za magonjwa ni rahisi sana ukaenda upande mmoja ukasema magonjwa yote chanzo chake ni mapepo lakini Biblia haisemi hivyo. Biblia inasema kuna magonjwa chanzo chake ni mapepo na si kila ugonjwa chanzo chake ni mapepo. Na makundi haya yanatofautiana na kuhudumiwa kwao kuko tofauti.
*JAMBO LA PILI*
*2. KUNA MAGONJWA AMBAYO CHANZO CHAKE NI MAPEPO*
Ili huyu mwenye ugonjwa wa pepo/mapepo apone lazima mapepo yatolewe kabla hajapokea uponyaji wake.
Hili tuliangalie kwa mifano kadhaa kama ifuatavyo:-
MFANO WA KWANZA
*I. Luka 4: 38 - 39*
_“Akatoka katika sinagogi, akaingia katika nyumba ya Simoni. Naye mkwewe Simoni, mamaye mkewe, alikuwa ameshikwa na homa kali, wakamwomba kwa ajili yake. Akasimama karibu naye, akaikemea ile homa, ikamwacha; mara hiyo akainuka, akawatumikia.”_
Si kila aliyeandika habari hii, ameandika jinsi Luka alivyoandika. Sijajua kwa sababu yeye ni daktari kuna vitu ambavyo alikuwa anaviona kuhusu uponyaji. Ukisoma kitabu cha Luka habari zile zile kwa magonjwa ambae Yesu alikuwa anamhudumia, kuna vitu Luka ameandika lakini wengine hawajaandika. Kama wewe msomaji wa Biblia angalia uone hiyo labda alitazama kwa jicho la daktari na aliona vitu vingine ambavyo wenzake hawajaviona. Kwa sababu hapa anaandika ya kwamba Yesu alisimama karibu na mama mkwe wa Petro na kuikemea ile homa, ikamwacha.
Biblia inasema homa kali haituambii homa ipi. Homa kali ni matokeo ya kitu kingine kilichopo ndani ya mwili lakini hii homa ni ya ajabu sana kwa sababu inasikia “akaikemea ikasikia na ikamwacha”. Kwa hiyo inaonesha ya kwamba hii homa ambayo ni roho au ni roho iliyobeba homa na kwa lugha tuliyozoea tungesema ni pepo lililobeba homa na alipolikemea likasikia, na lilipoondoka na homa ikaondoka.
Kwa sababu chanzo cha homa ni pepo utaona Yesu akishughulikia pepo kwanza na baada ya pepo kuondoka na ule ugonjwa unaondoka.
Kwa hiyo ukikemea pepo likatoka saa hiyo hiyo au mapepo yakalipuka saa hiyo hiyo na kumuacha, usije ukaanza kutafuta watu wote wenye homa ukafikiri nayo ni mapepo.
MFANO WA PILI
*II. Mathayo 9:32-33*
_“Hata hao walipokuwa wakitoka, tazama, walimletea mtu bubu mwenye pepo. Na pepo alipotolewa, yule bubu alinena, makutano wakastajabu, wakasema, Haijaonekana hivi katika Israeli wakati wo wote.”_
Huyu alikuwa na shida ya kuongea (bubu) na Biblia imeweka wazi kabisa ya kwamba ni bubu mwenye pepo. Sasa si kila bubu ana pepo. Lakini huyu tunayemsoma alikuwa na pepo na kufuatana kwa jinsi alivyo hudumiwa katika uponyaji wake Biblia inasema pepo alipotolewa yule bubu alinena. Kwa hiyo ina maanisha chanzo cha ububu wake ni yule pepo aliyekuwa ndani yake. YESU hakushughulikia ububu alishughulikia lile pepo lililokuwa ndani yake.
Mambo haya ukianza kuyafahamu kidogo kidogo na kuyafanyia mazoezi/kazi mara kwa mara utaanza kuona matokeo. Shida kubwa sana ya watu inapofika kwenye kuomba wanaogopa kushindwa. Sasa huwezi kuwa mwanafunzi kama unaogopa kushindwa. Kwa hiyo inapofika kwenye kuombea wagonjwa kisikusumbue kuona hajapona, wewe rudi kwa YESU na kumuuliza mbona hajapona, nakueleza haya ili kukutia moyo ili uweze kujua hivi vitu.
*USHUHUDA*
Tulienda mkoa mmoja na sijajua ni nini kilikuwa kinaendelea kwenye ule mkoa. Viongozi wanahusika kwenye mambo ya usalama hawakuwa na uhakika kama waturuhusu kuendelea kufanya semina au la, kulikuwa na ugomvi fulani wa kidini sijui hata ulikuwa umetokea wapi, tukazungumza nao na mwishoni wakatukubalia kufanya semina pamoja na kutupa ulinzi wa kutosha. Sasa sisi hatukujua kilichokuwa kinaendelea maana tulifika kwenye mji jana yake tukaelezwa tu na hatukujua kwamba kimefikia kwenye ngazi ya namna hiyo, na hivyo hawakujua kama watakaofika kwenye semina watakuwa na nia nzuri au mbaya ambacho ni sahihi kabisa kwa wenzetu wanaoshughulika na masuala ya usalama, nasi tulimshukuru MUNGU kwamba walituruhusu kufanya semina chini ya ulinzi mkali. Na tulikuwa tunafanyia ndani ya kanisa, siku ya kwanza watu walikuja wengi sana wamejaa ndani na nje. Nikaita wagonjwa waje mbele kuombewa, nikaanza kupita kuombea nikiuliza mmoja mmoja anachoumwa halafu namwombea. Nikafika kwa mama mmoja alikuwa na msichana mdogo kama miaka 8 hivi nikauliza nani ana shida wewe au mtoto? Akasema mtoto, nikauliza wa nani? Akasema wa kwangu, nikauliza ana shida gani? Akasema hasikii, nikamuuliza kutoka lini? Akasema, toka anasoma shule yuko darasa la tatu walimu walinipigia simu wakasema ghafla mtoto wako hasikii, akasema nilienda kumchukua nimezunguka kila hospitali hawaoni ugonjwa lakini hasikii. Nikamuuliza mtoto anaitwa nani? Akanitajia jina, sasa tuko live(mubashara) wakati huo na jina lilikuwa si la mkristo watu wote walitega sikio, nikauliza swali lingine, unaamini ya kwamba YESU anaweza akaponya mtoto wako? Akasema ndiyo nina amini, na mimi nikasema na iwe kwako kama ulivyoamini. Nikaweka vidole vyangu kwenye masikio ya yule mtoto nikakemea pepo kiziwi kumuachia yule mtoto na kuamuru yalel masikio yaanze kusikia tena halafu nikatoa vidole vyangu. Nikaita jina la yule mtoto akaitika saa hiyo hiyo.
Kwanini nakueleza mambo haya, nataka ujue ya kwamba kilichomfanya huyu mtoto kuwa kiziwi kwa muda wote huo haukuwa tu ugonjwa wa kawaida. Sasa si kila kiziwi ana shida hiyo. Lakini ROHO MTAKATIFU alinisemesha ya kwamba hapa kuna pepo na nikakemea akaanza kusikia.
Kwa hiyo unaposhughulika na magonjwa ya namna hiyo ushughuliki na ugonjwa bali unashughulika na chanzo, unashughulika na lile pepo ukisha shughulika nalo magonjwa/ugonjwa hauwezi kukaa.
MFANO WA TATU
*III. Marko 5:1-15*
_“Wakafika ng’ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi. Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu; makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo; kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikata-kata kwa mawe. Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia; akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese. Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu. Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi. Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi ile. Na hapo milimani palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, wakilisha. Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao. Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini. 14Wachungaji wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka walione lililotokea. Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa.”_
Kwa hiyo ukisoma Bibilia alikuwa anaishia kukaa makaburini alipomuona Yesu akakimbilia hapo na yale mapepo yakaanza kuongea ndani yake na akayauliza jina yakasema ni jeshi kubwa, kama unafuatilia utaona jinsi yalivyoomba ayatoe kwenye lile na kuwaingia nguruwe na Yesu akayaruhusu yakaingia kwenye nguruwe na nguruwe wote wakaingia majini sasa angalia mstari wa 15; _wakamwendea Yesu wakamwona yule mwenye pepo ameketi amevaa nguo ana akili zake naye ndiye aliyekuwa na jeshi wakaogopa_
Kwa nini nimekuonyesha kitu cha namna hii kwa lugha tuliyonayo tungesema alikuwa kichaa hana nguo hana akili maana yake akili zake hazipo kikawaida, kwa hiyo kwa lugha ya kawaida ukikutana naye huku mjini utasema nimekutana na kichaa utasikia lugha hiyo ipo sasa si kila kichaa chanzo chake ni pepo! Ni rahisi sana kufikiria kila kichaa chanzo chake ni Pepo lakini ukienda vizuri kibiblia na ukienda vizuri kidaktari kwa sababu kama unafuatilia maswala ya uponyaji kibiblia jifunze kukaa na kuongea na madaktari utajifunza vitu vingi sana na utaelewa vitu vingi vilivyo ndani ya Biblia vinavyoelezea masuala ya uponyaji utaelewa kirahisi sana. Napata nafasi ya kuzungumza na madaktari nawauliza maswali mengi na mengine magumu sana kwa sababu kuna vitu vingine wala sio vya kukemea. Watu wengi huenda hospitali na wakipewa dawa huwa hawaulizi kilichosababisha ni nini Kwa hiyo saa ingine daktari atakwambia saa nyingine hakuambii lakini usipojua chanzo chake uwe na uhakika ukifanya makosa yale yale yaliyosababisha ugonjwa ukaja utarudi tena.
Huyu alikuwa kichaa na kichaa chake kilikuwa na mapepo ndani alipoenda kwa Yesu alikuwa hana akili timamu hana nguo, hakuna aliyekuwa anaweza kumshika sasa fikiria anakuja namna hiyo Yesu hakumwombea na kumwambia nenda kavae nguo asingeweza kwenda kuvaa nguo kwa sababu yanayomfanya avue nguo kwa hiyo watu wa namna hiyo kama kuna mtu anaye anamfungia ndani, na inasumbua lakini Mungu ana njia nyingi yale mapepo yalipotoka ghafla akili zake zikarudi alafu ghafla akagundua yuko uchi anatafuta nguo
Nilienda mkoa moja nlipokuwa kwenye mkutano nikaletewa mtu moja akaniambia nina ndugu yangu ni kijana tu mzuri lakini hatujui kilichotokea ghafla amekua kichaa anasema anachana magodoro, nguo, akikaa na kitabu anachana nikawauliza ni mwanafunzi au mfanyakazi , wakasema ni mfanyakazi mzuri sana kabisa nikawauliza yuko wapi wakasema yuko hospital nikasema unatakaje akasema sijajua kama una nafasi, ninaomba twende hospitali tukamwombee nikamwambia nafasi sina ila nenda kanunue kitambaa halafu rudi tena akarudi nikamuuliza umewahi kuona mtu anaombea kitambaa anampelekea mgonjwa akasema nimesikia tu ila sijaona nikampitisha kwenye maandiko Biblia unasema zilitoka lesso kwenye mifuko ya Paulo wagojwa walipona na mapepo yakakimbia kwa hiyo nikaiombea ile leso vizuri na kuamuru nguvu za giza zilizomshikilia huyu kijana na kumfanya awe kichaa zimwachie kwa hiyo nikampa kile kitambaa nikamwambia nenda nacho akasema huwa wanamfungia kwa hiyo si rahisi nikamwambia wewe nenda kaombe kwamba unataka kumsalimia halafu halafu usimwonyeshe kile kitambaa mapema kwa sababu yale mapepo saa nyingine yakiona yanaweza kugoma kupokea hicho kitambaa kwa hiyo akaenda kesho yake akarudi kunieleza. Akasema alienda akawaomba wale viongozi wa hospitali wakamruhusu akaenda moja kwa moja wakati yule ndugu yake anashangaa na kila kitu kikichanwa na nguo alizokuwa nazo akajitahidi kushika mkono kama vile anataka kumsalimia na yule mtu akampa alipomalika tu namna hii ghafla akabaki anashangaa halafu yule ndugu yake akaondoka ananiambia kesho yake wakampigia simu wakamwambia sijui kilichotokea lakini ulipoondoka tukaona tu ndugu yako ametulia, njoo umchukue ndugu yako kwa hiyo akaenda hospitali akamchukua ndugu yake na akarudi kazini!
Nataka ujue wakati uweza wa Mungu unashughulika na tatizo lako la ugonjwa nenda vizuri kwenye Biblia sehemu kubwa haishughuliki na ugonjwa inashughulika na chanzo cha ugonjwa halafu ugonjwa unaondoka.
Leo tunaangalia tu kidogo magonjwa ambayo chanzo chake ni mapepo na nimekueleza si kila mtu mwenye kichaa chanzo chake ni mapepo utizame unaweza kusema na huyu ni pepo Mengine sio mapepo.
MFANO WA NNE
*IV. Mathayo. 12:22‭-‬24*
_Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu; akamponya, hata yule bubu akanena na kuona. Makutano wote wakashangaa, wakasema, Huyu siye mwana wa Daudi? Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo._
Nimekusomea huu msitari ili uweze kujua Biblia inasema alimponya tu haionyeshi alimponyaje ila hapa chini inatuambia alikuwa na pepo ndio maana ukaanza mjadala wa pepo hapo. Ameletewa mtu alie kipofu na bubu kilichosababisha hayo yote lilikuwa ni pepo lililokuwa ndani yake, sasa Yesu hakushugulika na upofu na ububu wake alishughulika na pepo lilomfanya awe bubu na kipofu na waliokuwa wanatazama ndio wakasema lazima anatumia mkuu wa mapepo na Yesu akawaambia kama pepo anaweza kumtoa pepo mwenzake basi ufalme wake umefitinika ndio maana lazima uwe mwangalifu sana unapokutana na mazingira ya aina hiyo kwa sababu pepo hawezi kumtoa pepo mwezake atamnyamazisha tu kwa kumpa vitu anavyotaka kama ni maji,pete nk
Huna sababu ya kwenda kwa mungu mdogo wakati kuna MUNGU mkubwa anaeweza kuyatoa mapepo yote kwa sababu biblia inatuambia kuna Mungu wa miungu, kwa hiyo mimi ningekuwa wewe hakuna sababu ya kwenda kwa hawa miungu wadogo hauko mbali sana unatakiwa tu kuja kwa Mungu wetu mkubwa utapata msaada. *Ndio maana ukimuona mtu anachinja mbuzi na kuku ili apone usigombane nae hatakuelewa msaidie tu kumwambia kuna damu iliyo bora zaidi sio ya kuku inaitwa damu ya Yesu* asije akasema unamtangazia dini yako maana msalaba hauna dini,unaweza kusema “sasa mbona wakristo wanajivunia msalaba”       Biblia inasema ni kwa kila aaminiye na Yesu alikufa ni kwa ajili ya watu wote unaamua kama unataka kumwamini au hutaki,sasa lazima ujue si kila mtu mwenye shida ya kipofu na bubu ni shida ya kipepo  najaribu tu kukuonyesha kwenye Biblia mifano michache ambayo Yesu alikuwa anaona chanzo cha ugonjwa huu ni pepo.
MFANO WA TANO
*V. Mathayo. 17:14‭-‬15‭, ‬17‭-‬18*
_Nao walipoufikia mkutano, mtu mmoja akamjia, akampigia magoti, akisema, Bwana, umrehemu mwanangu, kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa vibaya; maana mara nyingi huanguka motoni, na mara nyingi majini. Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu. Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile._
Yule kijana alikuwa na kifafa na kifafa ni ugonjwa lakini unaona hapa kuwa kifafa kililetwa na pepo lilokuwa ndani yake, na maandiko yanatuambia hivi kuwa YESU hakushughulika na kifafa bali pepo lilokuwa linaleta kifafa. Akamkemea pepo na akamtoka na yule kijana alipona tangu saa ile.  Sasa sikuambii kuombea ugonjwa ni vibaya, tutaangalia wiki hii kuona ni maeneo gani ya kuomba na kukemea kwa pamoja, inategemea Roho Mtakatifu anakuambia ni kitu gani. Nataka upate kujua kuwa kuna magonjwa vyanzo vyake ni mapepo na ukitaka kushughulika na ugonjwa shughulika na mapepo.
Pepo likitoka huo ugonjwa hauwezi kaa maana umebebwa na pepo.
*USHUHUDA*
Tulikuwa mahali fulani kwenye huduma alikuja dada mmoja alikuwa na shida ya kutokwa na damu kwa muda mrefu na alisema hadi damu imepungua mwilini, na alisema nimehangaika kila hospitali na alitueleza na miaka aliyoteseka. Sasa tulimhoji maswali mawili matatu pale na baada ya mahojiano tulijua kuwa ana pepo. Kwa hiyo nikamwambia kuwa weka mkono wako chini ya kitovu.  Sasa nikanyoosha kidole changu kuelekea mkono wake na nilipogusa  ghafla pepo likalipuka na akaanguka chini. Baada ya pale pepo lilitoka na baada ya pale alienda kucheki na tangu saa ile damu ilikoma. Sasa sio kila mtu anayetokwa na damu shida yake ni pepo. Unahitaji kujua Roho Mtakatifu anakuambia nini.  Kwa hiyo unahangaika na kinachosababisha damu itoke, kwa hiyo nilikemea pepo damu ikakakuka.
*USHUHUDA*
Nilikuwa mahali akaja mtu mmoja mahali nilipokuwa  akasema anakichwa kisichopona na kinamtesa sana. Nilimuuliza  kama amewahi kwenda hospitali alisema ndio amewahi kwenda lakini alisema anaumwa kichwa ambacho hata akinywa dawa bado kinamsumbua. Nikamwambia piga magoti. Nikabandika mkono wangu juu yake. Na mkono wangu ulipomfikia akaanguka chini, nikajua yako mapepo ndani yake. Sasa nikasema wewe pepo unaesababisha shida ndani ya huyu mtu toka. Lile pepo likaamua kunijibu likasema “huyu ni wa kwetu”.  Tumepewa tumuoe,  unatutoa ili twende wapi. Nikaliambia siwakemei ili mbishane na mimi haijalishi nani amewakabidhi nani lakini huku ndani lazima mtoke. Yakatoka, sasa baada ya pale kichwa kilitulia. Sikukemea maumivu ya kichwa nilikemea pepo lilokuwa linasababisha maumivu ya kichwa maana ukikimea pepo likitoka na maumivu ya kichwa hayawezi kaa.
*USHUHUDA*
Tulikutana na mama mmoja  mahali pengine alisema anapata shida ya kubeba mimba kwa mume wake, kwa hiyo alisema kila akibeba mimba huwa zinaharibika. Alikuja kwetu akihitaji maombi.  Tukasema mama weka mkono wako kwenye tumbo lako. Alipoweka tu pale akaanguka chini. Tukakemea mapepo yaliyopo kwenye tumbo lake baada ya miezi michache alisema mimi ni mjamzito.  Sasa si kila mwenye shida ya kubeba mimba shida yake ni mapepo.
Nakueleza haya  ili uweze kuelewa kuwa inapokuwa kuna magonjwa ambayo chanzo chake ni mapepo Yesu  ametuonesha njia na fanya kama alivyofanya utapata matokeo aliyopata.
*Sasa ngoja tufanye zoezi hapa kama unajua unaumwa au unajua una pepo au kama unaumwa na  ukienda hospitali hawaoni kitu, au wameona kitu  lakini ugonjwa hauishi. Umewahi fikiri yule mama mkwe wa Petro alipokuwa anaumwa homa kama angemeza dawa  lakini haiendi mahali maana pepo lililopo ndani yake halitameza dawa.*
Kama unaumwa na una pepo, maana tunaona katika Biblia kuwa mtu alikuwa anaumwa na walio mleta walijua ana pepo.. .. njoo tuombeee..
Nenda YouTube kwa link ya semina ya leo sikiliza maombi ya leo… angalia link pale juu semina ya leo YouTube  sogeza sikiliza kule mwishoni maombi ☝☝☝☝
[07:31, 11/05/2018] Filix Bwanji: *4⃣SEMINA YA NENO LA MUNGU-DODOMA UWANJA WA BARAFU*
*MWL.CHRISTOPHER MWAKASEGE*
*SOMO: UWEZO WA MUNGU JUU YA MAGONJWA NA VYANZO VYAKE.*
*TAREHE  09 MAY, 2018*
*SIKU YA NNE*
*👉LINK YA SEMINA YA LEO YOUTUBE* https://youtu.be/mFpCIWebVqs
*👉 NAMBA ZA SADAKA* https://goo.gl/Z3ozYB
*👉NAMNA YA KUPATA CD&DVD BONYEZA HAPA* https://goo.gl/tgwoub
*👉REDIO ZINAZORUSHA SEMINA HII* https://goo.gl/UzzqFP
Jana tuliangalia uweza wa Mungu kuponya magonjwa ambayo chanzo chake ni mapepo, tuliangalia points 2 na ni points muhimu sana. Kuna vitu vichache vingine nilitaka niendelee navyo lakini Roho Mtakatifu akanipa kitu kingine. Huko mbele Mungu akinipa nafasi ya kufundisha nitafundisha.
Leo tutaangalia
_*KUANGALIA UWEZA WA MUNGU JUU YA MAGONJWA AMBAYO CHANZO CHAKE NI KIFUNGO CHA KIROHO.*_
Kuna mambo kama manne tutakayoangalia leo kwa muhtasari. Na ninataka tuangalie kwa mtiriko huu
JAMBO LA KWANZA
*1.KUNA MAGONJWA AMBAYO CHANZO CHAKE NI KIFUNGO CHA KIROHO*
*Luka 13:10‭-‬12‭, ‬14‭, ‬16*
_“Siku ya sabato alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo. Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa. Yesu alipomwona alimwita, akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako. Basi mkuu wa sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akajibu, akawaambia mkutano, Kuna siku sita zifaazo kufanya kazi, basi njoni mponywe katika siku hizo, wala si katika siku ya sabato. Na huyu mwanamke, aliye wa uzao wa Abrahamu, ambaye Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato?”_
Kumbuka jana nilipoongea nawe na nilipoanza kukuonesha polepole utakuwa unaona kabisa picha kuwa Yesu alipoanza kuponya kwa kutumia ule uweza ulikuwepo juu yake na alikuwa anatembea nao na sasa ameuweka juu ya kanisa na ameuweka utembee na watu wake.
Yesu alipokuwa anashughulikia magonjwa utagundua magonjwa mengi ambayo aliyashughulikia, alishughulika na chanzo. Akishughulikia chanzo huo ugonjwa haukai. Ndio maana nikakupeleka jana na tukaona magonjwa ambayo alishughulikia vyanzo vyake vilikuwa ni mapepo, kwa kukemea mapepo mgonjwa anapona.
Lakini unaona huyu alikuwa ana pepo lakini Biblia inasema alikuwa amefungwa na alikuwa ni mgonjwa na uti wa mgongo wake kupinda kwa sababu alikuwa hawezi kujinyoosha kwa kujipinda. Na maandiko yanatuambia lile pepo la udhaifu lilikuwa limemfunga miaka kumi na minane na Yesu akaweka mikono yake juu yake wala hakukemea. Na Biblia inasema naye akanyooka mara hiyo. Na aliponyooka namna hiyo yule mkuu wa Sinagogi yeye aliona ni uponyaji wa kawaida ndio maana alikuwa anasema jamani wanaohitaji kupona waje kwenye siku sita siku ya Sabato wasije. Na wewe unaweza ukaona Yesu akiwaponya wengi na kila mmoja uponyaji wake unatofautiana.
Kwenye mstari wa 16 Yesu alizungumza neno zito pale
*Luka 13 : 16*
_“Na huyu mwanamke, aliye wa uzao wa Abrahamu, ambaye Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato?”_
Sio kwamba shetani alimfanya kuumwa bali alimfunga, katika kile kifungo ugonjwa ndio ukaonekana.
*Marko 7:31‭-‬35*
_“Akatoka tena katika mipaka ya Tiro, akapita katikati ya Sidoni, akaenda mpaka ziwa la Galilaya, kati ya mipaka ya Dekapoli. Wakamletea kiziwi, naye ni mwenye utasi, wakamsihi amwekee mikono. Akamtenga na mkutano faraghani, akatia vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa ulimi, akatazama juu mbinguni, akapiga kite, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka. *Mara masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri.*
Kwa hiyo huu haukuwa ugonjwa wa kawaida wa masikio na kwa jinsi ya nje alikuwa ni kiziwi lakini kwa jinsi ya rohoni sikio lake lilifungwa kwa Biblia kusema kuwa *masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri.* kwa hiyo ulimi wake ulikuwa umefungwa.
Sasa haina maana ya kwamba kila aliepinda mgongo au alie kiziwi au mwenye kigugumizi kafungwa kwa sababu tunaona akiwahudumia tofauti tofauti
*Isaya 52:2*
Jikung'ute mavumbi; uondoke, Uketi, Ee Yerusalemu; Jifungue vifungo vya shingo yako, Ee binti Sayuni uliyefungwa.
Huyu kifungo kipo kwenye shingo.
Isaya 10:27*
_“Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta.”_
Sasa kwa wale wasiofahamau maana ya nira kwa ‘lugha’ iliyo nyepesi ni mti unaofungwa shingoni mwa punda wakati wanasukuma mkokoteni au maksai (ng'ombe dume) wakati wanalima kwa kufungiwa pamoja.
Ndio maana sio nira yako ni ‘nira yake’ maana yake yupo aliekufunga. Na Yesu anapotaka kutembea na wewe ili usipotee anasema jitie nira yangu, nira yangu ni laini tena ni nyepesi ili kwamba tusije tukapotea ili kila tuendapo twende na yeye pekee (nira yake Yesu inatakiwa iwe juu ya watu wake).
Ila hapo nira anayozungumza ni mbaya kwa sababu hii nira itaharibiwa kwa sababu ya kutiwa mafuta. Maana yake kuna upako/uweza wa Mungu uliotengwa mahususi kwa ajili ya kushuka juu ya viungo vya namna hiyo na kuyeyusha kabisa na kuviharibu ili huyo mtu aliefungwa apate kufunguliwa.
Saa nyingine tu unakuta shingo imekaa upande mmoja wa wataalam wanasema imelock, huwezi tena kugeuza mahali, utapewa dawa na wakati mwingine sindano baada ya muda inaweza kurudi na kugeuka upande mwingine lakini wakati mwingine hali inakuwa mbaya zaidi.
Sasa wakati mwingine ni lazima ukafanye check up kama shingo yako imefungwa maana unaweza ukapata shida ya koo au aina fulani ya saratani/ goita (kuvimba kwa tenzi ya throid) ambayo hata ukizifanyia upasuaji/operation unaona inatokea kwa juu yake tena. Nguvu za MUNGU zikishuka zinayeyusha
*USHUHUDA*
Tulikuwa mkoa mmoja mtu alikuja kushuhudia baada ya kutusikiliza kwenye radio, alikuwa na goita baada ya kufanyiwa upasuaji/operation ikaota tena. Sasa anatusimulia alipokuwa nyumbani kwake na kilipofika kipindi cha maombi naye akaweka mkono kwenye shingo yake akasema nguvu za MUNGU zilimshukia pale akaona kama kuna mtu anavuta vitu kwenye shingo yake halafu ghafla ule uvimbe na vile vitu alivyokuwa anavisikia vyote vikatoweka kabisa.
Kwenye shingo unaweza ukapata shida ya pingili zinazokaa kwenye shingo, sasa mimi sijasomea u daktari lakini kwa sababu ya kuwaombea watu nimelazimika kusoma vitu vingi sana kwenye mwili wa mtu pamoja na kwamba sekondari nilisoma biology kidogo. Kwenye shingo kuna mishipa ya fahamu inayopita kwenye hizo pingili, mingine inaenda kwenye macho, pua,sikio, mingine kwenye mabega. Sasa kama shingo yako ikifungwa kuna mishipa inaweza kubanwa na kusababisha kule ambapo inatakiwa kuunga kwenye mwili na utendaji wake unaweza kupata shida. Sasa sikwambii kila tatizo unalolipata kwenye shingo si kwa sababu ya kufungwa ila nataka nikwambie ya kwamba kuna magonjwa mengine ambayo yapo kwa sababu ya kifungo cha kiroho.
Ndiyo maana unakuta mara kwa mara wakati mwingine mtu akiniambia anaumwa nitamuuliza umeenda hospitali? Maana usije ukafikiri kwenda hospitali ni kukosa imani. Nenda hospitali hata kama huumwi ili ukafanye check up tu watakusaidia kugundua na mengine. Maana kama akili zipo za kupeleka gari kwa ukaguzi/check up kabla ya kusafiri na si kwamba ni mbovu bali kujihakikishia ili usije pata shida njiani, vivyo hivyo na mtu anahitaji check up. Au hujaona ndani ya Biblia neno hospitali kwa sababu haijaandika hospitali? Soma
*Yohana Mtakatifu 5:2-3*
_“Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano. Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yachemke.”_
Matao matano tungesema ni wodi tano za wagonjwa na zote zimejaa wagonjwa, wakisubiri malaika ashuke na kutumbukia ili achemshe maji na kila mmoja awahi na anayewahi anapona. YESU alikuja pale na kumkuta mwingine amekaa muda mrefu na kumponya.
Sasa ukienda hospitali na malaika wako hapo kutibua maji na anayewahi anapona. Maana unaenda kwa daktari huyohuyo na ugonjwa huohuo mwingine anapona na mwingine anakufa. Kwa sababu vitu vilivyopo ndani ya mwili hata ukivunjika mfupa hawawezi wakakuponya mfupa wako wanatengeneza mazingira ya nguvu za uponyaji zilizopo ndani ya mwili ziweze kufanya kazi.
Nakueleza haya ili uweze kuwa na usawa wa hivi vitu. Lakini pia inasaidia sana ukienda hospitali wakati wa kufanya uchunguzi na kukwambia unaumwa kitu gani, hii inarahisisha sana katika kuomba na kujua tunapambana na kitu gani katika mwili huu tunapoomba. Pamoja na kwamba wakati mwingine watakwambia unachoumwa lakini ni matokeo ya kitu ambacho unahitaji kukiangalia kwa undani zaidi na ROHO MTAKATIFU atakuwa pale kwa ajili ya kukusaidia.
JAMBO LA PILI
*2. IKIWA CHANZO CHA UGONJWA NI KIFUNGO CHA KIROHO, ROHO MTAKATIFU ATAKUONGOZA KUFUNGUA KIFUNGO CHA KIROHO KWANZA ILI MGONJWA APONE*
*Luka 4:17-18*
_“Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa,Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema.Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena,Kuwaacha huru waliosetwa,”_
ROHO MTAKATIFU aliyekuwa juu ya YESU kazi yake mojawapo ni kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao. Sasa si tu masuala ya kuwafunguliwa toka kwenye kifungo cha dhambi lakini katika ulimwengu wa roho kuna vifungo ambavyo vinajitokeza kwa jinsi ya mwili kwa namna tofautitofauti, vifungo vingine vikijitokeza kwa jinsi ya mwili vinaachilia magonjwa, yanaonekana na magonjwa kwa jinsi ya nje kama tulivyoona yule mama amepinda kwenye ile *Luka 13* YESU alishughulika na kufunguliwa kwake hakushughulika na ugonjwa wake, hata wale viongozi wa sinagogi na viongozi wengine walipoanza kubanana naye akawaambia huyu mama amefungwa na shetani kwa miaka 18 hii, hakusema shetani amemfanya aumwe, sasa mnajisikia vibaya akifunguliwa siku ya sabato? Na alipoletea yule mtu ambaye alikuwa kiziwi na ana kigugumizi unaona alikuwa amefungwa na yeye kwa sababu unaona YESU alilenga kumfunga, na alipomfungua akasikia na kuongea.
Ni muhimu uweze kufahamu ili, kwamba katika taratibu za Kibiblia msingi ya masuala ya kimwili ni ulimwengu wa roho na vifungo ni hivyo hivyo. Kukiwa na kifungo katika ulimwengu wa roho ni lazima kifunguliwe kwanza ili huyu mtu awe huru kwa jinsi ya nje la sivyo uhuru wake huo wa nje hautakuwa wa kudumu, hautamletea yale matokeo yanayotakiwa, hatakuwa huru kweli kweli kama YESU anavyosema.
JAMBO LA TATU
*3. KIBIBLIA KUNA WAFUNGWA WALIOFUNGWA HALALI NA KUNA WAFUNGWA WALIOFUNGWA KWA KUONEWA*
*Isaya 49:24*
_Je! Aliye hodari aweza kunyang'anywa mateka wake, au  jeshi lao *waliofungwa halali* wataokoka?_
Nataka uone lile neno *waliofungwa halali* kama kuna walifungwa halali kuna wengine hawakufungwa ki halali, Biblia isingetenganisha wafungwa halali kama kuna wafungwa wasio halali kwa hiyo kuna wafungwa halali ambao kwa lugha nyingine kuna vitu wamefanya na kufuatana na sheria iliyopo wakati huo na wamefungwa halali.
*Matendo 10:38*
_habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huku na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote *walioonewa na Ibilisi;* kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye._
Nataka uone lile Neno *walionewa na ibilisi* kwa hiyo kuna watu ambao wanateswa kihalali na kuna wengine ambao wameonewa hata katika mazingira ya kawaida ukienda ukashitakiwa umeiba na kesi yako ikatangazwa au umekuja ukashikwa ndugu zako watakimbizana kutafuta wakili na kukuwekea mdhamana saa ukikaa kuzungumza na wakili swali mojawapo atakalo kuuliza ni kwamba niambie ukweli umeiba au hukuiba? Uwe na uhakika hilo swali atakurudishia mara mbili mara tatu kwa sababu anataka ajue anamtetea mwizi aliyehalali au aliyeonewa. Kwa sababu kama ni mwizi halali atatafuta kila aina ya kipengele atakuambia hii kesi ni mbaya kukutoa kabisa inaweza isiwe rahisi labda nikutetee kukupunguzia kipindi cha kufungwa ukikataa atakwambia labda utafute mtu mwingine naye atakulia hela tu mi nimeona nikueleze wazi hii kesi haijakaa vizuri kwako sioni ni namna gani unatoka hapa ila tuone tu sheria itakavyoweza kukupunguzia kwa sababu ninaona hapa una miaka mitatu jela labda nitafute mbinu ya kuzungumza (ni kosa la kwanza, tena ameoa mwezi uliopita) atajaribu kila lugha sasa hapa itategemea huruma ya hakimu na vipengele vya sheria vina mruhusu kiasi gani na kama umeonewa atajaribu kutafuta kila njia ya kuona haki inatendeka na unaachiwa kwenye sheria humo humo lakini atataka kwanza kujua umeiba au hukuiba
Haya ni mambo ya msingi kabisa hasa unamhudumia mtu wa namna hiyo katika ulimwengu wa Roho kuna vitu unahitaji kujua saa nyingine Roho Mtakatifu atakujulisha kabla huyo mtu hajakujulisha au yule mtu amenyamaza Mungu anakusemesha mapema au anakupa njia ya kumwombea ambayo inashughulika na kesi yake na kufunguliwa kwake.
*Danieli 4:1-36*
_Mfalme Nebukadneza, kwa watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wanaokaa katika dunia yote; Amani iongezeke kwenu. Mimi nimeona vema kutangaza habari za ishara na maajabu, aliyonitendea Mungu aliye juu. Ishara zake ni kubwa kama nini! Na maajabu yake yana uweza kama nini! Ufalme wake ni ufalme wa milele; na mamlaka yake ni ya kizazi hata kizazi.  Mimi, Nebukadneza, nilikuwa nikistarehe nyumbani kwangu, nikineemeka katika nyumba yangu ya enzi. Nikaota ndoto iliyonitia hofu; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha._
Sasa kama ni msomaji wa Biblia utaelewa hii habari inaenda wapi akatafuta watasfri hakupata msaada isipokuwa kwa Daniel na Daniel aliposikia yale maneno hakupenda kabisa tafsiri ile impate mfalme lakini akamweleza tafsiri yake kwa sababu kama ule mti umekatwa anamweleza anasema ule mti ni wewe utaezuliwa utaondolewa utaenda kukaa pamoja na wanyama nyakati saba tuseme kwa jinsi ya kawaida miaka saba mpaka utakapojua mbingu ndizo zinazotawala na Biblia inazungumza vitu vigumu sana na Nabukadreza anatoa ushuhuda. Daniel 4 ni ushuhuda wa kimaandishi (press release) ya Nabukadreza baada ya kupona ili watu wajue kilichotokea kwa sababu ni ngumu sana kujua kilichotokea kama asingesema na Biblia inazungumza katika mstari wa 27
_ Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; uache dhambi zako kwa kutenda haki, uache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za fanaka._
Kwa hiyo alimpa   na mshauri kama anataka asiingie kwenye kile kifungo alimpa ushauri kama anataka kuendelea kukaa katika raha usiende katika hiyo shida ya nyakati saba, shauri langu Daniel anamwambia mstari wa 27; Biblia inasema mstari wa 28;
_Hayo yote yakampata mfalme Nebukadneza.Baada ya miezi kumi na miwili, alikuwa akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli. Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe makao yangu ya kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu? Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadneza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme huu umeondoka kwako. Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa mwituni; utalishwa majani kama ng'ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye Juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote. Saa hiyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadneza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng'ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege._
Kwa lugha ya sasa tungesema amekuwa kichaa unasema umejuaje anakula majani kama ng’ombe maana yake hatumii mikono anaenda na mikono yote anakula majani kama ng’ombe hakuwa na nguo tena na kwa sababu ya umande uliokuwa unammwagikia vinyweleo vyake vikawa kama manyoya ya tai kwa ajili ya kulinda mwili wake,  alikuwa hakati kucha mbaya zaidi hata watu wake waliokuwa karibu naye walikuja baada ya miaka saba (nyakati saba) hawakumpelekea hata nguo kwanini nimekuonesha hii picha fikiria wewe ni mtumishi wa Mungu unaletewa Nabukadreza ana manyoya kama manyoya ya tai na wanasema jamani tumsaidie huyu ni mfalme! Si umesikia habari za mfalme wa Babeli ndio huyu sasa kaacha familia yake mke na watoto hata nafasi yake iko hivyo hivyo lakini hakuna mtu anayemshughulikia hata anayemletea chakula hata chakula cha wanadamu hali anakula majani, wanakwambia tunaomba umsaidie wewe ni mtumishi wa Mungu.
Unajua kitu utakachoanza kufanya ni kuanza kukemea mapepo ya kichawi yule hakuwa na mapepo ya kichawi bali vifungo (hukumu). Biblia inasema hukumu hii imekuja kwa ajili ya Watakatifu. Katika kufungwa kwake ndipo kimejitokeza nje akaonekana kama kichaa alikuwa mfungwa tena mfungwa halali.
Saa nyingine usiseme tu tumwombee huyu, labda yeye hana imani au wewe huna imani, unatakiwa kuwa mwangalifu sana kwa kumsikiliza Roho Mtakatifu anasemaje katika hilo. Mtu wa jinsi hiyo lazima kwanza ushughulikie kifungo chake la sivyo hatoki. Na watu wanaougua kwa style hii, Mungu huwa anawaonesha kwa njia ya ndoto mapema au umemwombea mtu kama huyo na usiku unaoneshewa yuko kwenye shimo na kafungwa na kamba au yupo mahali anatandikwa viboko. Kwa namna hiyo Mungu anakujulisha kuwa usikimbizane na ugonjwa huo bali ukimbizane na chanzo chake katika ulimwengu wa roho na ukishafanya hivyo ugonjwa hautaweza kukaa hata kidogo.
Ila kama ni kifungo halali au ameonewa lazima ujue namna ya kushughulika nayo
Sasa wewe ambae Mungu amekupa nafasi ya kumhudumia huyo mtu unahitajika kukaa mkao wa kumsikia Mungu akikusemesha wakati huo kwa sababu sina uhakika kama Nebukadneza alifahamu hili akiwa katika mazingira hayo kama alikuwa ana uwezo wa kujieleza labda ndugu zake waweze kueleza kidogo.
JAMBO LA NNE
*4. MAGONJWA AMBAYO NI VIFUNGO, KIWE NI HALALI AU KUONEWA MARA NYINGI YANAFUNGULIWA KWA KUTANGAZA KUFUNGULIWA KWA MTU YULE HUKU UKITUMIA DAMU YA YESU.*
Tusome vifungu vifuatavyo
*Waraka kwa Waebrania 12:24*
_“Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.”_
*Ufunuo 5:9*
_“na waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuifungua mihuri yake; kwa kuwa ulichinjwa, ukawa fidia kwa Mungu na kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,”_
*Waefeso 1:7*
_“Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.”_
*Wakolosai 1:13‭-‬14*
_“Naye alituokoa kutoka kwa nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake mpendwa; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi.”_
*Luka 4:18*
_“Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini Habari Njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,”_
Hapa kwenye jambo la nne magonjwa ambayo (ni vifungo) au chanzo chake ni vifungo vya kiroho mara nyingi yanafunguliwa kwa kutangaza kufunguliwa kwa huyo mtu kwa kutumia Damu ya Yesu Kristo.
Kuna mambo ya msingi unahitaji kuyafahamu juu ya msalaba kwamba msalaba ni matokeo ya upendo wa Mungu kwa watu na ni matokeo ya upendo wa Yesu kwa wote.
*Yohana 3:16*
_“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”_
Hakuna upendo mkubwa wa namna hii ambao mtu anautoa uhai wake kwa ajili ya mtu mwingine.
Lakini pia Yesu alikufa tungali wenye dhambi kwa hiyo alikupenda sio kwa sababu wewe ni Mzuri.
Unahitaji kufahamu msingi wa msalaba.
👉Msalaba hauiti wenye haki ila wasio na haki wapate haki.
👉Msalaba hauiti wasafi, bali wachafu
Biblia inasema alikufa kwa ajili yetu wakati bado tuna dhambi. Kwa hiyo alionesha pendo lake kwa kufa kwa ajili yetu wakati hatujatubu, Mungu alimtuma mwana wake wa pekee kwa ajili yetu hata hatujajifunza sala ya toba maana yake ni nini.
Hatujajua hasara ya dhambi maana yake ni nini.
Hao walikuwa wanasoma katika agano la kale kulikuwa na madhara ya dhambi waliyokuwa wanayafahamu kwa ngazi fulani lakini soma agano jipya utajua madhara ya dhambi yalivyo magumu na ndipo utaelewa ya kwamba kama Mungu atafunua ugumu wa dhambi kwa style hiyo lazima kuwe na dawa iliyo bora kuliko sawa ya agano la kale na ndio maana tuna agano lililo bora zaidi lililoahidiwa ambao msingi wake ni damu iliyo bora kuliko damu zingine zote
Katika agano jipya ni agano lilo bora zaidi na ahadi bora zaidi, na damu ya Yesu ni damu bora  kuliko damu zingine. Damu ya Yesu ipo kumsaidia mfungwa halali na mfungwa aliyeonewa. Ni rahisi sana ukafikiri  Damu ya Yesu ni kuwasaidia tu wale walioonewa ambao matendo yao ni mazuri  au wamesingiziwa kwa hiyo Damu ya Yesu itakimbia kuwasaidia tu hao. Biblia ninayosoma inasema yeyote aliyefungwa kihalali au kwa kuonewa damu ya Yesu inakusaidia. Lakini kibiblia imezungumzwa kitofauti. Biblia inazungumza juu ya ukombozi na kununua.
*Kukomboa* maana yake kilichokua cha kwako na kilichukuliwa na mwingine kihalali. Kwa mfano mko watoto wanne kwenye familia na mmoja mmemwacha kijijini mnarudi nyumbani Krisimasi  mnakuta ameuza nyumba na wameandikishana kila kitu. Nyumba ni yenu lakini inamilikiwa na mtu mwingine. Sasa mkitaka kuirudisha ni lazima muikomboe. Tunakwenda sawa sawa?.
Huwezi kusema tumeonewa, sasa kama hazungumzi huko ndani ni ya kwenu sasa yule aliyenunua anaimiliki kahalali maana kafuata sheria kwa hiyo nyumba anakuwa ni mfungwa wake halali. Sasa nyie kama mnataka kuirudisha anasema  hamna shida anasema nirudishieni hela yangu. Sasa kama hamna hiyo hela ….
Shetani akikukamata na akaamua kukufunga au Mungu akiachilia adhabu ambayo atakuwa amekufunga kwenye kufungo. Ukitaka kutoka ni lazima utafute utaratibu maana ni mfungwa halali. Nebukadreza  aliambiwa kitu gani, haloo adhabu yako ni hii, sasa kwa kiingereza tunasema ni “suspended sentence”. Alipewa nafasi ya kutafakari kuwa kama Ukitubu utapona ila kama ni hivyo adhabu yake ni miaka saba. Kipindi cha kutafakari alipewa miezi kumi na mbili. Alipewa na nafasi ya kutengeneza, na angekuwa katika kipindi cha sasa, angepewa kuwa kifungo cha miaka saba au fine ya shilingi milioni tano au vyote viwili. Na  unapewa kipindi cha miezi kumi na mbili katafakari.  Baada ya miezi kumi na mbili Jaji anakuita na kuuliza kuwa umeamuaje? Una milioni tano za kulipa  anasema sina, kwa hiyo Jaji anamuuliza nikupeleke jela? Anasema ndio basi anampeleka jela, kwa sababu alipewa miezi kumi na mbili na kashindwa kutafuta milioni tano.
Kwa sababu hata ukipewa miezi mingi hamna mtu anaweza lipa mshahara wa dhambi, ukitafuta  hayupo. Ndio maana Yesu alipokufa huwezi kulipa kwa matendo mazuri ni lazima ulipe kwa tiba ili damu ya Yesu iingie kazini kwa ajili ya kukusaidia. Ndio maana nimekusomea Waebrania 12:24 inayosema Damu ya agano jipya  damu ya kunyunyiza inenayo mema kuliko ile damu ya Habili. Maana yake ni damu inayoongea kwa niaba ya yule mtu ambaye anaombea. Mungu aliwaambia wana wa Israeli kuwa nimewapa hiyo damu katika madhabahu ili ifanye upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu. Kwa hiyo unapoomba Toba mbele za Bwana, hiyo toba lazima ibebwe na damu. Ili damu sasa ndio unaruhusiwa kisheria kuzungumza na Mungu,  kwa maana inafanya upatanisho kwenye madhabahu kwa ajili ya nafsi ya mtu. Huwezi ukajisema mwenyewe maana ndio gharama mojawapo ya dhambi  ilivyo mbaya. Na ndio maana hata ukienda kwenye nguvu za giza kuna baadhi ya mapepo huwezi kuongea nayo hadi useme kwa kupitia damu fulani kwa hiyo iwe ya kuku au ya mbuzi,  kwa hiyo katika ulimwengu wa roho huwezi ukajisemea wewe mwenyewe kwa sababu mshahara wa dhambi ni mauti, kulikata katika ulimwengu wa roho na hakuna mawasiliano na daraja linalotakiwa ni damu.
Kwa sababu sasa katika  ulimwengu huu wa giza hawana damu iliyo bora kama damu ya Yesu wao wanatumia damu zingine wakifikiri Mungu bado anatumia staili ile ya zamani kabadilisha kabisa  na anatumia damu ya Yesu. Kwa sababu damu ya Yesu inakubalika mbinguni. Heshima yake ni kubwa mbinguni, duniani, kuzimu na kila mahali. Damu yake ikiingia kwa afisa magereza na ikija kumsemea huyu mtu afunguliwe, unadai kitu gani. Chochote ambacho  shetani atadai unaweza kulipa kwa damu ya Yesu.  Kama unadai kitu na shetani anasema siwezi kurudisha, lazima ulipe faini, biblia inasema unaweza tumia damu ya Yesu  kumnunua. Biblia inasema alitununua kwa damu. Na ukiachilia damu kwa staili hiyo shetani hawezi bisha maana anajua kilichotokea katika ulimwengu wa roho,  kama ni dhambi,  damu itanena mema kwa ajili yako maana itasema huyu hakujua kuwa hiki kilichofanyika, Mungu msaidie tu huyu, hata kama shetani atasema amefanya dhambi  kubwa lakini hakuna dhambi kubwa kuliko Damu ya Yesu.
Kwa hiyo kama ni mfungwa halali, achilia damu ya Yesu hiyo damu itafanya kazi  kwenye kifungo chako na kesi yako na kuweka rufaa kwa Mungu na ili ufunguliwe. Ukinipa jina la mtu ambaye unataka aombewe kifungo chake halali, utasikia nikisema nanyunyiza damu ya Yesu ya agano jipya juu ya fulani.  Hiyo damu kwenye madhabahu ya Mungu itaanza kuongea. Sasa utajiuliza kuwa damu inaongeaje?. Damu inabeba uhai, na Yesu amekaa mkono wa kuume wa Mungu kwa hiyo nikitaja namna hiyo Yesu anaanza kuongea na Mungu anauliza kulikoni. Anasema kule duniani Mwakasege kataja Damu yangu juu ya huyu mtu. Mungu atauliza lakini si amefanya dhambi,  Yesu atasema nilikufa kwa ajili yake.
Ndio maana saa nyingine wenye dhambi wanapona wakati hawajatubu. Kamuulize Nebukadreza alianza kumsifu Mungu kabla ya ufahamu wake kurudi. Ufahamu wake uliporudi ndipo alijua kuwa kumbe huyu Mungu ni mkubwa namna hii  lakini kakaa kifungoni miaka saba na ndio maana alianza kutoa ushuhuda mkubwa. Sasa ndio maana kuna baadhi ya watu ambao Mungu anawafungua katika vifungo vigumu na ndipo wanaanza kutangaza ushuhuda mkubwa na kuzunguka huku na huko kitu ambacho Yesu kawatendea. Maana Yesu aliwafuata wakiwa kwenye dhambi na hawampendi na hawamtaki,  lakini bado anasema nimekufa kwa ajili yako  na anakusaidia.
Kama umeonewa biblia inasema utahesabiwa haki katika Damu ya Yesu  na ndio maana utaona Yesu anazunguka kumtafuta kila mtu aliyeonewa na ibilisi.  Na anaachilia Damu  yake na kumwambia shetani huyu unamuonea na inatakiwa umuachie sasa hivi. Huyu haki yake ni kuwa na afya  anatakiwa mgongo wake unyooke,  masikio yake yasikie, mdomo wake uongee, haki yake sio kuimba bolingo bolingo ni kuhubiri injili  kwa njia ya nyimbo.
Biblia inasema  Roho wa Bwana yu juu yangu kwa maana amenitia mafuta kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao. Kwa hiyo hawezi kuhangaika, na upako na wa kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao ukafikiri ni kitu chepesi.  Sasa nimeingia ndani kidogo ili ujue, maana unapoona tunaomba hapa unaweza ukafikiri ni kitu chepesi. Kumbe Yesu alifanya vitu vizito ndani, na ndio maana  kama hajafunguliwa, unahitaji kunyunyiza damu ya Yesu mara ya kwanza,  mara ya tatu. Biblia inaniambia kuwa katika agano la kale walikuwa wanapewa kunyunyiza mara saba mahali pengine mara tatu, na mahali pengine  mara moja. Kwanini, inategema huyo mtu kesi yake imekaeje.
Sasa unaweza ukafikiri kuwa amefungwa kwa kosa moja lakini kumbe huko ndani amehesabiwa makosa matano, na yote  amehesabiwa kwa pamoja au tofauti.  Na yeye kaenda jela anatumikia makosa matano sasa wewe unaenda kushughulikia kosa moja.  Unamtoa kwa kosa moja anarudishwa ndani kwa kosa lingine ndio maana  utaona mwingine kuwa Unanyunyiza damu ya Yesu anafunguka kiasi, endelea kunyunyiza  hadi afunguke. Shetani atakuwa anapiga kelele huko ndani ili kile kingine alichoficha usikione.
*Sasa ngoja tufanye zoezi kidogo hapa, kama unaumwa……..*
Shaloom shaloom semina hii ni nzuri sana.. basi nenda YouTube kwa link pale juu kusikiliza maombi ☝☝☝(Sogeza hadi kule mwishoni ili usikilize maombi)... tuonane tena Kesho ✋✋✋✋✋
[10:55, 12/05/2018] Filix Bwanji: *5⃣SEMINA YA NENO LA MUNGU-DODOMA UWANJA WA BARAFU*
*MWL.CHRISTOPHER MWAKASEGE*
*SOMO: UWEZO WA MUNGU JUU YA MAGONJWA NA VYANZO VYAKE.*
*TAREHE  10 MAY, 2018*
*SIKU YA TANO*
*👉LINK YA SEMINA YA LEO YOUTUBE* https://youtu.be/DJL4Yo9SocI
*👉 NAMBA ZA SADAKA* https://goo.gl/Z3ozYB
*👉NAMNA YA KUPATA CD&DVD BONYEZA HAPA* https://goo.gl/tgwoub
*👉REDIO ZINAZORUSHA SEMINA HII* https://goo.gl/UzzqFP
Hakikisha unapata hizi CD au Kanda uendelee kusikiliza na kusikiliza usije ukaacha. Ni mambo ambayo unahitaji kusikia kwa sababu imani huja kwa kusikia na kadri unavyoendelea kusikiliza Mungu anakuwekea kitu ndani yako kwa sababu saa nyingine unaweza ukafikiri umedaka kila kitu wakati mwalimu akifundisha.
Ukija kusikiliza baadae ndipo unagundua pia kuna kitu kimekupita na hujasikia vizuri. Kwa hiyo unaposikiliza vizuri pia unaweza ukawa upo na wenzako na kupata muda wa kujadiliana Kibiblia juu ya mistari na mambo mbalimbali nitakayokuwa ninayozungumza.
Endelea kusikiliza na kusikiliza itakusaidia.
Leo nataka tuangalie
*UWEZO WA MUNGU JUU YA MAGONJWA AMBAYO CHANZO CHAKE NI URITHI WA ADHABU TOKA KWA WALIOKUTANGULIA*
Kuna mambo kadhaa tutayaona hapa.
JAMBO LA KWANZA
*I. KUNA MAGONJWA MENGINE NI ADHABU YA KIROHO INAYOTOKANA NA UASI*
*2 Mambo ya Nyakati 21:13‭-‬15*
_“lakini umeiendea njia ya wafalme wa Israeli, ukawaongoza Yuda na wakazi wa Yerusalemu kwenye kukosa uaminifu, kama walivyofanya nyumba ya Ahabu; tena umewaua ndugu zako wa nyumba ya baba yako, waliokuwa wema kuliko wewe; tazama, BWANA atawapiga pigo kubwa watu wako, na watoto wako, na wake zako, na mali yako yote; nawe utakuwa na ugonjwa mkuu kwa maradhi ya matumbo, yatakapotokea matumbo yako kwa sababu ya ugonjwa huo siku kwa siku.”_
Nataka uone hiyo adhabu ambayo mtu hupewa. Ndani ya adhabu kuna ugonjwa na ameeleza kabisa kuwa huu ugonjwa utaenda kuibukia wapi ni kwenye matumbo yake. Anaposema kwenye matumbo yake, wanaume wana matumbo matatu; wanawake wana matumbo manne:-
➖Kuna tumbo la chakula (chakula hukaa kwa muda mfupi)
➖Kuna utumbo mdogo
➖Kuna utumbo mkubwa
➖Kuna tumbo la uzazi (hili ni kwa wanawake tu)
Kwa hiyo anaposema hayo magonjwa yataenda kwenye matumbo anamaanisha kabisa na yanakuja kama adhabu na ugonjwa huu utakuwa unakuja mara kwa mara
*Kumbukumbu la Torati 28:15‭-‬16*
_“Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata. Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani.”_
Hapa anazungumzia juu ya laana zinazokuja kwa sababu mtu hajafuata maagizo ambayo Mungu amempa kwa wakati ule alipompa. Biblia inasema zitakapomjia na kumpata kutokuwa na furaha, amani, kutokufanikiwa hata kumwama n.k.
Hapo amesema hata kama uko wapi uwe mjini au mashambani usipofuata maelekezo Mungu anayokupa unaweza ukapata baadhi ya vitu nilivyotaja.
*Kumbukumbu la Torati 28:22*
_“BWANA atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa joto jingi, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie.”_
Unaweza ukaona hayo magonjwa yote yaliyotajwa hapo kuja kumpata mtu mmoja.
*Kumbukumbu la Torati 28:27‭-‬28‭, ‬35*
_“BWANA atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa. BWANA atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni; BWANA atakupiga magoti na miguu kwa jipu lililo zito, usilopata kupozwa, tokea wayo wa mguu mpaka utosi wa kichwa.”_
Mpaka hapo nimekuonesha kwa upande wa Mungu, pia zipo kwa upande wa shetani naye ana magonjwa kama hayo na mengine anayofungulia mlango anapogundua kwamba kuna maelekezo umekiuka kufuatana na mapatano yaliyokuwepo na adhabu mojawapo anayoweza kukuletea ni ugonjwa. Sasa si kila ugonjwa chanzo chake ni hiki, ndio maana nilikuwa nakuonesha vyanzo tofauti tofauti.
Dhambi ilipoingia ilituvuruga sana, lakini iliingiza kitu kikubwa mauti (mshahara wa dhambi ni mauti). Sasa toka mauti ilipoanza kutawala, iliachilia vitu vingi sana.
JAMBO LA PILI.
*2. ADHABU YA KIROHO INAWEZA KURITHIWA.*
*Kutoka 20:5*
_“Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,”_
Ukianza kuangalia kuna kitu Mungu anawaambia watu kuwa
*Kutoka 20:2‭-‬3*
_“Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi.”_
Sasa anasema _nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,_
Kibiblia kizazi kimoja ni wastani wa miaka mia moja (100 years). Sasa akisema kizazi cha tatu hiyo ni miaka mia tatu. Kwa hiyo usiposhughulikia hilo tatizo mapema linaweza likakaa kwenye familia kwa muda gani.
Unaweza ukapata shida sana na ikakupata shida sana.
Unaona adhabu ya kiroho unayoweza kurithi ndani ya familia
*2 Samweli 21:1*
_“Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa BWANA. BWANA akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni.”_
Huyu ni Daudi ametawala badala ya Sauli na katika kutawala kwake ghafla kukatokea ukame mfululizo miaka mitatu, mwishoni akaamua kuuliza. Inawezekana aliamua kunyamaza akidhani ni kitu kinapita tu na alipoona miaka miwili imepita akajiuliza kuwa hichi si kitu cha kawaida na kwa sababu ya uhusiano aliokuwa nao kwa Mungu aliamua kumuuliza Mungu. Na Mungu akamjibu moja kwa moja na kumwambia hii haijaja kwa sababu yako bali ni kwa sababu ya Sauli kwa kufanya kitu kwenye uongozi wake.
Angalia kwanini Sauli asipate adhabu yeye bali imekuja kwa mwingine? Ni kwa sababu *si tu kuwa amerithi nafasi na cheo lakini amerithi na adhabu*
Ukisoma habari za Sulemani alipomkorofisha Mungu, Mungu akaamua kurarua ufalme wake na kugawa na kumpa Kabila kumi (10) mfanyakazi wake na Kabila mbili (2) mtoto wake na akasema kuwa kinachonifanya nibakize Kabila mbili si kwa sababu ya mtoto wako bali ni kwa sababu ya Daudi. Kwa sababu nilimuahidi katika agano nililofunga naye kuwa hatakosa mtu wa kutawala la sivyo ningemnyang’anya kabisa, usimpate mtoto hata atakaekaa kwenye kiti lakini ni kwa sababu ya Daudi Mtumishi wangu. Yuda na Benjamini zikatawaliwa na mtoto wa Sulemani na Kabila kumi zikatawaliwa na mfanyakazi kama adhabu.
Bado swali linakuja pale pale kwanini Sulemani hakupata adhabu yeye akaja kupata mtoto wake?
Na hiki hakikuwa kitu chepesi sana kwao sababu unaona Daudi kile kiti kilichoweza kulinda nafasi akapata mtoto wa Sulemani (Mjukuu wake) kiti hicho hicho hakikumsaidia yeye kulindwa na adhabu ya kosa la Sauli kulikuwa na shida gani? Unahitaji kusoma sana Biblia kuelewa hivi vitu.
*Kuna vitu vichache ambavyo ninaweza kukueleza vikakusaidia baada ya kuviona ndani Biblia juu ya habari hii ya Daudi, Sauli na Sulemani:-*
Daudi alipoanza kutawala aliingia kama vile si kwa muda wa kwake, kwanini? Kwa sababu Sauli hakuacha kazi kikawaida alifukuzwa, na alipofukuzwa alikaa madarakani bila upako wa MUNGU kuwepo hapo. Ilipofika saa akafa Daudi alichukua ile nafasi pamoja na kwamba alikuwa ameshaandaliwa na kupakwa mafuta lakini alikuwa na kitu kingine kikubwa ambacho alitakiwa kukifanya.
Si suala tu la kwamba unaweza ukarithi kutoka kwa wazazi wako pia unaweza ukarithi kutoka kwenye nafasi uliyochukua. Tunaona Daudi akirithi adhabu mtoto wa Sulemani akirithi adhabu lakini si hilo tu, Daudi hakuruhusiwa kujenga hekalu kwa sababu mikono yake ilijaa damu. Na hata kufukuzwa kazi kwa Sauli ni baada ya kudharau maagizo ya MUNGU baada ya kupelekwa kule vitani. Kwa hiyo alifukuzwa kazi kwenye vita na Daudi akapewa kazi kwenye vita na kwa sababu hiyo alirithi kiti ambacho kilikuwa kinapigana vita/kinamwaga damu. Akajikuta na yeye akimwaga damu na kikamzuia na yeye kujenga hekalu.
Ngoja tuangalie tena  kile kitabu cha *Esta 1*
Watu wengi sana wanasoma kitabu cha Esta kama vile kimeanza na Esta, kitabu cha Esta hakikuanza na Esta sema tu Esta amechukua sura nyingi. Esta alikuwa mke wa pili wa Mfalme Ahasuero, mke wa kwanza aliitwa Vashti. Na siku moja Mfalme alikuwa amekaa mahali amefurahi na washauri wake wamemzunguka, Biblia inasema akataka Vashti malkia wamlete mbele ya Mfalme amevaa taji ya kifalme ili kuwaonyesha watu na maakida uzuri wake maana alikuwa mzuri wa uso.
Biblia inasema Vashti alikataa, *Esta 1:12-15*
_“Bali Vashti, malkia, alikataa kuja kwa amri ya mfalme kwa mkono wa wasimamizi-wa-nyumba; kwa hiyo mfalme akaghadhibika sana, na hasira yake ikawaka ndani yake. Basi mfalme akawaambia wenye hekima, walio na elimu ya nyakati; maana ndivyo ilivyokuwa desturi ya mfalme kwa wote waliojua sheria na hukumu; na karibu naye wameketi Karshena, Shethari, Admatha, Tarshishi, Meresi, Marsena, na Memukani, wale maakida saba wa Uajemi na Umedi, waliouona uso wa mfalme, na kuketi wa kwanza katika ufalme; akawauliza, Tumfanyieje Vashti, malkia, kwa sheria, kwa sababu hakufanya kama vile alivyoamriwa na mfalme Ahasuero kwa mkono wa wasimamizi-wa-nyumba?”_
Sasa nilitaka ujue ya kwamba huyu ndugu aligombana na mke wake halafu akapeleka kesi ya mke wake kwenye kikao cha wasaidizi wake kwa kutotii amri ya kuitwa naye na kukataa.
*Esta 1:19*
_“Basi mfalme akiona vema, na itoke kwake amri ya kifalme, nayo iandikwe katika sheria za Waajemi na Wamedi isitanguke, ya kwamba Vashti asifike tena mbele ya mfalme Ahasuero; na umalkia wake mfalme ampe mwingine aliye mwema kuliko yeye.”_
Nimekuonyesha vitu vichache lakini nilichotaka uone ni uangalie kilichotokea kwa Esta kwa sababu matangazo ya kwamba Ahasuero anataka mke mwingine ni baaada ya Vashti kufukuzwa, ndipo Esta alikopata nafasi ya kuwa mke wa Ahasuero.
Biblia inatuambia waebrania au wahahudi walipo tangaziwa kuuwawa,  Mordekai anaenda kwa Esta na kumwambia kuna tangazo limetoka kwamba waebrania wote watauwawa tunahitaji msaada wako zungumza na mfalme, lakini Esta alijibu kwamba imetoka amri kwa mfalme hakuna mtu anayeruhusiwa kumuona hata mimi mwenyewe mpaka kwa kibali maalum anyooshewe fimbo ya dhahabu la sivyo anauwawa.
Nilitaka uone ya kwamba sheria ile ile ambayo ilimwondoa Vashti naye akawekewa sheria, kitu gani ninachotaka kusema? Kwamba alikaa na kuchukua nafasi ya mke mwenzake aliyetangulia bila kusafisha kilichomwaondoa yule wa kwanza. Vashti na Esta hawakuwa ndugu lakini ile tu kwamba wanarithi kwenye kiti kuna kitu kiliachwa kwenye kiti usipokisafisha kinakufuatilia. Esta hakujua ya kwamba kilichovuruga uhusiano wake na mume wake ni kitu kilichoachwa kwenye kiti.
Sasa ukipata magonjwa ya kurithi ya mfumo wa namna hii yatakuhangaisha kweli mpaka hata hospitali, utapata tu dawa za kukupoozesha lakini maangaiko yake ni makali kwa sababu chanzo chake ni adhabu, usishughulikia hiyo adhabu huko kwingine huwezi vuka. Lazima uwe mwangalifu sana mfano wewe leo ni mke wa pili huyo mwenzako aliondokaje? Au wewe umeoa huo mwanamke alikuwa mke wa mtu mahali je waliachanaje?
YESU alitoa mfano huu: kaka mkubwa ana wadogo zake sita kaoa Biblia inasema hakupata mtoto akafa wakakubaliana mdogo mtu kumuoa huyo mama ili amtengenezee jina kaka yake ikaenda mpaka yule wa nne naye anakabidhiwa ili asaidie kumzalisha yule mama apate watoto watatu kwa ajili ya ndugu zake ndipo azae wa kwake,  naye akafa bila kupata mtoto ikaenda hivyo hivyo na hakuna aliye shtuka kwa hili na Biblia inasaema waliisha wote saba na yule mama akafa.
Sasa nilitaka uone na kujua ya kwamba kuna nafasi zinabeba vitu vya kurithi vingine vizuri na vingine vibaya. Angalia mwenzako ili ujue unakaaje kwenye hiyo nafasi ili uweze kufanikiwa ili kama kulikuwa na kitu cha ugonjwa kinachosumbua kila mtu anayekaa kwenye hiyo nafasi usijifanye kwamba mimi sitapata shida.
Nilienda ofisi moja mtu wa ofisi nyingine aliponiona nimeingia kwenye hiyo ofisi akaja akanitafuta akasema ninashida ninahitaji maombi, nikamuuliza unahitaji maombi wapi akasema ofisini kwa hiyo nikaenda ofisini kwake akasema unaiona hii oifisi ufunguo nakaa nao mwenyewe, nafungua mwenyewe na kufunga mwenyewe madirisha na kila kitu, akasema siku moja niliingia ofisini nikakuta kwenye kiti kuna ndege amekufa nikatazama kila mahali madirisha yote yamefungwa, milango imefungwa na mimi ndio mwenye ufunguo ndege amekufa kwenye kiti. Nikamuuliza sasa ukafanyaje akasema nilimtoa na nikawaambia wafanyakazi wamwondoe hapo, ila tangu wakati huo nimeanza kuumwa sikuwa na muda sana kukaa hapo nikamweleza namna ya kuomba kwa sababu kuna maombi mengine unamwita tu mtu unamchoma tu sindano lakini kuna maombi si ya kuchoma sindano unamweleza vitu vya kufanya kwa hatua, nikaomba Mungu amsaidie kwenye hizo hatua kwa sababu nilikuwa nasafiri kwenda mahali pengine nikaondoka baada ya miezi kadhaa nikasikia amekufa. Liliniingia moyoni mwangu anaye mbadili ile ofisi! sijui hata ni nani aliyembadili lakini nikisoma habari za akina Daudi, Vashti na Esta siachi kujiuliza maswali ya namna hiyo
Mfano mwingine
*2Wafalme 17:24-29*
_Naye mfalme wa Ashuru akaleta watu kutoka Babeli, na Kutha, na Ava, na Hamathi, na Sefarvaimu, akawaweka katika miji ya Samaria badala ya wana wa Israeli; wakaumiliki Samaria, wakakaa katika miji yake. Basi ikawa, wakati ule walipoanza kukaa huko, hawakumcha BWANA; kwa hiyo BWANA akapeleka simba kati yao, nao wakawaua baadhi yao. Kwa hiyo wakamwambia mfalme wa Ashuru, wakasema, Wale wa mataifa uliowahamisha, na kuwaweka katika miji ya Samaria, hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi; kwa hiyo amepeleka simba kati yao, na tazama, wanawaua, kwa sababu hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi. Ndipo mfalme wa Ashuru akatoa amri, akasema, Mpelekeni mmojawapo wa makuhani, mliowachukua kutoka huko; aende akakae huko, akawafundishe kawaida ya Mungu wa nchi. Basi mmoja wa makuhani waliochukuliwa kutoka Samaria akaenda akakaa katika Betheli, akawafundisha jinsi ilivyowapasa kumcha BWANA. Lakini pamoja na hayo watu wa kila taifa wakajifanyia miungu yao wenyewe, wakaiweka katika nyumba za mahali pa juu, walipopafanya Wasamaria, kila taifa katika miji yao walimokaa._
Biblia inatueleza jinsi mfalme Ashuru alivyopigana vita na wana wa Israeli akawashinda akaamua kuwahamisha wana wa Israeli kutoka eneo la Samaria na akawaleta watu wengine kutoka Babeli na kutha na Ava, na Hamathi, na Sefarvaimu .
Hawa wameondolewa wamekuja wapya kwa lugha ya kawaida wamerithi eneo ambalo halikuwa lao hapo mwanzo, hawa walikuwa na Mungu wao ambaye walikubaliana namna ya kuishi naye pale na taratibu za eneo la pale na ile ndio ilikuwa inatengeneza nidhamu. Biblia inasema kumcha Bwana maana yake hofu ya Mungu na inatengeneza nidhamu ya eneo Biblia inasema kumcha Bwana ni kukataa uovu ni chanzo cha maarifa, kumcha Bwana ni chanzo cha hekima ndio iliyokuwa inatengeneza nidhamu. Sasa watu hawa wamehamishwa na walipohama waliacha Mungu wao hapo hawakuondoka na vitu vilivyoweka alama ya Mungu wao hapo, hawa wageni wanakuja na wao wana miungu yao wamekaa wakashangaa simba wanatokea wakaanza kuwararua walipotafuta kujua wakagundua hii ni adhabu wanapata na ni kwa sababu hawaishi jinsi Mungu wa nchi anavyotaka, sasa ili simba aache kuwavuruga wakatafuta kuhani aje awafundishe namna ya kukaa na Mungu wa nchi na aliwaeleza taratibu wakaanza kuzifuata na simba akanyamaza maana hatuoni tena akiwavuruga lakini baadae wakaona tunaweza kuendelea na miungu ya kwetu na bado tukamcha Bwana.
Hujawahi kuona unatoka eneo moja kwenda eneo jingine au mikoa au ulikuwa eneo moja una nyumba ya kupanga una hamia eneo jingine na unakaa kwenye nyumba ya kupanga, ghafla usiku hulali unaanza kuugua tu unapata shida unapohangaika namna hiyo utapata tu watu wa kukupa taarifa watakuambia eneo kama hili huwezi kukaa tu hivi hivi lazima uzungumze na makuhani wa hapa wakusaidie namna ya kukaa na mungu wa hii nyumba, na ukristo wako unaenda kutafuta na unarudi na masharti ya kila namna ambayo na wewe unaenda kuyaongezea kwenye nyumba ya kwako ukienda kanisani unamsifu Mungu kwelikweli, lakini nyumbani kwako umeweka mlinzi mungu mwingine baada ya muda hiyo vurugu iliyopo nyumbani itaendelea kukusumbua.
Watu wengi hawajajua unaporithi eneo saa nyingine Roho Mtakatifu atakusaidia kukueleza kuna kitu gani mahali pale  ili uweze kuomba na mambo yapo kwenye Biblia. 60% ya maisha ya kwetu tuko kwenye nyumba za watu wengine huwezi ukasafiri kama tunavyosafiri Mungu asikuonyeshe hivi vitu utateseka sana kwa sababu huwezi jua mwenye hotel amesemea maneno gani kwenye msingi, hujui ameenda wapi kutafuta msaada ili apate wateja  si unajua kila mtu ana uhuru wa kutafuta msaada wa kiroho popote, anapoona ni bora kwake lakini sasa wewe  unapoingia pale hujui kawaida ya mungu wa ile hoteli, ni shida gani unaileta kwa mungu wa ile hoteli au kawaida ya Nyumba uliyopanga ghafla unaanza kupata shida usiku ukitaka kujua tofauti ukilala hapo siku mbili au tatu unakuta una maumivu na magonjwa yasiyo chanzo lakini asubuhi unajikuta upo mzima,  shida ukirudi tu kulala kwa hiyo unaanza kuogopa kulala. Ukitaka kujua tofauti kesho yake unaweza kwenda sehemu nyingine ukalala unashangaa unalala vizuri, kama huamini tafuta bwana afya magonjwa ya kuambukiza wakishajua kulikuwa na mgonjwa hapa hata ndugu zako hawaruhusiwi kuingia au kushika nguo zake mpaka washughulikie kile chumba kwa sababu wanajua ule ugonjwa bado upo kwenye chumba. Hata kwenye sayansi ya kawaida wanajua kuna magonjwa mengine  hata ukimtoa mgonjwa yanabaki kwa hiyo lazima watafute utaalamu wa kushughulikia kile chumba mpaka baada ya muda ndio mpewe ruhusa ya kuingia, kuna maeneo yanakuwa na tatizo la magonjwa ya kuambukiza namna hiyo watu wanahamishwa au waliopo kule ndani hawaruhusiwi kutoka mpaka watibiwe na wengine hawaruhusiwi kuingia. Tunaposafiri kwenda nchi mbalimbali unapofika airport kwenye nchi mojawapo wanakuuliza umetokea wapi? unasema, umepita nchi Fulani? au kuna kitu chochote ubeba kutoka nchi fulani unawaambia hapana wanakuruhusu baadae ukiuliza kwenye nchi fulani kuna kitu gani utaambiwa kuna ugonjwa wa kuambukiza umeanza. Kwa hiyo ungesema tu umetokea nchi gani tu wanakubana!
Nimezungumza kwa mapana kidogo ili uweze kujua  tunapozungumzia juu ya adhabu ya kurithi ya magonjwa yanayo tokana na  kurithi lazima uweze kufahamu si tu kwamba inatoka kwenye uzao lakini pia inatoka kwenye nafasi na pia inatika kwenye eneo.
JAMBO LA TATU
*MRITHI NI YULE ANAEPOKEA KITU KUTOKA KWA MWINGINE NA KINAKUWA CHA KWAKE KWA SABABU YA JAMBO HALALI LINALOWAUNGANJSHA*
*Waebrania. 1:1‭-‬4*
_Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu; amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao._
Kwa hiyo jina la Yesu halikuwa jina la Yesu, lilikuwa jina la baba yake alimpa mtoto wake na likawa lake kihalali, kwa hiyo kama Yesu amerithi halikuwa lake.
*Yohana 5:43*
_Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo_
Anasema jina la Yesu sio langu nimekuja kwa jina la baba yangu wala hamkunipokea lakini mwingine akija kwa jina lake mnampokea huyo, sasa huyu ni Yesu anasema.
*Yohana. 17:1‭, ‬6‭-‬6‭, ‬11*
_Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe; Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika.  Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo_
Anaweka msisitizo “kwa jina lako ulilonipa” ili tujue kuwa jina hilo halikuwa lake ila amelirithi kihalali na likawa lake
*Wafilipi. 2:9‭-‬11*
_Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba._
Kama Mungu angekuwa na jina jingine basi jina la Yesu lisingekuwa jina lipitalo kila jina, msomaji wa biblia kama unataka kufuatilia jina la Yesu alipewa mara tatu, kwa njia tatu, na kwa sababu tatu tofauti. Anapozungumza anasema “kwa hiyo tena” alipewa alipokuwa mtii hata mauti yaani alipofufuka na hata alipozaliwa alipewa hilo jina kwa sababu lilikuwa na kazi yake, kama unataka kufuatilia juu ya jina la Yesu itakusaidia kuimarisha imani yako juu ya Mamlaka iliyomo ndani ya jina lake, kama ukijua sababu aliyopewa hilo jina na nafasi iliyopo.
Ukija kwangu jina langu naitwa *CHRISTOPHER MWAKASEGE* kwako wewe ni jina la mtumishi, kwa mke wangu ni jina la mume wake, kwa watoto wangu ni jina la baba yao, kwa hiyo mke wangu akiliita kwa nafasi yake kama mke jina linachukua heshima yake, watoto wangu wakiliita jina linachukua heshima yake na wapendwa wakiniita jina linachukua heshima yake, lakini ni mtu yule yule mmoja lakini wamelipata kwa aina tofauti, mke wangu amelipata kwa kuolewa, watoto wangu wamelipata kwa kuzaliwa na wapendwa wamelipata kwa kusikia mtumishi wa Mungu. Kasome juu ya jina la Yesu nakufundisha tu juu ya mambo ya kurithi.
Ndio maana ukisoma kitabu cha warumi inasema “tunapokuwa wana wa Mungu tunakuwa warithi wa Mungu” na kwa sababu hiyo mtu aliyeokoka anaweza akalitumia hilo jina na likafanya kazi lakini kwa ambaye hajaokoka kuna mahali anaweza kulitumia na lisifanye kazi kwa sababu sio mrithi kihalali. Na biblia inasema sisi tumeirithi pamoja na Kristo na moja ya tulichorithi ni jina la Yesu
Biblia inasem Yesu ni kichwa na kanisa ni mwili wake, kwani nani anagawa kichwa tofauti na mwili tofauti, kwa hiyo kama kichwa kinaitwa Yesu na mwili unaitwa Yesu kwa sababu kichwa ni cha Yesu na mwili ni wa Yesu. Sasa utaelewa kuna msitari umeandikwa “ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu wakijinyenyekesha” huo mstari sio wa kila mtu ni kwa ajili ya wale walioitwa kwa jina lake, na ili uitwe kwa jina hilo ni lazima uwe mwana. Hebu tuangalie huu msitari kwanza ili uweze kujua kabla hatujaanza kushughulika na magonjwa ya kurithi
*Wagalatia 4:7*
_Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu._
*Wagalatia 3:27*
_Na kama *ninyi ni wa Kristo,* basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi_
Ule msitari wa 29 unaonesha umiliki wa sisi kuwa wa Kristo, maana yake sisi ni mali ya Kristo yaaani Yesu anapokuwa Bwana sisi tunakuwa mali yake. Neno “BWANA”linatoka kwenye neno la kiingereza “LORD” linaunganishwa na property kama vile unavyoweza kusema “simu yangu”, “nyumba yangu” kwa hiyo hata wale wa Kristo yaani mali yake, sasa biblia inasema hivi sisi ni warithi yaani watoto wa Ibrahimu na Ibrahimu alipewa ahadi ya kwamba hii ahadi ni kwa ajili yako na uzao wako milele sasa kwa sababu wewe sasa umekuwa uzao wa Ibrahimu unaingizwa kwenye urithi wa Ibrahim sawa sawa na ahadi.*sasa huwi mrithi wa Ibrahim kwa sababu umeomba, bali unakuwa mrithi kwa sababu wewe umekuwa mkristo* napoenda Israeli kati ya jambo ninaloomba kwa Mungu ni kuwa “namshukuru Mungu kwa sababu umenirudisha tena nyumbani” kwa sababu hii nchi ni ya kwangu ki-ahadi sawa sawa na Ibrahim kwa jinsi ya kuzaliwa kwa mwili, mimi ni mtanzania lakini kuzaliwa kwa jinsi ya Rohoni ninaingizwa kwenye urithi ambao  kwa jinsi ya kibinadamu siwezi kuupata  kwa hiyo ninakuwa ni mtoto wa Mungu. Lakini kwa kuwa Yesu ni uzao wa Ibrahimu na mimi naingizwa kwenye uzao wa Ibrahimu na mrithi sawa sawa na ahadi. Kwa hiyo kuna vitu kwenye biblia Mjngu alimuahidi Ibrahimu na uzao wake, kwa hiyo na mimi nakuwa na uhalali wa kwenda mbele za Mungu kusema hivi ni vya kwangu.  Na Damu ya Yesu itanipa.
Lazima kuwa na uhalali wa jambo fulani, linalosababisha urithi ugonjwa na uwe kama wa kwako, lakini ni wa kurithi lakini ungekuwa wa mtu mwingine ungeweza kuusukuma na ukakimbia.Lakini kwa sababu ni wa kurithi na huwezi kuwa mrithi hado kuwe na kitu, ulichokipokea kutoka kwa mtu mwingine na kikawa chako kihalali kwa sababu kuna jambo halali linalo waunganisha na mtu mwingine. Huyo aliyekuwa na ugonjwa na ikasababisha na wewe ulipochukua tu nafasi,  na wewe ukawa mlengwa.
*USHUHUDA*
Tuliambiwa habari za mama mmoja aliyekufa kwa kansa, alafu tuliambiwa  na mama yake mzazi alikufa kwa kansa akiwa na umri huo huo. Tukaangalia na tuliambiwa habari za baba mmoja ambaye ndugu yake wa kiume alikufa na ugonjwa huo huo na Yeye alikuja kufa kwa ugonjwa huo huo.
Nilikuwa mahali fulani niliambiwa habari za mama mmoja kuwa alikuwa na shida na mguu wake ulikuwa na shida na anatembea kwa shida,. Kwa hiyo wakaniambia anataka kuniona. Basi nikamfuata  mahali alipokuwa. Kwa hiyo aliponiona  akaanza kulia na kusema Mwalimu naomba nisaidie maombi, wasikate mguu wangu. Nikautazama mguu wake  umefungwa bandeji. Nikamuuliza mguu wako una shida gani akasema shida ni sukari.  Alisema nina ndugu 30 wote wana kisukari na kati ya hao 10 wameshakatwa miguu. Naomba ombea wa kwangu usikatwe.
Sasa unamsaidiaje mtu wa namna hiyo, sio kazi nyepesi  aliniambia kuwa kama kidonda chake hakitapona basi mguu wake utakatwa. Akasema mwalimu naomba ombea mguu wangu.  Lakini tatizo sio mguu, tatizo sio sukari, tatizo ni chanzo uhalali uliopitisha kutoka pale na pale.
Nyumbani kwa  Ibrahimu kulikuwa nan shida na unahitaji kufuatilia, alioa mwanamke wa kwanza Sara na akawa na tatizo la kupata mtoto japo baadae alikuja kupata lakini alizaa na msichana wa kazi. Kasome biblia yako, Isaka ambaye alichukua agano na yeye akaoa mke na akapata shida ya kuzaa. Mke wa Yakobo mtoto wa Isaka mke aliyempenda (Raheli)  nae alikuwa  anapata shida ya kupata watoto.  Shida ya kupata watoto haikuwa ya wale wamama bali ilikuwa katika nyumba ya Ibrahimu.
Nilienda mkoa mmoja  nikakuta mtu mmoja aliniambia kuwa wametoka kwenye msiba mahali,  mama fulani kafiwa na mtoto wake.  Wakaniambia huyu ni dada wa nne kwenye familia kufiwa na mume na amebaki mmoja tu mwenye mume. Wote wanaugua wanakufa, kwa hiyo wote wanne ni wajane. Sasa huyu aliyebaki akiugua na ukaanza kuombea ugonjwa tu kawaida  usije ukashangaa na yeye ukimpoteza kwa hiyo lazima ujue kuwa kuna kitu fulani kinamfuatilia.
Dada mmoja alipata kansa ya ziwa (matiti)  alisema naomba niombeeni maana hata mama yangu alipata kansa ya matiti na akakatwa titi lake na akafa. Mwingine alikuwa ananisimulia jinsi baba yake alivyokufa hana meno maana yote yaling’olewa na alisema hata babu yake nae alikufa meno yake yakiwa yameng’olewa yote. Kwa hiyo babu na baba walikufa wana meno ya bandia wote. Kwa hiyo na yeye meno yake yalianza kupata shida, anatafuta msaada wa maombi. Sasa si kila ugonjwa wa kurithi una tatizo  la kiroho ndani yake.  Sasa si kila ugonjwa huu unaweza kutatuliwa hospitali na ndio maana watalaam wanaweza kukueleza chanzo chake.
Kwa hiyo sisemi usiende hospitali maana wao watakusaidia namna ya ‘ku manage ugonjwa”  na utapata kitu kikubwa cha kukusaidia ila nakuambia ili kuumaliza ni lazima ushughulike na chanzo.
*Tutaenda kuomba hapa kama kuna shida ya ugonjwa wa kurithi kwenye ukoo wenu andika jina la ugonjwa  (tutumie maombi yako kwa namba pale juu za sadaka au tuandikie kwa tovuti ya kwetu au tuma kwa ukurasa wa facebook (inbox).*
Kwa hiyo tutaenda mbele za Mungu mimi na wewe tuombe kwa Mungu atupe utatuzi wa chanzo chake, vitu vingine Mungu atasema na wewe moja kwa moja kwani hatufanani, tuombe rehema zake
Magonjwa ya kurithi yanasumbua na kama hayapo kwako unatamani watoto wako, wajukuu wasipate, kwa hiyo yapige ribiti yasiende kizazi kingine. Usiseme mimi niko okay, nimeokoka niko okay. Kamuuliza Daudi atakusimulia alipakwa mafuta mara tatu, lakini alirithi adhabu ya Sauli. Kwanini ule upako usimsaidie? Ni kwa sababu kuna sheria katika ulimwengu wa roho. Ila sheria ikidai katika ulimwengu wa roho usijue kitu cha kufanya, huwezi maliza hili tatizo.
Maombi ya kunena kwa lugha………..
Mungu anatusemsha mambo ya ndani maana  ningeweza kukuhubiria au kukuombea kwa mistari hii hii ila sasa natamani uingie jikoni kidogo ujifunze na wewe ujue hata mchuzi unakakorogwaje?.usije ukalala njaa… kazi ya  mwalimu ni kuachilia vitu alivyo navyo ndani ili watu wengine viwasaidie.
Unajua inapofika mahali biblia inasema nikatafuta mtu miongoni mwao, kuna watu wengine ambao wanaogopa hadi kwao maana wameona mfululizo fulani wa matukio, kila wakienda hawakai au wanaugua, na hawakai na akirudi anakuwa hayuko kama alivyoenda.
Tulienda mkoa mmoja na  tulimkuta mama mmoja akihitaji maombi, maana mimba kama sita hivi ziliharibika hivi. Tukaomba akapata watoto watatu.  Tulipokutana nae alipokuwa na mtoto wa tatu kuwa anataka kuwapeleka watoto kwa wazazi wake, na tulimuuliza kwanini hujawapeleka alitueleza vitu vigumu sana.  Sasa huyo ni mama wa watoto  alitueleza vilivyompata na mpaka alipokutana na Yesu na Yesu alimsaidia. Na alisema nafahamu nikiwapeleka katika mazingira haya na wao watafanyiwa vitu ambavyo na mimi nilifanyiwa. Utasema naongea kitu gani, kuna mungu wa familia, kila mtu anaingia kwenye hiyo familia kuna vitu inatakiwa afanyiwe maana bila hivyo kuna vurugu itatokea..
Wewe ambaye unafuatilia somo hili taja jina lako mbele za Bwana na ugonjwa ambao wa kurithi unawasumbua.  Tumwamini Mungu…….. (Tuma maombi yako kwenye namba za sadaka)
Nenda Youtube kasikilize maombi  Youtube kwenye link niliyoweka pale juu☝☝☝
Barikiwa sana na  Bwana Yesu na atakuvusha.
[12:01, 13/05/2018] Filix Bwanji: *6⃣.SEMINA YA NENO LA MUNGU DODOMA UWANJA WA BARAFU*
*MWL.CHRISTOPHER MWAKASEGE*
*SOMO: UWEZO WA MUNGU JUU YA MAGONJWA NA VYANZO VYAKE.*
*TAREHE  11 MAY, 2018*
*SIKU YA SITA*
*👉REDIO ZINAZORUSHA SEMINA HII* https://goo.gl/UzzqFP
*👉 NAMBA ZA SADAKA* https://goo.gl/Z3ozYB
*👉LINK YA SEMINA YA LEO YOUTUBE* https://youtu.be/96oxGlY0TmE
*👉NAMNA YA KUPATA CD&DVD BONYEZA HAPA* https://goo.gl/tgwoub
Leo ikiwa ni siku yetu ya sita au mfululizo wa sita kama upo hapa mjini Dodoma hakikisha unapata CD yako au ukiwa mbali na una ndugu au rafiki yako hapa unaweza kumwambia akuandalie CD au Kanda ili usikilize na kusikiliza.
Jana tulikuwa tunajifunza magonjwa ambayo chanzo chake ni urithi wa adhabu toka kwa waliokutangulia. Na tuliangalia vitu kama vitatu, nitavitaja tu ili kama ndio mara ya kwanza kushiriki tuweze kuenda kwa pamoja.
➖Jambo la kwanza lilikuwa ni *kuna magonjwa mengine ni adhabu ya kiroho inayotokana na uasi*
➖ Jambo la pili ni *adhabu ya kiroho inaweza kurithi wa hasa adhabu inayojifungua nje kwa njia ya magonjwa* na
➖ Jambo la tatu nilikuambia *mrithi ni yule anayepokea kitu cha mwingine na kinakuwa chake kwa sababu ya jambo halali linalowauganisha*
Leo tutajifunza kuhusu jambo la nne
*4. HATUA ZIFUATAZO ZITAKUSAIDIA KUKUPA MWONGOZO WA KUOMBEA UPONYAJI WA MAGONJWA YA KURITHI*
Hatua hizi zinabaki kuwa kama mwongozo na Mungu anabaki kuwa Mungu anaweza akamponya mtu saa yoyote anavyotaka, anaweza asifunguke na hizi hatua ninazotaka kusema.
Nakupa hatua hizi ili zikusaidie kujua Biblia inazungumza kitu gani juu ya namna ya kutoka kwenye tatizo la namna hii ili uweze kutumia kwa sababu kati ya jambo mojawapo ambalo Mungu
➖Analifuatilia ni neno lake apate kulitimizà.
➖Analithibitisha neno lake kwamba ni la kwake.
➖Neno lake linatupa kujua mapenzi yake ili tukiomba lolote kwa jina lake tuweze kulipokea na tuna uhakika kuwa anatusikia.
Ningeweza nisikuambie hizi hatua bali nikakuombea kwa kutumia hatua hizi bila kujua kwamba ni hatua ipi kwa maana ningeomba tu mfululizo. Kwa sababu si watu wote/wengi sana saa wanaombewa huwa wanasikiliza sala inayotumika kuwaombea kwa sababu saa hiyo unachowaza ni kupokea muujiza wa wako, uponyaji wake bila kufikiria huyu mwingine anaombaje.
Hata ukisoma katika Biblia wengi sana watatazama mgonjwa aliyeponywa na Yesu, hawataangalia Yesu aliombaje wakati anamponya yule mgonjwa
Ukiwa Mtumishi wa Mungu utaangalia upande huu kwanza kuwa Yesu aliombaje kwa sababu ndivyo alivyosema kuwa kile ninachokifanya nanyi mtakifanya na vikubwa kuliko hivi mtavifanya kwa sababu naenda kwa Baba.
Biblia inasema Yesu ni mtangulizi ili sisi tufuate kwa hiyo tunaangalia, alivyokanyaga, alivyosema na alivyoomba. Pia lazima tuangalie huyu mwingine alieponywa kwa sababu na wewe siku moja unaweza ukaugua, ili ujue namna ya kupokea uponyaji kwa sababu saa nyingine unaweza ukafikiri walio wahubiri hawaugui kumbe wanaugua na wao na Mungu hana upendeleo kwa sababu taratibu za uponyaji ni zile zilizopo kwenye Biblia.
Saa nyingine nakutana na watu wanasema wameombewa wengine wamepona ila yeye bado ni mgonjwa, je kuna shida gani. Ni kwa sababu alikuwa ana imani ya kuombewa wengine na KUPONA lakini yeye imani hakupokea kwa sababu mistari ya kuombea ni tofauti na ya kupokea ni tofauti.
Kwa hiyo nimeona niweke huu utangulizi kwa hizi hatua ili tuweze kufahamu, pia na Mungu anaweza akakupa na zingine ambazo sitazitaja.
Leo tuanze kwa hii hatua ya kwanza
HATUA YA KWANZA.
*1. KUBALI MOYONI MWAKO YA KUWA JAMBO LA URITHI WA MAMBO YA KIROHO NI JAMBO LA KISHERIA KATIKA UTENDAJI WA ATHARI ZAKE NA UTATUZI WAKE*
*Warumi 8:1‭-‬4*
Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili; ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.”_
Kaweka mambo mazito katika maneno machache, Biblia inatuambia kuna sheria katika ulimwengu wa roho kama ilivyo katika ulimwengu wa mwili na zina kazi yake.
Ukienda katika Biblia kuna kazi za sheria ambazo hazina utofauti sanaa na kazi za sheria ambazo tunazifahamu zilizopo sema tu ndani ya Biblia wamekupanulia vitu vingine kidogo kwa kukutana na sheria na amri unahitaji kuzijua.
Sheria Zina kazi mbalimbali na mojawapo ni
>Kutengeneza mfumo wa maisha.
➖Sheria ya Shule ni kutengeneza mfumo katika shule.
➖Sheria za nchi kazi yake ni kutengeneza mfumo wa maisha katika nchi
➖Sheria katika kijiji kazi yake ni kutengeneza mfumo wa maisha katika kijiji husika
➖Sheria katika kazi, kazi yake ni kutengeneza mfumo wa maisha pale kazini.
Biblia inatuambia sheria ni kiongozi kwa kusema Torati ni kiongozi kwa Wakristo, kwa hiyo sheria inatupeleka mahali. Sheria haikai tu hewani. Ukisoma kwenye Biblia, inasema _“bila maono watu huacha kujizuia, ana heri anayefuata sheria”._ Kwa hiyo kazi ya sheria ni kulinda maono
Lakini pia kufuatana na huu mstari tuliosoma kazi ya sheria ni kumuweka mtu huru. Biblia inasema “hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.” Sasa watu wengine hawasomi mstari unaofuata, mstari wa pili utaona sababu kwa kusema _“Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru,”._
Kwa hiyo si suala tu kwamba hakuna hukumu ndani yao walio katika KRISTO YESU hiyo hukumu haiwezi kuwasumbua kama watajifunza kutembea katika sheria ya ROHO wa Uzima. Kwa sababu hiyo sheria ya ROHO wa Uzima ndiyo inayotumika kukuweka huru mbali na sheria ya roho wa mauti, roho ya dhambi.
Kwa hiyo inamaanisha ya kwamba sheria ya dhambi ina mfumo fulani inatengeneza, kuna mahali inakupeleka, kuna mahali inalinda na kuna kitu ina linda. Na kuna sheria ya mauti, dhambi na mauti vinafanya kazi pamoja maana mshahara wa dhambi ni mauti. Mauti haikupata nafasi mpaka dhambi ilipoingia.
Kwanini nimeanza hatua hii? Kubali moyoni mwako suala la urithi ni suala la kisheria na kama tunazungumzia urithi wa kiroho inamaanisha kuna sheria za kiroho zinazohusiana na urithi kama vile masuala ya kawaida ya urithi hapa duniani lazima uende kwa sheria. (Sheria ya mirathi inaweza ikafanya mali nyingine za kwako zisiwe za kwako)
Mfalme Hezekia aliambiwa tengeneza mambo ya nyumba yako kwa sababu utakufa. Shida haikuwa kazini au kwenye huduma ilikuwa nyumbani ndiyo maana hakuambiwa tengeneza mambo ya ofisini au hudumani, alikuwa anataka kuondoka kabla ya kuweka mambo sawa, MUNGU akampelekea ujumbe wa kuweka mambo yake sawa maana ataondoka. Hezekia akagundua siku zilizobaki yawezekana ni chache na mambo ya kutengeneza ni mengi akaomba aongezewe muda, akapewa miaka 15.
Mambo ya mirathi ni sheria, na sheria ndiyo itakayokupa au kukunyima. Inapofika katika masuala ya kiroho  kubali ndani ya moyo wako kwamba katika Agano jipya kuna sheria, kwa sababu watu wakishaokoka wanazitazama sheria vibaya kwa sababu ya sura ya torati wakifikiri ya kwamba tunatakiwa kuishi kama torati. Fahamu jambo hili, YESU hakuja kutangua wala kuondoa torati au sheria, alikuja kutimiza na kusaidia palipo pungua na upungufu mmojawapo mkubwa  ni kwa sababu mwili ulikuwa hawezi kutii sheria zote zilizowekwa (Hakuna namna mwili ungeweza kutii sheria zote alijaribu akagundua haiwezekani) ndiyo maana akasema nitafanya Agano jipya na ndani ya Agano jipya nitaandika sheria yangu ndani yao. Kwa hiyo siyo kwamba sheria zinaondolewa bali unarahisishiwa namna kutembea ndani yake. Sasa katika kule kurahisishiwa usije ukafikiri sheria imeondoka. Kwa hiyo haja ya kuwepo sheria iko pale pale ile kwamba huko chini ya neema haina maana sasa ukae mbali na sheria, sheria inabaki pale pale.
Hutamwambia MUNGU aondoe sheria za amri kumi! Hatoi! Neema inapokuja ndani yako inakuondolea kiu ya kuua, kuiba, kuabudu miungu mingine. Lakini kama hiyo kiu imeisha sheria inabaki pale pale ukiondoka kwenye neema sheria iko pale pale ili ikuzuie usiibe na ujue kosa liko pale pale. Hii ni ili ujue ya kwamba ndani ya neema ya KRISTO tunapewa tuwe warithi pamoja naye, tunaorithi pamoja na KRISTO, iko neema inayotusaidia lakini lazima ujue kuna sheria ya ROHO wa Uzima, yule yule aliyetufanya tuwe warithi pamoja na KRISTO anao utaratibu wa kwake.
HATUA YA PILI
*OMBA MUNGU NA TAFUTA KUJUA UGONJWA WA KURITHI UMEUPATA KUPITIA NJIA IPI HADI UKAKUFIKIA*
Kama ulikuwepo jana nilikuwa  nakufundisha na kukwambia huwezi kurithi kitu cha kwako. Ukiwa mrithi maana yake unarithi cha mwingine, kikaja kwako kihalali. Ule uhalali umefanya kitu cha mwingine kimekuwa cha kwako halali. Kwa hiyo kama kuna ugonjwa ambao umekuja kama sehemu ya adhabu ya kiroho na umekufikia tafuta kujua umepitia njia ipi na MUNGU atakupa ufahamu.
*NJIA YA UZAO*
Jana nilikupa mifano michache ya kwamba unaweza ukapitia kwenye *UZAO/KIZAZI*
*Kutoka 20:5*
_“Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,”_
Kwa hiyo kuna magonjwa ya kurithi ambayo unayapata mahali ulipozaliwa/ kwenye ukoo au familia uliyozaliwa
*NJIA YA NAFASI*
Lakini pia jana nilikupa mfano wa *NAFASI*
*2Samweli 21:1*
_“Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa BWANA. BWANA akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni.”_
Kipindi cha Daudi kulikuwa na njaa miaka mitatu mfululizo, mwaka kwa mwaka na Daudi akatafuta uso wa BWANA kumuuliza kulikoni, na MUNGU akamwambia ni kwa sababu ya Sauli ambaye alimwaga damu. Kwa hiyo aliporithi nafasi alirithi na adhabu iliyokuwa pale bila yeye kujua. Na MUNGU anajaribu kumuonesha ya kwamba hii adhabu haijaja kwa ajili yako umeikuta kwenye nafasi uliyoingia. Na kwa sababu wewe ndiyo uliyoikuta na inakutesa wewe huyu mwingine aliyeondoka si kazi yake kuiondoa bali ni kazi yako wewe kuiondoa.
Na jana nilikupa mifano, mpaka tukaangalia mfano wa *ESTA* alipata shida kwenye ndoa na Ahasuero kwa kutumia sheria iliyompiga marufuku kuonana na mume wake mpaka aitwe na alipata hiyo shida kwa sababu hakushughulikia tatizo lililomwondoa mke wa kwanza wa Ahasuero aliyeitwa Vashti, kwa sababu naye aliondolewa kisheria.
Kwa hiyo inategemea nafasi, inawezekana ni nafasi ya ofisini au ya kwenye familia. Kwenye nafasi ya kwenye familia utakuta mke,watoto,mume lakini pia ndani ya watoto kuna nafasi ya mzaliwa wa kwanza na wa mwisho wanavitu vya kwao Kibiblia.
*NJIA YA ENEO*
Jana pia nilikuwa mfano wa *Eneo*
*2Wafalme 17:24-29*
_“Naye mfalme wa Ashuru akaleta watu kutoka Babeli, na Kutha, na Ava, na Hamathi, na Sefarvaimu, akawaweka katika miji ya Samaria badala ya wana wa Israeli; wakaumiliki Samaria, wakakaa katika miji yake. Basi ikawa, wakati ule walipoanza kukaa huko, hawakumcha BWANA; kwa hiyo BWANA akapeleka simba kati yao, nao wakawaua baadhi yao. Kwa hiyo wakamwambia mfalme wa Ashuru, wakasema, Wale wa mataifa uliowahamisha, na kuwaweka katika miji ya Samaria, hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi; kwa hiyo amepeleka simba kati yao, na tazama, wanawaua, kwa sababu hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi. Ndipo mfalme wa Ashuru akatoa amri, akasema, Mpelekeni mmojawapo wa makuhani, mliowachukua kutoka huko; aende akakae huko, akawafundishe kawaida ya Mungu wa nchi. Basi mmoja wa makuhani waliochukuliwa kutoka Samaria akaenda akakaa katika Betheli, akawafundisha jinsi ilivyowapasa kumcha BWANA. Lakini pamoja na hayo watu wa kila taifa wakajifanyia miungu yao wenyewe, wakaiweka katika nyumba za mahali pa juu, walipopafanya Wasamaria, kila taifa katika miji yao walimokaa.”_
Habari za wana wa Isaraeli kuhamishwa na Mfalme wa Ashuru kuondolewa kutoka Samaria na yule mfalme akaleta watu wengine kutoka maeneo mbalimbali wakakaa Samaria na hawakuuliza MUNGU wa nchi au MUNGU wa Wayahudi alikuwa anaishije na alikuwa amewatengenezea mfumo upi wa maisha, Biblia inasema ghafla wakaanza kuraruliwa na simba, ndipo wakajua ya kwamba kuna kitu tumekorofisha hapa hatujajua MUNGU wa nchi anavyotaka mambo yaende ikabidi watafutwe makuhani waje kuwafundisha ili wajue kitu cha kufanya.
Kwa hiyo unaweza ukaenda kwenye eneo na hilo eneo likiwa na adhabu siyo simba lakini ni ugonjwa ukikaa pale utakutana na huo ugonjwa na inategemea adhabu imeenda kwa nani kama imeenda kwa wamama inamaanisha wamama wanaokaa pale ndiyo watapata shida na kama imeenda kwa wababa au watoto basi nao itatokea vivyo hivyo.
Ngoja nikuonyeshe jambo jingine ambalo sikukuonyesha Jana.
*2 Wafalme 5:26-27*
_Akamwambia, Je! Moyo wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? Je! Huu ndio wakati wa kupokea fedha, na kupokea mavazi, na mashamba ya mizeituni, na mizabibu, na kondoo, na ng'ombe, na watumwa, na wajakazi? Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele. Naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama theluji._
Usicheze na sadaka Naamani ameenda kutafuta msaada wa kuombewa, msichana ambaye walifanikiwa kumteka mateka akafanikiwa kutoa taarifa anasema naona Naamani anaukoma akasema lakini laiti angekutana na nabii yuko kule Israel angemponya, taarifa akapelekewa mfalme na mfalme akaandika waraka kwa mfalme wa Israeli nimemtuma Naaman umponye, Mfalme akararua mavazi yake akasema huyu anatafuta tu kisingizio mimi nitamponyaje mtu ukoma. Elisha akapata taarifa akasema mwambieni Naaman aje nabii yupo katika Israeli Naamani akaja amejipanga vizuri na sadaka yake na kila kitu akafika nyumbani kwa Elisha akagonga mlango Elisha hakutoka nje hata kumsalimia akamwambia nenda kajichovye mto Yordani mara saba utatakasika Biblia inasema Naamani alikasirika sana kwamba huyu ndugu nilitegemea atatoka nje hata anibandike mikono nipone alikuwa anatokea Syria ya sasa, kule kwetu tuna mito mizuri kuliko Yordani kama ni mambo ya maji hata kule ningeoga, wafanyakazi wake aliokuja nao ndio waliomtuliza kuna shida gani wewe nenda tu kajichovye akaenda akajichovya akapona alipopona akarudi tena kwa Elisha kutoa sadaka ya shukrani Elisha akakataa.
Gehazi ambaye alikuwa mfanyakazi wa Elisha akaona  Naamani anarudi na burungutu la sadaka akatafuta mbinu ya kumfuata kimya kimya akamkimbilia na Naamani alipoona akateremka akasimamisha gari yake akasema je ni amani! Ndio akasema wana wa manabii wanataka hii sadaka, halafu akasema sadaka kidogo sana Naamani akampa nyingi na  watu wa kumsindikiza walipokaribia mahali walipokuwa anataka kuificha akawaambia mnaweza mkaenda akaenda akaficha! Akaenda kwa Elisha akaulizwa ulikuwa wapi akadanganya nilikuwa hapa hapa! ndipo unauona huu mstari wa 26 akamwambia moyo wangu ulienda pamoja na wewe na nikaona kitu ulichofanya. Kwa lugha nyingine anasema si ungeniuliza kwanini wewe umeikataa hii sadaka ?
Kwa sababu sadaka zinauwezo wa kubeba kitu cha kiroho, zinabeba moyo wa mtu na zinabeba aina ya roho, hii ya Naamani ilibeba ukoma Elisha kaikataa Gehazi akaamua kuichukua, sasa akaambiwa kwa sababu umeipokea akaambiwa umekuwa na ukoma sasa shida inakuja ni pamoja na watoto wake milele kwa hiyo ni pamoja na wale ambao hawajazaliwa, hutaona kwenye Biblia ikizungumzia wajukuu Bibi au Babu, Yakobo ni mtoto wa Ibrahimu, Yesu ni mtoto wa Ibrahim haisemi ni mjukuu! Na mjukuu! Mpaka leo ukiwauliza Waisraeli Ibrahimu ni nani watasema baba yetu
Nilitaka uone hapa hawa watoto kitu gani kilichotokea si tu kwamba uso wa Gehazi ulipata uko na mbegu yake ilipata ukoma kwa hiyo watoto wanaozaliwa kutokea kwake Wote wanazaliwa na mazingira ambayo wanaweza kupata ukoma na shida ni sadaka.  Jana nilikusomea
*Ezekiel 21:21-23*
Unamkuta yule mfalme wa Babeli yuko kwenye njia panda akifanya mambo ya uganga na alipokuwa anafanya mambo ya uganga Biblia inasema akatikisa terafi.angalia ule matari wa 21.
_Maana mfalme wa Babeli alisimama penye njia panda, penye kichwa cha njia hizo mbili, ili atumie uganga; aliitikisa mishale huku na huko, akaziuliza terafi, akayatazama maini._
Terafi ni sawa sawa na kibuyu kwamba anatikisa kibuyu anauliza maswali lakini jibu analipata kwenye maini, Biblia haituambii ni maini ya kitu gani lakini ni sadaka aliyokwenda nayo. Fikiria huyu mfalme ni baba yako au bibi yako au mama yako kaenda mahali kabeba sadaka ya maini, anapobeba sadaka ya maini na yanawezekana katika sheria alizopewa yanatakiwa maini ya kwao lakini badala ya kutoa maini ya kwao sheria ya ile sadaka inasema unaweza kuleta maini ya kitu fulani kwa hiyo unaleta sadaka ya maini ya mbuzi kama sheria inavyodai, au sadaka ya maini ya kuku kama sheria inavyodai usije ukafikiri unapeleka tu maini ya kuku bali ni maini ya kuku kwa niaba ya maini ya kwako!
Biblia inasema Mungu alisema wazaliwa wakwanza wote ni wangu sio wenu na kutoka na sheria aliyoiweka juu ya wazaliwa wa kwanza wote wa wanadamu na wa wanyama wote lazima wauawe na wanatolewa sadaka, kwa jinsi ya kiroho maana yake wanapoteza nafasi alikuwa nayo kwa jinsi ya kibinadamu Mungu anawapa majukumu mengine katikati ya wanadamu wale ambao hataki kuwapa majukumu kama punda alikuwa anawamaliza kabisa lakini hawa wengine anawapa majukumu mengine kwa jinsi ya kiroho kwa hiyo mzaliwa wa kwanza wanadamu wa kiyahudi  alikuwa anakabidhiwa kwa Mungu sasa Mungu akasema badala yake nataka walawi, walawi walipokuwa wachache akasema nataka sadaka ya ukombozi ya mzaliwa wa kwanza.
Kwa hiyo ile sadaka ya mzaliwa wa kwanza ilikuwa inabeba roho ya mzaliwa wa kwanza 
Nilienda mahali fulani mkoa moja nikapewa taarifa juu ya shamba ambalo lilikuwa la Mzungu na likaenda kwa Mwafrika, yule mwafrika akawa anashangaa kwenye eneo moja kwenye lile shamba kila mwaka ng’ombe alikuwa anakufa katika mazingira ambayo hawaelewi, wanaenda machungunani jioni wanakuta ng’ombe anakufa eneo lile lile kila mwaka iliwachukua muda kidogo kila mwaka wanaona ng’ombe wanakufa, ndipo wakaanza kuuliza ndipo wakaambiwa na wale waliokuwa wanafanya kazi na mzungu mwanzoni wakamwambia! Huyu mzungu alikuwa anatoa kafara ya ng’ombe kila mwaka hilo eneo lilikuwa na kisima cha maji alikuwa anatoa kafara kila mwaka, alipopewa mtu mwingine yule aliyeondoka hakumpa sheria za mungu wa lile eneo yale mapepo yaliyokuwa yanapokea sadaka yakaanza kudai ng’ombe yenyewe, kwa hiyo yakawa yanachukua kisima kikakauka yule mtu akatafuta namna nyingine ya kupata maji kwa njia nyingine akawa anapata lakini pale pakawa bado pale palikuwa panapoteza ng’ombe.
Usipofahamu kitu gani kinatokea kwa misingi hiyo si rahisi sana ukajua namna ya kumwombea mtu wa namna hiyo, unaweza ukaomba maombi ya jumla na ukarudi mwaka ujao ukakuta shida imerudi au ikapotea mwaka moja au miwili ikarudi.
Nilikuwa nafundisha mahali fulani kitu kama hiki mtu moja akaniandikia akasema sasa ninaelewa kwanini kwetu  tunasumbuliwa na vifua, anasema ugonjwa wa kifua unatusumbua karibu kila mtu anaugua kipindi fulani cha maisha akasema wazee wa wazee wao huko walikokuwa, walikuwa wanatoa sadaka ya vidari kama ni kuku kidari kama ni mbuzi kidari, kidari cha ng’ombe, sasa wameacha shetani anadai vidari vyao. Cheki vizuri kama unaumwa cheki  kitu gani kinakusumbua kama ni ugonjwa wa kuambukizwa, kama ni shida ya sukari ni bandama, huko kuna historia ya namna gani!
Sasa sikuelezi kwamba kila kwenye shida ya sukari walikuwa  wanatoa sadaka ya bandama mahali, mimi najaribu kukufikirisha, kama mnapata shida ya figo cheki kisayansi figo zina matatizo yake na vyanzo vyake lakini kama mnatoa sadaka mahali kutakuwa shida za figo ambazo kwa taratibu za kawaida za kihospitali hata zikitafutiwa msaada hazitapata msaada unaotakiwa.  Cheki wale ambao kitovu chao kilikuwa kinatolewa sadaka mahali wengi wao wanashida na magonjwa ya tumbo la uzazi na unakuta ni kitu cha kurithi ndio maana nimekueleza hili jambo la pili, Hakikisha unafuatilia saa ingine Mungu anaweza kukusemesha kwa ndoto kama unajua kutafsiri utajua kwamba Mungu anajaribu kukujibu swali nililomuuliza hiki chanzo chake kinatokea wapi.
HATUA YA TATU
*OMBA TOBA KWA AJILI YA UOVU WA WALIOKUTANGULIA KUUPATA HUO UGONJWA NA OMBA TOBA KWA AJILI YA DHAMBI ZAKO*
*Daniel. 9:1‭-‬3,16
_Katika mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya Wakaldayo; katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la BWANA lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini. Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu_
_16.Ee Bwana sawasawa na haki yako yote, nakusihi, hasira yako na ghadhabu yako zigeuzwe na kuuacha mji wako Yerusalemu, mlima wako mtakatifu; maana kwa sababu ya dhambi zetu, na maovu ya baba zetu, Yerusalemu na watu wako wamepata kulaumiwa na watu wote wanaotuzunguka_
Nilitaka uone kaomba toba kwa ajili ya uovu wa baba zao waliowatangulia, ni vizuri tufuatane hapa vizuri maana katika kutoka 20:5 anazungumza juu ya kupatiliza uovu wa baba zao sio wa dhambi za baba zao.
*Maombolezo. 5:7*
_Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao._
Kwa hiyo anaposema napatiliza uovu hasemi dhambi, kwa wanaofuatilia kwenye Biblia utagundua biblia imegawa dhambi na uovu, na kila mtu na dhambi yake. Kama  umeona baba yako amefanya hiyo dhambi na wewe ukaikataa baba yako ndio atakaebeba, lakini wewe ukiona na ukaamua kufanya utaamua kupewa adhabu kwa sababu na wewe umefanya. Inapofika kwenye uovu anahamisha kutoka kwa huyu aliefanya dhambi inamaanisha kuna kitu kinatengenezwa baada ya mtu kufanya dhambi,ukisoma kwenye biblia utaelewa utakuta mahali pengine wametumia neno “weakness” na “infirmity” , au “inequity” kama unasoma biblia na unaelewa kiingereza katafute utaona,vlakini kwenye tafsiri zetu za kiswahili utakuta maneno mawili makubwa “UOVU” “UDHAIFU”.
Unapofanya dhambi yaani uasi 1Yoh 3;4, Uasi ni kwenda kinyume cha.., sasa Mungu alipokuwa anamuumba mwanadamu na kumuweka katika ulimwengu huu alitengeneza sheria, tunapokwenda kinyume na sheria  tunavunja sheria, alijiwekea katika moyo wake na mshahara wake ni mauti, lakini unapoganya dhambi pia inafanya uharibifu ndani yako na inaondoa uwepo wa Mungu kwenye lile eneo.
Ukitumia gari inayotumia petrol ujue injini yake imetengenezwa kutumia petrol tu, sasa unapoenda petrol station (sheli) wale wanaokuwekea mafuta wasitazame vizuri labda na wewe usiulize wakaweka diesel, usije fikiri kuwa gari halitatembea, litatembea mwanzoni injini itakunywa diesel na baadae itagundua kuwa hiki sio kinywaji tulichoumbiwa ghafla utaona mlio umebadilika, na harufu itabadilika utaanza kusikia mlio wa diesel sio tena wa petrol na unaenda kwa fundi, hebu nitazamie shida ni nini? Fundi atakwambia umeweka diesel badala ya petrol kwa hiyo itabidi tutoe tank tusafishe na baadae tuangalie uharubifu wowote kwenye injini wataangalia kila kitu na kucheki shida yote. Sasa mwingine atatoa tu tank na kusafisha alafu anaweka petrol akifikiri zile mashine kule ndani zitafanya kazi kama mwanzo, haziwezi *zinapata kitu kinaitwa udhaifu* hata kama ukiweka petrol haiwezi kurudi kwenye hali yake ya kawaida mpaka ubadilishe vitu huko ndani.
Dhambi ikiingia ndani ya mtu ni uasi na kuna adhabu ya uasi, lakini pia inaharibu vitu ndani kunatokea kitu kinaitwa Udhaifu, Roho wa Mungu anapokataliwa kule ndani kuna vitu sasa huwezi kufanya kwa sababu sasa kuna udhaifu, lakini pia dhambi inapoanza kuharibu utendaji wa vitu ndani yako. Sasa maandiko yanasema Mungu anapatiliza uovu, sasa hapatilizi ile dhambi ya kuvuta sigara bali unazaliwa na udhaifu kwenye mapafu yako na unazaliwa na udhaifu kwenye nafsi yako, sio rahisi kushindana na moshi ukiusikia baada ya muda nguvu yako ya kupambana na uvutaji wa sigara ambayo anayo mtoto mwingine kwa sababu umezaliwa na udhaifu huo.
Ndio maana unakuta kama kuna ugonjwa wa kuambukiza au wa kurithi kuna kiungo kimoja ambacho ndio kinapata shida kubwa kuliko vingine. Ukienda hospitali alafu wakakukuta una tatizo la sukari watakuuliza “je kwenye familia yenu kuna mtu mwenye tatizo la sukari?” ili wajue namna ya kukutibu, maana kuna tofauti sana ya mtu anaepambana na sukari ya kwake yeye mwenyewe na ya kurithi, kwa sababu sukari ya kurithi unazaliwa na weakness au udhaifu kwenye viungo vyako, ni tofauti sana na yule ambae kwao hawana hiyo historia,bukimwambia daktari namna hiyo atajua nini shida.
Nataka uelewe kitu gani kiliandikwa kwenye kitabu cha
*Mathayo 8:16‭-‬17*
_Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi, ili litimie lile neno *lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.*_
Sasa watu wengi sana ule udhaifu na magonjwa vinafanana, biblia inataka tujue ya kwamba pia alikuwa anashugulika na kitu cha kurithi,wamezaliwa na madhaifu yanayowafanya wapate magonjwa ya aina fulani..
*USHUHUDA*
Nilikuwa nasikiliza ushuhuda wa mtu mmoja kule Australia alipogundulika ana ugonjwa
Fulani kwenye damu unaotokea kwenye mifupa na haukuwa na dawa wakamwambia atakufa sio muda, baada ya muda hali yake ikawa mbaya akaanza kumuomba Mungu amsaidie sasa hawakutaka afie kule wakamrudisha kwao Marekani, alipofika marekani akashangaa tu anaona hali yake inakuwa nzuri kwa hiyo akaenda kwa Daktari wa familia akamueleza na kila kitu akampa na file la vipimo alivyochukua kule Australia, sio tu kwamba walimkuta amepona walimkuta mpaka Damu imebadilishwa mpaka group lake, Mungu alibadilisha.
Kwa hiyo si tu kwamba Mungu alimponya bali alibadilisha na ini akaweka na vifaa na kila kitu kipya. Sasa kama inakubidi Mungu akubadilishie Engine acha abadilishe lakini utembee.
Kama unasumbuliwa na tatizo la kurithi maana tatizo ni zaidi ya ugonjwa, kuna kitu cha zaidi unachosumbuka nacho kwenye mwili, na usipojua kitu cha kufanya itakusumbuza zaidi.
*Waebrania 9 : 16-17*
_Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya. Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya._
Haya ni masuala ya kisheria, agano ni sheria mama ina maana kuna patano. Mahali ambapo limefanyika agano la urithi, wanaingizwa na wengine ambao hawahusiki. Ina maana ni wewe unaingia agano na uzao wako, ni wewe unaingia agano na kampuni yako, ni wewe unaingia agano na kanisa lako, ni wewe unaingia agani na kabila lako. Ukishaingia agano la namna hiyo ambalo linahusisha na watu ambao hawapo na watakuja kuzaliwa baadae  linaitwa agano la kurithi.  Kwa sheria ya ulimwengu wa roho linanguvu inapotokea kufa kwa mtu aliyetangulia au aliyefanya agano hilo. Kama huyo yuko hai yule aliyefanya agano hilo, biblia inasema  halina nguvu inayotakiwa.
Kwa hiyo mauti, inasukuma kitu cha kurithi kwenda kwa mtu mwingine. Kwa hiyo utaona watu wengi sana wanapata magonjwa ya kurithi kwa nguvu  wale  waliotanguliwa wanapokufa. Wakiwa hai inakuwepo ila inakuwa haina nguvu sana saa nyingine  hakuna. Lakini  wakifa tu, iwe ni tabia ya kurithi au ugonjwa wa kurithi au utumishi wa kurithi kuna kitu kinaamka.
Wangapi huwa mnamtazama *Joel Osteen*, Baba yake wakati anakufa, Joel Osteen alikuwa mpiga Kamera, Dada yake ndio alikuwa anahubiri wakati baba yake yuko hai. Yeye alikuwa na aibu na ndio alikuwa anashughulika  na Kamera. Baba yake alipokufa na baada ya kumaliza mazishi, baraza la wazee ndio likasema tunakuteua wewe kuwa mchungaji.  Hajawahi kuhubiri, maana alitegemea kuwa dada yake ndio atapewa. Mauti ya baba yake iliachilia kitu cha kurithi kilicho bora. Ghafla yule mtu ambaye walikuwa wanaona haongei wanakuta anaongea.
Kasome habari za Isaka, biblia inazungumza  Isaka kuwa mrithi wa Ibrahimu.  Mungu alimkataa Eliazeri, alikamkataa Ishmael, aliwakataa wana watano wa Ketura (Mke wa Ibrahimu baada ya Sara kufariki). Urithi alipewa Isaka. Alipewa kabla Ibrahimu hajafa, . Kasome biblia yako inasema baada ya kumaliza mazishi ya Ibrahimu bibilia inasema Mungu akambariki Isaka.  Baada ya baba yake kufa.
Mauti inaachilia kusukuma kitu cha Urithi. Kama ni sheria katika ulimwengu wa roho imepewa nguvu ya kusukuma kitu, kizuri itasukuma, na kama ni kibaya itasukuma kitu kibaya.
Haijalishi alikufa lini, kinaweza kwenda kizazi cha tatu na cha nne. Damu ya Yesu  inaweza kushughulika. Maana ni jambo la kisheria kwa hiyo unahitaji kuwa na maandiko ya kutosha Ili kuongeza imani yako.
*Ufunuo 13:8*
_Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha *Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia*._
Misingi ya dunia iliwekwa lini, wakati Mungu alipokuwa anaumba mbingu na nchi, na ndivyo kitabu cha Ayubu kinatumbia. Mungu alikuwa anamuuliza Ayubu kuwa alikuwa wapi wakati Mungu anaweka misingi na bahari na malango ya maji. Ndio maana wasomaji wa biblia wanaamini Kitabu cha Ayubu  ndio kilikuwa kitabu cha kwanza kuandikwa.
Wote tunaosoma biblia tunajua kuwa Yesu alichinjwa msalabani lakini maandiko yanatuambia kuwa alichinjwa tangu kuweka kwa misingi ya ulimwengu. Ili tujue kuwa Yesu alichinjwa  msalabani na damu yake ilimwagika msalabani lakini nguvu ya damu yake inaenda huku nyuma mpaka wakati msingi wa dunia ukiwekwa. Huku mbele unaenda  mpaka milele.
Lengo ni ili mtu anayetaka msaada wa Mungu aweze kupata katika Damu ya Yesu. Haijalishi huku nyuma ni miaka mingapi na mlango uliofunguliwa Damu ya Yesu inaweza ikaja na ikashughulika.
Nilikuwa mahali fulani nilifundisha somo hili kutoka kona nyingine, nikasema kila mtu anyunyize damu ya Yesu kwa mtu aliyekufa, nilisema kwenye mauti yake. Kama kuna shida hapo tutajua. Kuna mtu mmoja alikuwa ananisikiliza kwa njia ya Redio.  Anasema alinyunyiza Damu ya Yesu kwenye mauti ya mama yake aliyekuwa amekufa miaka mitano iliyopita. Anasema alipoachilia hiyo Damu kuna kitu kilikamata tumbo lake,  anasema alifikiri litapasuka maana alipata maumivu makali sana. Ina maana kuna kitu kiliachiliwa kwenye ile mauti.
Kazi  ya mwalimu ni kukupekea jikoni namna  ya kuandaa mchuzi,  lakini mwinjilisti ni kukupeleka  restaurant kula. Anasema huyu ni kuku amini, kama unataka kula, mwamini mwinjilisti  unakula kuku na utapata uzima wa milele. Mwalimu anakupeleka jikoni, akuonenyeshe kuwa kuku hajafa kibudu na kachinjwa vizuri kabisa.
Lengo ni ili kesho na kesho kutwa uwe na mistari ya kusimamia na uweze kumsaidia na mtu mwingine. Kwa sababu saa nyingine hujui kosa walilofanya, na wamekufa na wewe umebaki peke yako, na huna cha baba au mama na huna mtu utakaye muuliza  na hayupo na huna mtu wa kumuuliza, lakini unasumbuliwa na unaambiwa huu ni ugonjwa wa kurithi. Sasa hapo ndio unahitaji damu ya Yesu kuingia kazini. Unasema inaingiaje kazini, waulize wana wa Israel,   lakini Mungu aliwaambia wapake damu kwenye miimo ya malango.  Hawakuomba kitu chochote bali aliwaambia wapake damu tu. Kwanini, hawakujua kitu cha kuomba maana wamekaa miaka mia nne labda wasimuliwe. Walienda pale Misri kimakosa kwa sababu walikorofishana na Yusufu na hilo ndio lilikuwa kosa kubwa sana.  Njaa ilipokua waliuza baraka yao, na walikuwa hawana mtu wakuwasaidia ilibidi wafuate mahali baraka zao zilipo.
Walipata msaada wakati yupo hai, alipo kufa alikuja Farao asiye mjua Yusufu. Na mateso yakaanza,  baada ya miaka mia nne kule ndani walikufa wengi sana. Sasa baada ya hapo unakuja kuwaambia kuwa nataka niwatoe niwapeleke Israeli wanasema ngoja kidogo,  unatuplekea wapi? Unasema nawapeleka Kaanani wanasema ngoja hapa ndio kwetu maana huko Kaanani ndio wapi?  Maana baba alituambia babu na bibi walizaliwa hapa sasa unataka kutupeleka Kaanani ndio wapi?. Hii historia umeipata wapi?
Wewe unajua kwanini  wazazi wako wamejenga hapo walipojenga? Wasipokueleza unaweza usijue,   leo nataka twende mbele za Mungu kwa toba, maana toba inaweza fanya kitu kikubwa sana maana toba inaweza kukutoa mahali kama toba tu. Maana biblia inasema palipo na toba pana ukombozi. Kuna watu hapa watavuka na watapokea muujiza wao
Kwa hiyo utakuwa unaangalia hilo tatizo liko namna gani,  hapo biblia inasema uovu, unatubu tu, kwa hiyo unatakiwa kuelewa  maana kuna aina ya vyakula hutakiwi kula kama unataka kutunza afya. Kama unafikiri natania endelea kula alafu siku moja tutakukuta hospitali. Daktari atakupa dawa na masharti yenyewe maana umekula unafikiri umekula chakula kizuri kumbe ndio  unaharibu mwili.
Mzee mmoja alikuwa anakula kila kitu kilichowekwa mezani, akaugua, akaenda hospitali ma alipewa masharti ya chakula mengi kuliko dawa.  Sasa alikuwa akienda mahali, alikuwa nawaambia watu kuleni kwa uangalifu chakula kinaua.
Inawezekana wazazi wako kuna kitu walifanya na hawana meno kwa sasa, . Sasa hii isiwe sababu ya wewe kutopiga mswaki maana hapo  utakuwa umefanya kosa la udhaifu uliokuwa nao jumlisha na uovu wa wazazi wako.  Sasa kutopiga mswaki ni dhambi na unatakuwa kuelewa hapa. 
SIKILIZA MAOMBI YOUTUBE KWA LINK PALE JUU….
[22:03, 14/05/2018] Filix Bwanji: *7⃣SEMINA YA NENO LA MUNGU-DODOMA UWANJA WA BARAFU*
*MWL.CHRISTOPHER MWAKASEGE*
*SOMO: UWEZO WA MUNGU JUU YA MAGONJWA NA VYANZO VYAKE.*
*TAREHE  12 MAY, 2018*
*SIKU YA SABA*

*LINK YA SEMINA YA LEO YOUTUBE* 👉https://youtu.be/wqUAEyoLhH4
*NAMBA ZA SADAKA* 👉https://goo.gl/Z3ozYB
*NAMNA YA KUPATA CD&DVD BONYEZA HAPA*👉 https://goo.gl/tgwoub
Leo ikiwa ni siku yetu ya saba muda uliopita nimekueleza jinsi Mungu anavyotamani uwezo wake unapokuwa mahali watu wajue kwamba upo na upo kwa ajili ya kuponya.
Na nilikuambia ukienda kwenye maandiko utaona Yesu anavyoponya magonjwa na yeye anashughulikia chanzo cha ugonjwa kabla ya kuponya ugonjwa wenyewe kwa kukemea pepo na ugonjwa unaondoka wenyewe. Na vyanzo vingine tuliviangalia
Uwezo wa Mungu unapoenda mahali kwa ajili ya kumshughulikia mgonjwa unaanzia kwenye chanzo ndio unakuja kwenye ugonjwa wenyewe. Usiposhughulikia chanzo, ugonjwa utarudi ni sawa na kukata matawi lakini mizizi bado iko pale kwa sababu ikipata mazingira mazuri unachipuka kwa sababu utajua mizizi ya chanzo chake havijashughulikiwa ni sawa na ugonjwa usiooondolewa chanzo chake.
Ukienda kidaktari ni hivyo hivyo, huwezi kukamua jipu ukaacha hivi hivi, watakuambia mpaka uondoe na nyumba yake kwa kuifuatilizia mpaka waitoe unaona sawasawa na jipu linanyauka na kupona kabisa. Lakini usipoondoa kiini chake uwe na uhakika kila baada ya muda hilo jipu litakusumbua.
Jinsi ilivyo kisayansi ni hivyo hivyo kiroho. Lazima ushughulikie chanzo kama ukiona mwenzako ofisini amekufa na ugonjwa akiwa kazini na wewe ukapewa hiyo kazi usiende tu kienyeji kienyeji. Kwa sababu mwingine si kwamba anapata ugonjwa kwa sababu ya shida aliyonayo lakini ni kwa sababu ya kitu kilichotokea kazini.
Kama unaolewa katika ndoa au unaoa ndoa ya pili au ya tatu angalia vizuri huyo mnayeoana alietangulia aliondokaje au mahali unakoolewa, huyo mke mwingine aliondokaje. Na mengine mengi tumeyaona kwa hiyo tafuta CD au Kanda upate hili somo kwa uzuri kabisa usikilize na kusikiliza.
Leo nataka nikufundishe tofauti kidogo na nataka nitaje hatua zinazofuata na tutakazopitia zote halafu Mungu ataniongoza za kuchukua ni zipi.
HATUA YA NNE
*4. ONDOA JINA LAKO KWENYE AGANO NA TANGUA AU BATILISHA  KIAPO KILICHOFANYA UWE MRITHI NA UKAUGUA*
*Isaya  28:18*
_“Na agano lenu mliloagana na mauti litabatilika, tena mapatano yenu mliyopatana na kuzimu hayatasimama; pigo lifurikalo litakapopita, ndipo ninyi mtakapokanyagwa nalo.”_
*Hesabu 30:2*
_“Mtu atakapomwekea BWANA nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa ahadi, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake.”_
*Ezekieli 21:21-23*
_“Maana mfalme wa Babeli alisimama penye njia panda, penye kichwa cha njia hizo mbili, ili atumie uganga; aliitikisa mishale huku na huko, akaziuliza terafi, akayatazama maini. Katika mkono wake wa kulia alikuwa na kura ya Yerusalemu, kuviweka vyombo vya kubomolea, kufumbua kinywa katika machinjo, kuiinua sauti kwa kupiga kelele sana, kuweka vyombo vya kubomolea juu ya malango, kufanya maboma, na kujenga ngome. Jambo hili litakuwa kwao kama uganga wa ubatili, mbele ya macho yao waliowaapia viapo lakini ataufanya uovu ukumbukwe, ili kwamba wakamatwe.”_
*Mathayo 26:28*
_“kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.”_
HATUA YA TANO
*5. NYUNYIZIA DAMU YA YESU  JUU YA ENEO AU KIUNGO KINACHOUMA AU JUU YA AINA YA UGONJWA WA KURITHI UNAOKUSUMBUA*
*Waraka kwa Waebrania 9:7‭, ‬19‭-‬22*
_“Lakini katika hema hiyo ya pili kuhani mkuu huingia peke yake, mara moja kila mwaka; wala si pasipo damu, atoayo kwa ajili ya nafsi yake na kwa dhambi walizozitenda hao watu bila kujua. Maana kila amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru sheria, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote, akisema, Hii ni damu ya agano mliloamriwa na Mungu. Na ile hema nayo na vyombo vyote vya ibada alivinyunyizia damu vivyo hivyo. Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.”_
*Ufunuo 13:8*
_“Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.”_
*Ufunuo 5:9‭-‬10*
_“Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuifungua mihuri yake; kwa kuwa ulichinjwa, ukawa fidia kwa Mungu na kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.”_
HATUA YA SITA
*6. NYUNYIZA DAMU YA YESU JUU YA MAUTI YA MTU MNAYEHUSIANA NAYE KUFUATANA NA UGONJWA ULIORITHI*
Kama ukiangalia vizuri pointi ile ya kwanza nilikuorodheshea hayo magonjwa yanaweza kupitia wapi
*Waebrania  9:16-17*
_“Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya. Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya.”_
*Waebrania 2:14-15*
_“Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa.”_
HATUA YA SABA
*7. KEMEA PEPO LA KURITHI LILILOBEBA UGONJWA HUO NA KUKAA NAO KWENYE KIUNGO AU KWENYE NAFASI AU KWENYE ENEO LINALOKUHUSU*
*Marko 16:17-20*
_“Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya. Kupaa kwa Yesu. Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu. Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.]”_
HATUA YA NANE
*8. OMBA UPONYAJI WA UDHAIFU NA WA UGONJWA JUU YAKO AU JUU YA YULE UNAYEMUOMBEA*
*Mathayo 8:16-17*
_“Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi, ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,”_
HATUA YA TISA
*9. KAA CHINI YA UVULI WA YESU ILI ULINDWE UGONJWA USIKURUDIE AU USIKUPATE KAMA BADO HUJAUGUA/HUJAPATA HIYO SHIDA YA KURITHI*
*Zaburi 91:1-16*
_“Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu. Atakaa katika uvuli wake  Mwenyezi. Nitasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini. Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo. Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao. Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana, Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri, Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe. Ila kwa macho yako utatazama, Na kuyaona malipo ya wasio haki. Kwa kuwa Wewe BWANA ndiwe kimbilio langu; Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako. Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako. Kwa kuwa atakuagizia malaika zake, Wakulinde katika njia zako zote. Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. Utawakanyaga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu. Kwa kuwa amekaza kunipenda. Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu. Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza; Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.”_
Kutoka 12:12-24
_“Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA. Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lolote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri. Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa BWANA; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele Mtakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba; siku hiyo ya kwanza mtaondoa chachu yote isiwe katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu ye yote atakayekula mkate uliochachwa tangu siku hiyo ya kwanza hata siku ya saba, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na Israeli. Siku ya kwanza kutakuwa kwenu na kusanyiko takatifu, na siku ya saba kutakuwa kusanyiko takatifu; haitafanywa kazi yo yote katika siku hizo, isipokuwa kwa hiyo ambayo kila mtu hana budi kula, hiyo tu ifanyike kwenu. Nanyi mtaitunza ile sikukuu ya mikate isiyochachwa; kwa kuwa katika siku iyo hiyo mimi nimeyatoa majeshi yenu katika nchi ya Misri; kwa hiyo mtaitunza siku hiyo katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele. Mwezi wa kwanza, siku ya mwezi kumi na nne, wakati wa jioni, mtakula mikate isiyochachwa, hata siku ya mwezi ishirini na moja jioni. Muda wa siku saba isionekane chachu katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu ye yote atakayekula hiyo iliyotiwa chachu, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na mkutano wa Israeli, akiwa mwenye kukaa hali ya ugeni, au akiwa mtu aliyezaliwa katika nchi. Msile kitu chochote kilichochachwa; mtakula mikate isiyochachwa katika makao yenu yote. Hapo ndipo Musa akawaita wazee wa Israeli, na kuwaambia, Nendeni, mkajitwalie wana-kondoo kama jamaa zenu zilivyo mkamchinje pasaka. Nanyi twaeni tawi la hisopu, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi. Kwa kuwa BWANA atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, BWANA atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi. Nanyi mtalitunza jambo hili kuwa ni amri kwako na kwa wanao milele.”_
HATUA YA KUMI
*10. FUATA MAELEKEZO YA NAMNA YA KUISHI KIROHO NA KIMWILI NA MAELEKEZO YA NAMNA YA KULA CHAKULA ILI UDUMU KATIKA AFYA*
*3 Yohana 1:2*
_“Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.”_
*Mithali 4:20-23*
_“Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu. Zisiondoke machoni pako; Uzihifadhi ndani ya moyo wako. Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote. Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.”_
HATUA YA KUMI NA MOJA
*11. FUATA MAELEKEZO YA ROHO MTAKATIFU YA ZIADA AMBAYO ANATAKA UYAFUATE ILI KUMALIZA TATIZO HILO LA UGONJWA WA KURITHI*
*Warumi 5:1*
_“Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,”_
*Marko 11:25*
_“Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.”_
NImekupa haya (kwenye mfululizo) kwa nakusudi kabisa ili iwe rahisi kufuatilia. Unaweza kuona kama ni hatua ndefu lakini kama jana ulinisikiliza nikiomba unaona haya yote ni mambo niliyaombea na labda hata hatukumaliza nusu saa kwa hatua zote hizi niliziombea na kuzitumia. Unaweza kuziweka zote hizi kwa pamoja lakini kwa mtu kutaka kuelewa unahitaji kuzipanga hatua kwa hatua.
Mfano ukinunua TV kuna mambo mawili waweza fanya. Moja uunganishe mwenyewe kwa kutumia kitabu cha mwongozo (Manual) au uite mtaalam kuja kukuunganishia, na akija mtaalam yeye mwongozo mzima upo ndani yake hana haja ya kusoma anakuunganishia kwa urahisi.
Hata inapofika masuala ya MUNGU ni hivyo hivyo tuna maelekezo ndani ya Biblia na Biblia inasema NENO la KRISTO na lijae kwa wingi katika moyo wako katika hekima yote. Kwa hiyo wakati mwingine unaona waombaji wanapoomba wanakuwa kama yule mtaalam wa kuunganisha TV wao ni kuponyeza tu botton unaona mambo yanaenda, kama ni wagonjwa wanapona, watu wanaokoka. Sasa na wewe unataka kujaribu wakati hauna NENO ndani unaomba na kufunga.
Kwanini nakueleze vitu vya namna hii/mambo haya? Maana wakati mwingine unafika nyumbani unaanza kujiuliza hivi Mwakasege aliombaje pale unajaribu kukumbuka hata kusema ngoja nitazame tena DVD kwa sababu unatafuta namna Mwakasege alivyoomba. Lakini sikuwa (Mwakasege) na mahali pa kutazamia kwanini? Kwa sababu ndani (Mwakasege) nimeweka NENO na wewe unahitaji kujizoeza kuweka NENO ndani, maana kesho na kesho kutwa hao wanaoitwa wataalam wa maombi wasipokuwepo je? Wakiwepo ni rahisi sana unaweza hata kuwapigia simu.
Na wewe unahitaji kuweka Neno ndani kesho hao wataalamu wa maombi wasipokuwepo wakiwepo haa ni rahisi sana utapiga tu simu, mchungaji upo na shida sana hapa nyumbani unaweza ukaniombea anakuja na Biblia yake anakusomea mstari anakupa maelekezo mnaomba jambo linaisha na ni dakika chake tu anaondoka keshokutwa unampigia simu mchugaji kuna shida nyingine anakuambia Niko safari unampigia mwingine anasema hii sijui lakini Siku ile anafungua Biblia na kukuelekeza alitaka ujue namna ya kuomba kwa sababu angeweza kufika hapo akaomba na kuondoka, kwa nini nakueleza kitu cha namna hiyo maswala ya magonjwa ya kurithi ni vitu ambavyo unahitaji kupata msaada ninapoenda mfano hospitali na kufanya checkup mara kwa mara kuangalia mwili wangu umekaaje dactari lazima tukae nae tuangalie yale majibu pamoja alieze hiki ni kiko hivi na hiki nataka kujua akiniambia hiki hakijakaa vizuri namwambia maana yake nini hakijakaa vizuri atanieleza na ataniambia dawa yake ni hii namwambia usiniambie dawa kwanza namuuliza chanzo chake ni nini? Ili nilijue kwa sababu kesho na keshokutwa nitarudi utanishindilia tena dawa kwa hiyo ninakaa pale wanaanza kunieleza moja baada ya nyingine unaweza ukapewa dawa ukapona lakini usipojua chanzo chake uwe na uhakika utapata shida baada ya muda ile shida inarudi
Ndio maana nimezimeng’enyua hizi hatua kwa namna ambayo unaweza ukafuatilia mwenyewe kwa sababu kila moja ina umuhimu wake inategemea swala la kwako limekaaje Roho Mtakatifu atakusaidia na kukuongoza ni eneo gani kwako ambalo unahitaji kulitilia mkazo ndio maana nimekuambia ile hatua ya nne ondoa jina lako kwa sababu kama ni kama ni kitu kinachohusiana na agano ambalo lilifanyika huko nyuma na ukaingizwa wewe maana huwa wanasema mimi na uzao wangu kwa hiyo kabla hijazaliwa uliingizwa huko kwa hiyo na adhabu itakuja hivo hivo kwa sababu kwenye maandishi katika ulimwengu wa Roho jina lako lipo kwa hiyo unapozaliwa tu unaigizwa kwenye agano na kuna maagano mengine yanaambatana na viapo kinaweza kuwa kiapo kilichofanyika pale na sio watu wengi wanaelewa kiapo kinafanya kitu gani! Kiapo kinafunga nafsi ndio kazi ya kiapo kufuatana na kile kitabu cha
*Hesabu 30:2*
_Mtu atakapomwekea BWANA nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa ahadi, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake._
Kwa hiyo kiapo kinafunga na kinafunga nafsi ya mtu kwa hiyo kama kulikuwa na agano ambalo limeenda na kiapo maana yake nafsi yako imefungwa lazima utangue ubatilishe
*Isaya 28:18*
_Na agano lenu mliloagana na mauti litabatilika, tena mapatano yenu mliyopatana na kuzimu hayatasimama; pigo lifurikalo litakapopita, ndipo ninyi mtakapokanyagwa nalo._
Nilitaka uone lile neno agano linaweza kubatilishwa na mapatano yasisimame sasa shida inakuja inawezeka hujui kwamba kulikuwa na agano Roho Mtakatifu saa nyingine anaweza akakuonyesha nikulelezea juzi watu wengi sana wanajulishwa kwa njia ya ndoto ila hawajui kwa sababu Mungu atakuonyesha picha ya maagano kibiblia ndio maana utakuta watu wanaota ndoto na watu waliokufa na wanakula chakula sasa si ndoto zote za kula zina maagano ndani yake lakini ndani yake kuna kitu Mungu anakionyesha kufuatana na maandiko kama una maandiko ya kutosha utajua Mungu anazungumza kitu gani ndio maana nikakupa na ile *Mathayo 26:28* ujue ndani ya Damu ya Yesu kuna ondoleo maana Biblia inasema damu iliyomwagika unaweza kuondoa dhambi kama ina uwezo wa kuondoa dhambi inauwezo wa kuondoa na madhara ya dhambi.
Makosa ambayo unakuta saa nyingine watu wanafanya anaamua kupambana na agano lenyewe kwanza kwa sababu saa nyingine Roho Mtakatifu hakuruhusu kupambana na agano lenyewe kwanza kwa sababu wewe hujui limefungwaje na inawezekana huna spana za kutosha kufungua kwa hiyo anagh’ang’ana nayo na unaweza ukachokoza vitu vikubwa kuliko uwezo wa kiroho ulionao Biblia inasema kama unataka kumfunga wenye nguvu lazima uwe na nguvu zaidi yake lasivyo atakugeuka na kukushughulikia kweli kweli sasa ili iwe rahisi kwako ni rahisi sana kuondoa jina unasema unaliondoaje! Unatamka kama unavyotamka *Mungu ninaondoa jina langu kwenye maagano yote ya kifamilia ambayo si sahihi mbele zako naliondoa jina langu na kuzifuta record zote zilizowekwa za kumbukumbu za kipepo nina batilisha kila kiapo kilichohusisha jina langu na kuliunganisha na hivyo vitu* ukisha sema namna hiyo Biblia inasema amini ulichosema Mungu amesikia na ndiyo itakavyokuwa ili kusudi kwamba utoke wewe kwanza tengeneza msuli wako kwa kiroho kabla hujarudi kuanza kupambana na kitu cha kiroho kilichoko kwenye familia yako wakati nguvu ni kidogo na ndio maana unakuta watu wengi sana wanapata shida la sivyo katika maombi ya namna hiyo hakikisha umeenda na wenzako ambao unauhakika wanaweza kukufunika kwa maombi na kukulinda hii si maombi ya kienyeji enyeji hii ni vita ya kiroho kwa hiyo ni hatua muhimu sana kwa jinsi ya kawaida unaweza kufikiri ni kitu tu kinapita lakini katika ulimwengu wa Roho ukiondoa umeondoa saa nyingine Roho Mtakatifu atakuambia rarua hizo kumbukumbu futa hizo kumbukumbu. Wengine kama mnakumbuka mwaka Jana tulikuwa hapa wakati tunaombea mambo ya ndoto za kuoa au kuolewa kwenye ndoto au kuzini kwenye ndoto akatokea dada moja amebebwa na wahudumu mapepo yamelipuka wanamleta Roho Mtakatifu akaniambia chana kumbukumbu katika ulimwengu wa Roho kwa damu ya Yesu zilizoweka kumbukumbu ya ndoa yake wakamsogeza nikasema ninachana kumbukumbu zake lile pepo likapiga kelele likasema usichane hizo kumbukumbu kwanini kwa sababu katika ulimwengu wa Roho kuna alama za kumbukumbu.
Na kikakupa hatua ya tano nikakuambia *Nyunyiza damu ya Yesu kwenye eneo* ukienda hospitali uanaoewa dawa zinalolenga kwenye eneo moja kwa moja wanaweka dawa hapo hapo wakupiga sidano hapo hapo unaenda hospitali unasema  ninatatizo  kisukari muulize dactari chanzo cha tatizo la kisukari ni nini muulize atakusimulia ndipo atakuambia kuna sukari type 1 sukari type 2 unamuuliza ndio maana yake nini , uku kwenye mwili wangu kuna nini mbona wewe una kula starch je kweye mwili wangu kuna tatitizo gani ni kiungo gani bacho kimeshindwa kufanya kazi sasa sawa , ukikaa vizuri na dactari kama ana muda atakueleza pole pole ndio maana kuna tofauti ya kutibiwa sukari kawaida na kwenda clinic ya sukari   ukienda kwenye clinic ya sukari ndipo watakueleza hivi vitu kwa hiyo wakikuambia bandama yako haifanyi kazi sawa sawa na wewe una note  kufuatana na tatizo lako figo zimeanza kupata shida una note pole pole au kutokana na tatizo lako macho yanapata shida una note pole pole ukirudi nyumbani nyunyiza damu ya Yesu kwenye badama, nyunyiza damu ya Yesu kwenye figo, nyunyiza damu ya Yesu kwenye macho, endelea kunyunyiza namna hiyo mpaka uone mabadiliko kwa sababu damu ya Yesu itaingia pale na itasema kitu kwa niamba yako na kwa ajili yako haijalishi hilo tatizo limetokea wapi, kile kitabu cha *Ufunuo 13:8 inasema huyu mwana wa adamu alichinjwa tangu kuwekwa kwa misingi ya dunia* kama alichinjwa tangu kuwekwa kwa misingi ya dunia wakati tunajua alichinjwa msalabani Biblia inataka tujue ya kuwa damu ya Yesu iliyokwagika pale msalabani ina nguvu ya kushughulikia matatizo yote tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu kwa hiyo haijalishi ni babu yako amekaa miaka mia mbili iliyopita ndio alikingiza hicho kitu damu ya Yesu ianuwezo wa kushughulikia haijalishi ni kaka zake na Yusuphu waliomuuza miaka mia nne damu ya pasaka itawatoa wayahudi kule misri.
*Waebrania 9:7*
_Lakini katika hema hiyo ya pili kuhani mkuu huingia peke yake, mara moja kila mwaka; wala si pasipo damu, atoayo kwa ajili ya nafsi yake na kwa dhambi walizozitenda hao watu bila kujua._
Nataka uone hilo neno dhambi za kutokujua za hao watu , unaposimama kwenye nafasi ya kikuhani ukiwa umeokoka kufuatana na  *ufunuo 5:9-10* umefanyika kuhani kwa Mungu na kama umefanyika kuhani kwa Mungu unaweza ukasimama kwenye nafasi na kufanya kazi ambazo kuhani mkuu alikuwa anafanya unajua maana ya kuhani mkuu ni kuhani aliye mkuu kwanza lazima awe kuhani , mfano katibu mkuu, kwanza lazima awe katibu halafu ndio mkuu, unaelewa maana ya mkurugenzi mkuu ni mkurugenzi aliye mkuu kwa hiyo lazima awe na cheo cha ukurugenzi ndio anakuja kuongoza wenzake kwa hiyo kuhani mkuu anafanya kazi zote zingine anazofanya kuhani lakini yeye ni mkuu kwa hiyo kuna kazi zingine ambazo makuhani wengine wanafanya sio kwamba hajui kuhani mkuu anapofanya kazi ulizotakiwa uzifanye hapa chini umetega kazi  ni sawa sawa na katibu mkuu kufanya kazi sehemu ambayo amemuweka katibu afanye kazi hajafanya kazi katega kwa hiyo anamlazimisha huyo afanye kazi.
Yesu amefanyika kuhani mkuu mfano wa Melekizedeki na biblia inasema sisi ni makuhani chini yake na ukuhani wetu ni bora kuliko ule wa Lawi,kwa sababu ule wa Lawi umepitia kwenye zile kabila za pale lakini ule wa Yesu umepitia kwa Melekizedeki na unapofanya kazi  kama kuhani chini ya damu iliyo bora zaidi ufanisi wako unatakiwa uwe mkubwa zaidi kuliko ule wa Haruni sio ya mafahali tena,walikuwa wanafanya kazi chini ya ahadi ambayo sio bora zaidi kama ya kwetu, na ukitanya kazi kama kuhani nafasi yako inatakaiwa iwe na ufanisi mkuu kuliko ule wa Haruni ,sasa maadniko yanasema Haruni alipewa majukumu na anapoenda kuomba anaachilia damu na ile damu itazungumza na Mungu hata na dhambi za kutokujua zawale watu ambazo ndugu zaowalifanya wakafungulia nafasi ya uovu damu ya Yesu itanena mema mbele za Bwana,ndio maana unatakiwa ujifunze kuiamini damu ya Yesu.
*Waebrania 9:18‭-‬22*
_Kwa hiyo hata lile la kwanza halikuanzwa pasipo damu. Maana kila amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru sheria, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote, akisema, Hii ni damu ya agano mliloamriwa na Mungu. Na ile hema nayo na vyombo vyote vya ibada alivinyunyizia damu vivyo hivyo. Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo._
Biblia inasema aliweka damu katika kila kitu sasa kwa wewe unasema damu ni kwa ajilinya kwenda mbinguni unahitaji kusoma biblia yako sawasawa, kutakasa maana yake kutenga kwa kusudi maalum, unapotakaswa kwa damu maana yake umetengwa na dhambi na unaitwa mtakatifu si kwa kitu ulichofanya bali kwa kile Yesu alichofanya mslaabani na kuiruhusu damu ya Yesu ifanye kazi ndani yako na kukutenga na dhambi na madhara yake.
Sasa kwanini ilimlazimu anyunyuzie damu kila kitu hata hema,watu, maana yake ni kwamba alikuwa anavitenga na kitu chochote katika ulimwengu wa Roho na ambacho kinaweza kisiwe kizuri mbele za Bwana kiwekwe rasmi kwa ajili ya kazi ya Bwana,unaponunua kifaa cha kuimbia gitaa au kinanda mchungaji lazima akiweke wakfu na kusafishwa kwa ajili ya kazi ya Bwana tu. Ukinyunyiza damu ya Yesu juu ya bandama inaenda kwenye kitu chochote ambacho hakiendi sawasawa damu ya Yesu inaingia inatenganisha.
Ndio maana nakwambia nyunyiza moja kwa moja kwenye kiungo utashangaa sana kitu kinachofanya,hata kama kwenye familia yenu kuna shida yoyote au ya moyo wewe nyunyiza damu ya Yesu kwenye huo moyo hata kama wewe haijakupata. Nyunyiza damu ya Yesu kama kinga tu.dio maana nimekuonyesha kwenye maandiko unapoomba uponyaji unaomba uponyaji wa udhaifu na magonjwa na Biblia inasema alichukua udhaifu wetu akachukua na magonjwa kwa sababu unapokaa kwenye magonjwa ya kuritji kiungo chakomkinazaliwa na udhaifu yaani weakness fulani ambayo inakuwa rahisii kwa wewe kushambuliwa na hio uginjwa ndio maana biblia inasema Yesu alichukua huo udhaifu ili wewe uwe huru na ugonjwa utarudi huko, ndio maana nikakwambianketi katika kivuli cha Yesu na tauni haitakaribia hemani mwako ndio maana nakwambianjifunze kukaa chini ya toba.
Wewe unafikiri ni kwanini wale watu ambao hawakuwa wayahudi waliamua kuondoka nao kwa sababau waligundua hawa jamaa wana Mungu ambaye sio wa kawaida na wakawafuata,sasa ulinzi wa Mungu juuu ya wayahudi ukawa na juu yao pia, Paulo alikuwa kwenye meli na haikuzama kwa sababu Mungu alikuwa pamoja nao.
*USHUHUDA*
Wakati Mungu alipokuwa ananiita kwenye utumishi miaka ya 80, na kilikuwabkinanisumbua sana hii ndio maana yake nini? Kwa hiyo alinisemesha kwa ndoto na kwa maono ya wazi wazi ahsante Yesu nilikuwa naandika vingi na vingine navikumbuka mpaka leo japo vingine vilikuwa vinaogopesha kwa jinsi ya kibinadamu lakini namshukuru Mungu amekuwa akinisemesha mpaka leo vingine vikinizidia namwambia viondoe anaviondoa na wakati huo sikuwa na pikipiki wala gari,kwa hiyo nilikuwa narudi nyumbani nateremka saa 9 alafu nikaanza kutembea kwenda kwangu, ghafla mvua ikaanza kunyesha kubwa inakuja na upepo mkubwa. Ilipokuwa inayesha namna hiyo watu wanakimbia kujificha,sasa nikawaza najigjcha wapi maana nyumba zilizokuwa jirani zilikuwa bar na wapendwa wangeniona wangesema “mpendwa amepoa anajifanya anajificha lakini amepoa”,kwa hiyo nikajikaza nikaendelea na safari Kitu kilichonishangaza gahfla upinde wa mvua ukanizunguka na nilipokuwa nasogea na wenyewe unasogea na nikagundua nilikuwa silowani,nikapita chini ya mti nikakuta kuna mama na binti yake,nilipopita na ule upinde wa mvua ukaenda mpaka pale kwenye mti ule upinde wa mvua ukaenda mpaka na kwao yule mtoto akamuuliza mama yake “vipi mvua imeisha?” Nilipopita na ule upinde wa mvua ukawaacha wakaanza kunyeshewa na wao, usije ukafikiri kilikiuwa kitu chepesi. Wakai natembea namna hiyo ikaja gari ya mtu  Land Rover aliponioma akasimamisha gari, akaniambia twende, nikapanda, alinitazama akasema mbona hujaloa.  Nikamwambia kuwa tazama bonet ya gari lako,  wiper hapo mbele  kulikuwa hamna mvua. Akiangalia pembeni anaona mvua lakini mbele ya gari hamna mvua na kuna upinde wa mvua. Akanitazama usoni hakusema tena tukawa tunaenda kimya kimya. Sasa akinifikisha mahali natkiwa kushukua na akanipungia mkono  na mimi nikampungia mkono.
Sasa watu wengine watajua kuwa huyu ndugu kaloga, ila Mungu alikuwa ananisemesha, kuwa mimi ni Mungu wa agano,  wewe hukuzaliwa hivi hivi wewe ni wa agano langu. Na hakuna agano linaloanza pasipo damu maana damu ya Yesu ikiwa pale inakufunika, na itamsaidia na mwingine. Ukiitumia wewe itamsaidia na mwingine inategemea unatumia kwa namna gani . Watoto wako kabla hawajaoata shida nyunyiza daamu ya Yesu iliyoamriwa juu yao ili magonjwa ya kurithi ambayo yanasumbua kizazi chako yasiende kwao.Endelea kunyunyiza Damu ya Yesu kama unavyowapa uji kila siku.
Saa nyingine utajua Roho Mtakatifu atakukamatia kuomba kwa muda mrefu na ndio maana katika kile kipengele cha mwisho nimekuambia msikilize Roho Mtakatifu akupe maelekezo ya ziada. Kwa maana yanaweza kuwepo, maana biblia inasema ukiisha kuhesabiwa haki kwa imani basi tuwe na amani kwa Mungu. Maana yake ni kuwa palipo na imani pana amani na palipo na amani pana imani. Tunakwenda sawa sawa?
Kibiblia  amani ni pana, amani ni mafanikio,  amani uliyonayo ikishikikia na kupata kitu ambacho unaomba kwa Mungu, amani ikija ina maana kuwa kile ulicho kuwa unaomba kinakuja, hata kama kwa nje bado kwa hiyo unaanza kumshukuru Mungu. Sasa kama unaona ule mzigo hauja ondoka maana yake Roho Mtakatifu anakuambia kuwa  endelea kuomba. Tunakwenda pamoja?
Kwa sababu inategema maelekezo unayopewa. Mfalme Hezekia aliambiwa kuwa tengeneza mambo ya nyumbani kwako maana ugonjwa huu utakufa, biblia akageukia upande akilia na Mungu  akasikia msukumo wa kupeleka hoja zake kwa Mungu. Saa nyingine Mungu anakupa  nafasi ya kuweka hoja,  usije ukafikiri wewe hawezi kukusikiliza.
*USHUHUDA*
Sitakuja sahau, siku Mungu amenifundisha kumwandika barua, ndugu mmoja alipata ajali tena ajali mbaya, mbavu zake zilipasuka na zikapasua mapafu yake na hewa  ikaanza kutokea ndani na kiuno kikavunjia, maana kuna mfupa ulivunjika kwa hiyo alikuwa haruhusiwi kutembea alikuwa analala tu. Walipo mpeleka hospitali hawakuona haraka maana mbavu zilivyovunjika zilitoa pafu na hewa ikawa inapita kutokea ndani kwa hiyo tumbo likaanza kuongezeka.  Sasa Daktari wa zamu akapita na yule ndugu aliyepata ajali  akamuuliza  Daktari, “ Mzee hili tumbo kuna shida gani?, Yule Daktari akasema aaah bwana mdogo hicho ni kitambi tu.  Sasa yeye alikuwa nako kadogo yu ndio kanaanza,  sasa hakikuwa namna hiyo.  Sasa akaja rafiki yake ambaye ni daktari akamwambia afadhali umekuja naomba angalia tumbo langu. 
Maana Daktari wa zamu kapita hapa nimemuuliza kuwa acheki tumbo langu ila yeye kaniambia kuwa hicho ni kitambi,  wewe unalifahamu  tumbo langu hiki ni kitambi kweli?. Sasa yule daktari akakimbia kutafuta wenzake na wakampeleka kwenye X-ray  na wakakuta kumbe mbavu zimepasua pafu lake, na hewa imejaa sasa na karibu ina “collapse” yale mapafu.
Sasa wakamtoboa toboa ili kutoa hewa, na wakamwingiza ICU (chumba cha mahututi) maana hali yake ilikuwa mbaya sana. Sasa nilipofika kumuona,  Alisema kwa sauti ya chini na akasema niletee watoto tulikuwa na daktari pale, saaa sasa tulipotoka tukaona Daktari anafuta machozi  sasa ukiona daktari analia, Lazima u muulize vizuri,
Sasa nikamuukiza halooo niambie vizuri unapolia unameona nini, akasema akiamka vizuri asubuhi lazima iwe ni muujiza.  Sasa yule ndugu aling’ang’ana nimpelekee watoto.  Basi nikakimbia kuwachukua watoto na kumpelekea pale hospitali. Alishindwa kuongea akatupungia mkono, basi nikatazama wale watoto, na nikamwamgalia na yeye mwenyewe, na mke wake. Nikawaacha hapo na nikarudi kwangu.
Sikupata usingizi maana tulikuwa karibu sana na wakati huo tulikuwa na mikutano karibu,  Sasa nikawaza kuwa akiondoka lazima kila kitu kitavurugika. Basi nikaanza kuomba Mungu naomba nifundishe, naliombeaje jambo hili, Mungu akasema niandikie barau  kwanini unatakaa huyu mtu abaki. Kwa hiyo nikaamka pale  na nakaenda kuchukua barua.
KUTOKA KWA  CHRISTOPHER MWAKASEGE
KWA MUNGU BABA,
KATIKA JINA LA YESU,
Naomba fulani fulani  (Yule ndugu aliyepata ajali) naomba abaki, amelazwa hospitali hii asife, naomba mwongezee miaka ya kuishi kwa sababu
➖ hajafikisha miaka ya kuishi ile miaka 70
➖ Mke wake anamhitaji
➖Watoto wake wanamhitaji
➖ Tunamhitaji kwenye huduma
Kwa hiyo nikaorodhesha, nikamaliza. Baada ya hapo nilikuwa sijui nafanyeje baada ya kuandika Kwa hiyo nikamuuliza MUNGU kuwa sasa ndio nafanyeje? Akasema ibandike mikono, na nikaomba mpaka nikasikia amani huku ndani.
Sasa kesho yake asubuhi wakati naenda hospitali nikapita mahali ambapo pana photocopy,  nikatoa photocopy ile barua, nilipofika hospitali nikapita mahali ambapo mke wake alikuwa maana mke wake alisikia vibaya sana  maana hakuta kwenda hospitali asubuhi ile maana angekuta mume wake amekufa.
Kwa hiyo nikamkuta mahali apokuwa nikamwambia kuwa  nimemwandika Barua Mungu  angalia hizi point kama una za nyongeza andika. Akanitazama pale nikamwambia kuwa una haki kwa mume wako kuliko mimi, mimi nimejaribu kuandika tu. Nikamwambia kuwa si unamhitaji mume wako, ongeza basi pointi hapa,  basi nikamwachia  ile copy ya barau na nikasema twende hospitali sasa.
Tulipofika hospital tulikuta hajafa ila hali yake ni mbaya sana. Akasema Mwakasege una uhakika atapona, nikasema sio kwa kumuangalia hivi utakata tamaa. Nikasema sisi tuendelee kumsomea Mungu hii barua sawa sawa mama?, nikasema wewe rudi kwenye hoteli yako tuendelee kumsomea Mungu hii baraua na mimi Ntaendelea kumsomea Mungu barua. Kwa hiyo tukaachana (Hapa ninavyo ongea ni mzima mpaka leo, kama miaka 20/30 iliyopita)
Sasa akatusimua (Yule ndugu aliyepata ajali) kuwa baada ya siku mbili, akasikia sauti inamwambia kuwa umepona kaa. Sasa fikiria alikuwa amevunjika na haruhusiwi kukaa na kawakewa mipira ya hewa, sasa akakaa na akaanza  kuchomoa ile mipira na yule nesi akiyekuwa zamu akajua kuwa huyu lazima kapata kichaa akakimbia kumshikia kuwa rudi lala hapo. Yule ndugu akamwambia kuwa Yesu ameniambia kuwa nimepona. Nesi haelewi akasema lala, maana haelewi maana si kila mtu anayeingia ICU ana Yesu. Alipoona yule ndugu amekazana akasema lala hapa nikamwite daktari.  Sasa daktari alipokuwa alimkuta yule ndugu katoa mipira na anapumua kawaida kabisa.  Akashangaa sana akamuuliza kuna nini,  Yule ndugu akasema Yesu kaniambia kuwa nimepona.
Sasa Daktari akasema ngoja niangalie kama kweli basi akacheki pale,  na akamgeuza akaona tumbo limerudi kawaida liko sawa,  Sasa kidaktari wakasema hatuwezi kukuruhusu, basi wakampelekea wheelchair , baada ya siku moja wakaondoa wakampa magongo mawli, baada ya siku moja wakaondoa magongo mawili  wakabakiza moja. Baada ya siku tatu wakaondoa magongo yote.  Baada ya siku tano akaruhusiwa kutoka hospitali,  baada ya mwezi mmoja akaemdesha gari mwenyewe kwenda kuwashukuru madaktari. Ni mzima mpaka leo.
Nimekueleza hayo ili ujue kuwa Mungu anaweza akakuelekeza maelezo ya ziada,mimi nilipewa maelezo ya ziada sasa sijui ya kwako ya ziada  ni ya namna gani. Unahitaji kuteka sikio. *Ndio maana unahitaji kusoma kile kitabu cha Viashiria*  maana Mungu anaweza akakusemsha binafsi, Mungu alinipa maelekezo  wakati wengine wote wanasema haiwezekani. Ndani yako kama una amani, hata kama wanaona haiwezekani, wewe kama una amani huko ndani, utavuka.
Glory to God,  Glory to God.. haleluyaaaa haleluyaaaa. ...
Uko tayari kwa ajiri ya maombi. ... ..
*SIKILIZA MAOMBI KWA LINK YA YOUTUBE NILIYOWEKA PALE JUU ☝☝☝☝*
[07:43, 16/05/2018] Filix Bwanji: *8⃣.SEMINA YA NENO LA MUNGU DODOMA UWANJA WA BARAFU*
*MWL.CHRISTOPHER MWAKASEGE*
*SOMO: UWEZO WA MUNGU JUU YA MAGONJWA NA VYANZO VYAKE.*
*TAREHE  13 MAY, 2018*
*SIKU YA NANE*
*👉 NAMBA ZA SADAKA* https://goo.gl/Z3ozYB
*👉LINK YA SEMINA YA LEO YOUTUBE* https://youtu.be/9JiipLqBB4c
*👉NAMNA YA KUPATA CD&DVD BONYEZA HAPA* https://goo.gl/tgwoub
Leo ikiwa ni siku ya nane au mfululizo wa nane au vipindi saba vimetangulia na kama hukunisikiliza siku hizo saba zilizotangulia hakikisha unaagiza au unachukua CD au Kanda yako sikiliza na kusikiliza na kusikiliza kwa sababu imani huja kwa kusikia na kusikia huja kwa kusikia mara nyingi zaidi, kusikia mara moja haitoshi ili upate kitu cha kukusaidia.
Leo nataka tuangalie
*UWEZA WA MUNGU JUU YA MAGONJWA YANAYOPITIA KWENYE NDOTO NA KUJITOKEZA KWENYE MWILI WA MTU.*
*Danieli 4:4‭-‬33*
Ila nasoma 4-5
_“Mimi, Nebukadneza, nilikuwa nikistarehe nyumbani kwangu, nikineemeka katika nyumba yangu ya enzi. *Nikaota ndoto iliyonitia hofu; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha.*_
Akatafuta watu ili wamsaidie na hawakumsadia, bali Daniel akamsaidia kumwambia ndoto yake na tafsiri yake
24-26
_Tafsiri yake ni hii, Ee mfalme, nayo ni amri yake Aliye Juu, iliyomjia bwana wangu, mfalme; ya kuwa utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa mwituni, nawe utalazimishwa kula majani kama ng'ombe, nawe utanyeshewa na umande wa mbinguni, na nyakati saba zitapita juu yako; hata utakapojua ya kuwa Aliye Juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote. Na kwa kuwa waliamuru kukiacha kisiki cha shina lake; ufalme wako utakuwa imara kwako, baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala._
33
_Saa hiyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadneza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng'ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege._
Hapa tunaona jinsi ndoto inavyotumika kupitisha ugonjwa ndani ya mtu na kutokeza kwenye mwili wake. Huyu mtu aliota ndoto miezi kumi na mbili (12 months) iliyopita, kwenye ndoto kaoneshwa vitu kadhaa kama asingepata mtu wa kumsaidia kutafsiri labda asingejua lakini alihakikisha amempata mtu wa kumtafsiria ili ajue usahihi wa jambo na katika tafsiri ndipo anaelezwa kitakachotokea na matokeo yake, na kuambiwa kitakachompata. Hakuambiwa kitatokea lini ila atengeneze mambo yake bali yeye alikaa miezi 12 bila kutengeneza na kile alichotafsiriwa katika maisha yake (kwa lugha ya kawaida tunaweza kusema akawa kichaa) lakini angalia huo ugonjwa ulipitia kwenye ndoto.
Angalia
*Ayubu 4:12‭-‬16*
_“Basi, nililetewa neno kwa siri, Sikio langu likasikia manong'ono yake.   Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya usiku,(ndoto ya usiku) Hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu.  Hofu iliniangukia na kutetemeka, Iliyoitetemesha mifupa yangu yote.   Ndipo pepo ilipita mbele ya uso wangu; Na nywele za mwili wangu zilisimama.  Hiyo pepo ilisimama kimya, nisiweze kutambua sura zake, Mfano ulikuwa mbele ya macho yangu; Kulikuwa kimya, nami nilisikia sauti, ikinena,”_
Huyu ni Elifazi rafiki yake na Ayubu akieleza kilichompata baada ya kuota ndoto iliyosababisha hofu kumwingia pia aliona pepo kwa macho kamili. Na maandiko yanasema “mifupa yake ikatetemeka”. Kati ya magonjwa yanayosumbua ni magonjwa ambayo yanapita au yanapitia kwenye ndoto.
Mungu aliponipa nafasi ya kujua kwamba anazungumza na wanadamu kupitia kwenye ndoto na Mungu akaanza kunisemesha vitu mbalimbali ndio nikaanza kufuatilia siku nyingi kidogo. Ila nikaanza kujifunza kuwa kama kitu cha kwangu mwenyewe kwa kupitia kwenye maandiko na msaada maeneo mengine sikupata msaada unaotakiwa. Nilirudi kwa Mungu nikaendelea kuomba nae akanifundisha nikashangaa aliponiambia fundisha na wengine kwa sababu sikutegemea kama ni kitu cha kufundisha na wengine lakini kazi yangu ni kutii tu kile kidogo Mungu amenipa na kuwamegea wengine kidogo kidogo.
Sikutegemea ule mwitikio na watu kuandika kwenye barua na kwenye simu. Na tulikuwa tunaziweka kwenye mifuko tofauti tofauti, na nilipata nafasi ya kusoma ndoto nyingi (sijazimaliza zote) na nikawa nakusanya kimakundi kwa kuweka kila ndoto kwenye kundi lake, zingine nikizisoma naelewa moja kwa moja na nyingine zisielewi narudi kwenye maandiko na kumuuliza Mungu jibu lake liko wapi na Mungu ananioneshea kwenye Biblia.
Haijalishi chanzo chake ni Mungu, shetani au shughuli nyingi au hali ya kiroho ya mahali ambapo ulilala au umelala. Tafsiri sahihi ya ndoto utaipata ndani ya Biblia kwa Mungu alie hai kwa njia ya Kristo Yesu.
Haina maana mtu mwingine hatakutafsiria, atakutafsiria lakini hatakupa ujumbe wa Kimungu kwa sababu Mungu ndie anaejua ujumbe ulioko ndani.
Kama shetani ameficha kitu huko cha kwake au kama ukienda kwa mtu anaetumia nguvu za giza kukutafsiria unafikiri atasema ni tafsiri ya shetani, labda kama anakupa masharti fulani atakutafsiria kwa speed. Lakini kama ni kitu cha Kimungu au ni kitu cha shetani au kwa vyovyote vile, Mungu atakupa tafsiri.
LAZIMA uwe na fahamu, kwa sababu unapoanza kutafsiri au mtu kukutafsiria muulize imeandikwa wapi kwenye Biblia kwa sababu kusikia huja kwa neno la Kristo (sio kwa tafsiri). Kwa hiyo hata akikutafsiria lazima akupe na maandiko ili usikie na ujue ujumbe uliopo.
Nataka nikusomee baadhi watu ambao walituandikia bila kutaja wapi walipotokea na vitu vingine nimeacha kwa makusudi ili uweze kujua.
Mmoja katuandikia kwenye simu kuwa mwalimu
*SHUHUDA, NDOTO NA MAOMBI*
➖ Bwana Yesu asifiwe. Leo mchana mume wangu kalala hata dakika 40 hazijapita akashtuka akaona ametoka mjini na watoto na wakapata ajali mbaya.
➖Mwingine alituandikia kwenye simu na kusema BWANA YESU Asifiwe! Leo mchana mume wangu kalala hata dakika 40 hazijafika akashtuka akaniambia ameota ametoka mjini yuko na watoto na wakapata ajali mbaya, amegonga mtu akapasuka kichwa na kupoteza maisha. Aliposhtuka kutoka usingizini kichwa chote cha kwake upande wa kulia kinauma. Sasa kuna uhusiano gani kati ya ndoto aliyoota na kupasuka kwa kichwa cha mtu mwingine na maumivu yake?
➖Mwingine aliandika akisema Niliota ndoto maaskari watatu wananivamia kwenye ndoto na wakanichoma mkuki kwenye ndoto, kwenye macho na ndipo tatizo la macho likaanza hasa jicho langu la kulia. Sasa kuna uhusiano gani kati ya kuchomwa kwenye ndoto macho yake na jicho lake la kulia kupata shida?
➖Mwingine aliandikia kusema! Namshukuru sana MUNGU nimepona mgongo, nilichomwa kisu kiunoni kwenye ndoto mwaka 2015 nikapata shida kwenye uti wa mgongo, ndoa yangu ikaharibika, uchumi vivyo hivyo, watoto wakaanza kushindwa/kufail shule. Sasa hii aliandika baada ya kusikia nikifundisha somo la ndoto mahali pengine kwa hiyo akasema leo hii (siku hiyo ya kusikia) baada ya kusikia, maana sikuwahi kulisikia kabisa somo la namna hii hivyo nimepona. Kwa hiyo alikuwa anaandika ushuhuda baada ya kusikiliza maombi kwa njia ya radio. Si rahisi sana ukamweleza mtu mahusiano juu ya ndoto aliyoota na maumivu aliyoyapata kwenye mgongo wake
➖Mwingine aliandika: Mama yangu alikufa kwa ukimwi na dada yangu vivyo hivyo, mara baada ya dada yangu kufa niliota ndoto ambayo niliona mtu akiniambia kwenye ndoto kwamba na wewe utakufa kwa ukimwi. Nilipoamka nikaomba kwa MUNGU anisaidie ili neno hilo lisitimie kwangu. Ulipofika wakati wangu wa kuolewa tukaenda na mchumba wangu kupima afya zetu mchumba wangu akakutwa na afya nzuri lakini mimi nikakutwa na ukimwi. Tukakubaliana na mchumba wangu tusimwambie mtu na tuendelee kuomba na tuendelee na mipango ya harusi (Kulingana na mazungumzo yake waliamini hilo ni pando la shetani tu) waliamua kulipiga kwenye maombi bila kuwashirikisha watu wasije kuwakatisha tamaa. Anasema tukaowana na nikapata ujauzito, nilipoenda kliniki wakanipima na kukuta ukimwi bado upo siku chache baadaye nikasikia kuna semina ya NENO LA MUNGU inafanyika Jagwani ikiongozwa na Mwalimu Mwakasege nami nikaenda kusikiliza mafundisho. Wakati wa kipindi cha maombi nikasikia mwalimu akisema ukimwi unaondoka kwenye damu yako katika JINA LA YESU.
Niliposikia maneno hayo nikasema kwa sauti ni mimi napokea maneno hayo katika JINA LA YESU, baada ya semina nikaenda tena kliniki ile walionipima mwanzo na nikaomba wanipime upya. Baada ya kusita kwa muda mwishoni wakakubali, matokeo yalipotoka yakaonyesha ukimwi sina lakini nesi na daktari waliopima hawakuamini wakifikiri vipimo vimekosewa, wakapima tena na kukuta ukimwi hakuna, bado hawakuamini wakamwambia tunafuata matokeo yale ya mwanzo ya kwamba ukimwi unao, akasema nikaondoka bila kukubaliana na uamuzi wao nikaenda hospitali nyingine na kuomba nipimwe ukimwi, nikapimwa na kipimo kilipotoka nikakutwa sina ukimwi, nikarudi na hicho kipimo kwenye hospitali ya mwanzo na kumuonesha daktari wa mwanzo, daktari alishangaa sana huku akisema MUNGU ni mkubwa, halafu akaendelea kusema naendelea vizuri  na nilizaa mtoto bila shida na hana ukimwi na nilizaa na mtoto wa pili akiwa mzima na mimi ni mzima, lile tishio la ukimwi halipo kwani MUNGU ameniponya. Sasa angalia lilipopitia maana alisemewa neno kwenye ndoto na ikamsumbua.
➖Mwingine akaandika na kusema; BWANA YESU Asifiwe Mwalimu, nakumbuka siku chache kabla ya kufanya mtihani wa kidato cha sita niliota niko kwenye chumba cha mtihani wakati wa kukaa kwenye kiti ili nianze mtihani nikawa kama nimekaa vibaya nikashtua mgongo, nilipoamka kutoka usingizini nikakuta mgongo unaniuma mpaka sasa niko chuo kikuu mwaka wa kwanza mgongo unaniuma. Nimeokoka naomba uniombee. Kwa hiyo aliposikia nikifundisha ndipo alipoanza kuoanisha juu ya ndoto aliyoota na maumivu anayoyapata kwenye mgongo wake
➖Mwingine aliandika na kusema; Kuna siku niliota nimefungwa na sanda mwili mzima, wamechanganya kichwani na usoni wamenifunika kwa kitambaa cheusi na cheupe, kuanzia siku hiyo nilipoamka kutoka usingizini usoni nasikia kama kuna ngozi nyingine, ngozi imekakamaa na wakati mwingine nasikia kama utitiri unatembea usoni baba naomba uniombee.
➖Mwingine aliandika na kusema; Wakati karibu kunakucha niliota ndoto ambayo ndani yake niliumwa kwenye paja langu la kushoto na kitu ambacho sikukiona na mara nikashtuka kutoka usingizini, na muda si mrefu nilisikia mwili wote ukiniwasha sana na mara viuvimbe vingi vikatokea sehemu mbalimbali za mwili, na nilipoenda kupima hospitali nikakutwa na magonjwa mengine ambayo sikutarajia kuwa ningekuwa nayo nilipewa dawa lakini hazikunisaidia, lakini watu walikazana kuniombea na sasa nimepona kwa sehemu kubwa BWANA YESU Asifiwe! Sasa ndugu huyu alikuwa anaandika ushuhuda wake ili watu wengine waweze kujua ya kwamba hivi vitu vipo na unahitaji kuvifuatilia kwa njia ya maombi.
➖Mwingine aliandika na kusema; Niliota kuna mtu kavunjika mguu mpaka mfupa ukawa unaonekana na hata nilikuwa nikikaa labda nasafiri (maana yake alikuwa anafikiri labda anasafiri na kwamba yale maono yalikuwa yanamuhusu yeye na hakuwahi kuwaza kama ni vita, ndivyo alivyoandika). Mwezi mmoja baadaye (baada ya kuota hiyo ndoto) niliugua miguu na maumivu yalikuwa makali sana sikuweza kulala, ilikuwa ikifika saa saba usiku nashtuka, mwili unapata moto na hapo nitakuwa macho mpaka asubuhi. Hospitali tatizo halikuonekana, nilikunywa sana dawa mpaka kuja kuanza maombi na kukemea mapando ya kishetani ndipo nilipopata nafuu na hatimaye nikaweza kutembea vizuri. Mpaka muda huu sijamuacha MUNGU wangu na hakika sitamuacha. Ubarikiwe sana baba
➖Mwingine akaandika na kusema; Naomba niombewe niliota usiku damu inatoka sehemu za siri, inachuruzika kama mfereji mdogo, toka kipindi hicho nilipoamka mzunguko wa damu wa mwezi umebadilika na kuvurugika.
➖Mwingine akaandika na kusema; Niliota nyoka ameniingia mguu wa kushoto na tangu wakati huo upande wangu wa kushoto wa mwili unakufa ganzi mara kwa mara na kukakamaa.
➖Mwingine  akaandika na kusema; Naomba uniombee Mtumishi naumwa, niliota nang’atwa na mbwa mkononi, leo nausikia ule mkono niliong’atwa na mbwa unaniuma kuanzia kwenye bega na ni kama unakufa ganzi
Barua au meseji za namna hii zipo nyingi sana, na huwezi kumwombea mtu wa namna hii kirahisi ni lazima uende mbele za MUNGU ukamuulize aweze kukupa utaratibu wa kumsaidia. Lakini tunamshukuru MUNGU anayetupa nafasi ya kuviona vitu hivi na kujifunza hata kufanya maombi na watu wanapokea na kupona.
Sasa ziko *HATUA* kadhaa ambazo zinaweza kukusaidia kama ukipata shida ya namna hiyo au kuna mtu mwingine akapata shida ya namna hiyo akaeleza na ROHO MTAKATIFU akaweza kukuoanishia hivyo vitu viwili. Ziko *HATUA* kadhaa nami nitazitaja kwanza kwa mfululizo
Wale walio kuwepo Jana wanaelewa zile zingine nilipokuwa ninataja za masuala ya urithi ni kitu  ambacho ninaweza nikakitaja Mara moja na nikaziombea Mara moja usione mgawanyo huko ndani, lakini nakuwekea huu mgawanyo kwa makusudi kabisa ili uweze kujua kitu gani kipo huku ndani.
Ukienda hospitali saa nyingine unaumwa na ukapewa kidonge wakakwambia kidonge hiki kunywa mara moja kabla ya chakula, daktari anajua ndani ya kidonge kuna dawa tatu nne au tano kulingana na sheria za kimataifa lazima kila dawa lazima iandikwe ina vitu vingapi watakwambia hii ni % kadhaa na hii ni % kadhaa na hii ni milligrams kadhaa. Hizi ni sheria za kimataifa lakini wewe umekunywa kidonge kimoja unafikiri umekunywa kidonge kimoja dawa moja ni  tatu nne au tano wao ndio wanaoujua hii imewekwa kusaidia hiki na hii inasaidia hiki, saa nyingine huko nyuma ugonjwa mmoja ulikuwa unapewa vidonge vitano unarudi hospitali baada ya mwaka moja, unakuta wamekusaidia wameweka kidonge kimoja dawa tano  sasa usije ukafikiri vile vitano vimeondolewa, lakini technolojia imerahisisha dawa tano wameweka kwenye kidonge kimoja kwa hiyo kidonge kimoja kinakupa vitu vyote vilivyokuwa kwenye vidonge vitano, na saa nyingine unakuta wameongeza na kitu kingine. Kwenye Biblia ni hivyo hivyo unapokutana na mtu anaomba akasema neno moja usije ukafikiri ameomba neno moja ndani yake kuna vitu vingi ambavyo Mungu anavikusanya kwa pamoja, anajua shidaa hii au ugonjwa huu kidonge chake ni hiki anajua kabisa katika ugonjwa huu anahitaji vidonge vitatu kwa hiyo sasa anampa muhubiri anaweka ndani ya kidonge kimoja halafu anatamka neno halafu yule mtu anapokea uponyaji, wewe unapokea uponyaji ukifikiri ni lile neno lilotamkwa  ndio limemfanya yule mtu kapona hapana bali ni kilichopo ndani ya neno! Kilichobebwa na neno! Ndio maana huwezi kukopi na kupest lazima iwe ni imani yako kwa hiyo huwezi kukopi tu na kuhamisha kwa hiyo andika hizi hatua halafu tutazungumza baadae.
OMBA TOBA KWA KILICHOSABABISHA MLANGO WA NDOTO UKAPITISHA UGONJWA HUO.
NYUNYIZA DAMU YA JUU ENEO LILILOPATA SHIDA KWENYE NDOTO
          
*Waebrania 9:18-22 na Danieli 4:26 na Danieli 5:21*

NYUNYIZA DAMU YA YESU JUU YA ENEO LA MWILI WAKO LILILOPOKEA UGONJWA BAADA YA KUAMKA TOKA KWENYE NDOTO HASA IKIWA NI ENEO TOFAUTI NA LILE ULILOPATA SHIDA KWENYE NDOTO
NG’OA KWA KUTUMIA DAMU YA YESU PANDIKIZI LA UGONJWA NDANI YAKO LILOPANDWA KWA NJIA YA NDOTO
*Mathayo 5:13, Mathayo 26:28*
KEMEA KWA JINA LA YESU PEPO LILOPATA NAFASI YA KUKUBEBESHA UGONJWA HUO
*Marko 16:17, Ayubu 4:12-16*
NYUNYIZA DAMU YA YESU KWENYE LANGO LAKO LA NDOTO ZAKO ILI LISIPITISHE MAGONJWA.
*Waebrania 12:24, Kutoka 12:12-23*
Angalau hizo hatua sita zitakupa mtaji, haimaanishi zipo hizo tu lakini hizi ukizifuata zitakupa mtaji na Roho Mtakatifu atakupanulia kufuatana na mazingira ya hiyo ndoto unayoombea na ugonjwa unaouombea. Nimekueleza hizi hatua ndizo ambazo Mungu amenipa na nimekuwa nikizitumia kuwaombea watu waliopata hizi shida na wakapona, wengine mlinisikia nikishuhudia jambo hili kwa sababu unaweza kuona kitu ukabaki unashangaa kwa sababu nilikutana na dada ambaye aliota ndoto anacheza mpira wa miguu ilipofika zamu yake akapiga ule mpira alipoupiga ule mpira ndani ya ndoto mguu wake ukapata shida na alipoamka ule mguu alipojaribu kutembea anachechemea na alilala mzima kesho yake akaenda hospitali na mama yake, wakamwona daktari akawahudumia wakati wanatoka na Mimi nilikuwa napita hapo wakaja kunisalimia siwajui wakasema wananijua huwa wanakuja kwenye semina zangu, na tumekuona hapa tumeona tukusalimie nikauliza  kuna shida gani yule mama akasema “binti yangu amepata shida ya mguu” na yule msichana akasema “Baba niliota ndoto nacheza mpira ghafla nikapiga mpira na nimeamka mguu una shida” nikamuuliza “je uko tayari nikuombee?” maana ilikuwa mtaani kabisa, akasema “ndio” akaweka mkono wake kwenye shida na nikakusanya hizi hatua  nikaziweka kwenye kidonge kimoja  na nilipomaliza tu kuomba maumivu yote hayapo, nikamwambia chezesha tu mguu, wakatoka wanatembea vizuri wanashangaa na mimi nashangaa,maana ameingia hospitali anachechemea na walimpa dawa za maumivu za kumsaidia haikuchukua hata dakika mbili ameondoka mzima. Umewahi kufikiri umekutana na mtu wa aina hiyo usipojua utamuombea tu maombi ya kawaida tu.
Watu wengi sana wakiumwa kichwa wanakunywa Panadol hata bila kwenda hospitali, karibu kila nyumba ina panadol wanaenda hospitali alafu wanamwambia daktari nimekunywa dawa alafu kichwa hakiponi na wanagundua kuwa si kila kichwa dawa yake ni Panadol. Ungeenda kwa Daktari mapema angekutibu kilichosababisha kichwa kuuma na maumivu ya kichwa yangenyamaza. Na kwenye masuala ya kiroho divyo yalivyo na ndivyo Yesu alivyokuwa anafanya, alikuwa akishughulika tu na chanzo ugonjwa unaondoka.
Ndio maana ukiota ndoto za namna hii kumbuka hizi hatua na anza na *TOBA* Usijaribu kujihesabia haki maana toba ina kazi kubwa sana. Ukisoma kwenye kitabu cha Daniel wakati Nebukadreza anajieleza na Daniel alikuwa anamueleza vizuri kabisa kuwa hii hukumu imekuja kwa amri ya walinzi na unatakiwa kutengeneza na Mungu, maana kuna namna fulani Mungu anakutengenezea nafasi inayostahili kwenye maisha yako, rekebisha mambo yako na usiporekebisha mambo yako utaondolewa hapo na utakaa porini.
Kwanini nakuambia ufanye Toba, ni kwa sababu ndoto ni mlango wa kiroho na uliumbwa na Mungu kama njia mojawapo ya mawasiliano na mtu anapokuwa amelala. Dhambi ilipoingia ikatoa nafasi ya huo mlango kutumiwa na shetani pia, kwa hiyo ukiona ndoto imepitisha kitu cha namna hiyo ujue kuna shida mahali. Nebukadreza hakujua kama kile alichoota kwenye ndoto kitakuja kutokea miezi 12 baadae yeye amedharau na yakampata kweli.
Lakini hatua ya pili nikakwambia *NYUNYIZA DAMU YA YESU JUU YA ENEO LILILOPATA SHIDA KWENYE NDOTO* ukisoma kwenye kile kitabu cha Daniel.
*Danieli 4:26*
_Na kwa kuwa waliamuru kukiacha kisiki cha shina lake; ufalme wako utakuwa imara kwako, baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala._
Sasa anatoa tafsiri yake anasema hicho kisiki, kwenye biblia ametumia kiti cha enzi kitatunzwa imara mpaka utakapojua mbingu ndio zinazotawala na Mungu humpa nafasi yeyote amtakae. Alifanya kosa akiwa kwenye kiti matokeo yake amepata ugonjwa wa kichaa, kwa hiyo *unanyunyiza Damu ya Yesu kwenye nafasi* mwingine akasema nimeumwa kwenye mguu kwa hiyo unanyunyiza Damu ya Yesu kwenye mguu haijalishi hayo matatizo yanatokea wapi. Mwingine nimekusomea anasema “aliumwa na mdudu kwenye paja hata hajui ni wa aina gani, na huyu ambae aliota amegonga mtu na yule mtu kichwa kikapasuka.
Hili sio suala tu la kusema mimi sioti ndoto, ndugu umepunjwa maana ndoto ni njia mojawapo ambayo Mungu anatumia kuongea na watu kwa hiyo kama huoti ujue kuna mlango umezibwa shida ni aina ya ndoto unazoota. Mwingine anasema “kila nikiota zinatimia” pia sio sahihi kwa sababu sio kila ndoto unayoota lazima itimie tumeona kwenye kitabu cha Daniel, Daniel anamwambia Nebukadreza atengeneze mambo yake,kwa hiyo hatua ile ya kwanza ingeondoa ile ndoto yote na ile adhabu.
Hatua ya tatu: *HAKIKISHA UNANYUNYIZA DAMU YA YESU JUU YA ENEO LA MWILI WAKO LILOPOKEA UGONJWA BAADA YA KUAMKA KUTOKA KWENYE NDOTO.*
Sasa ukisoma kile kitabu cha Daniel unaona pale Nebukadreza aliona Kisiki hakujiona yeye bali aliona kisiki sasa  aliona Mtakatifu anatoa amri mti ukatwe  na akakatwa, yeye alifikiri ni mti kumbe ni yeye anaondolewa kwenye cheo lakini nafasi yake inatunzwa
*Daniel 4:33-34*
_Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadreza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng’ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege.   Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi;_
Kwa hiyo mti umekatwa, unanyunyiza Damu ya Yesu kwenye kiti chake au position yake, sasa hatua hii ya tatu ona uponyaji ulipoibukia, uliibukia kwenye ufahamu wake maana ndipo ulipokuwa umebanwa, akawa kichaa.
*Daniel 5:21*
_Akafukuzwa mbali na wanadamu, moyo wake ukafanywa kuwa kama moyo wa mnyama, na makao yake yalikuwa pamoja na punda-mwitu; akalishwa majani kama ng’ombe, mwili wake ukalowa maji kwa umande wa mbinguni; hata alipojua ya kuwa Mungu Aliye juu ndiye anayetawala katika ufalme wa wanadamu, na ya kuwa humweka juu yake yeye amtakaye, awaye yote._
Huyu ni Daniel anamueleza mtoto wa Nebukadreza kwa kosa kama la baba yake ambalo alilifanya kwa kutompa Mungu heshima anayostahili,  na biblia inaeleza kilichompata baba yake.  Biblia inasema moyo wake ukafanywa,  kwa hiyo unanyunyiza Damu ya Yesu kwenye cheo, kiti  au nafasi.
Hatua ya tatu, tazama ugonjwa ulipoibukia, moyo wake umebadilishwa,  kwa hiyo unanyunyiza Damu ya Yesu kwenye moyo wake na ufahamu wake.
Nilikuwa namuombea mtu aliyepata shida, aliumwa na nyoka kwenye mguu kwa hiyo nikawa naenda na hatua za namna hii, hakusema amepata shida kubwa ndani yake ya namna gani bali anaeleza tu namna ilivyokuwa.  Na mimi nikaenda hatua kwa hatu nikaomba, sasa nilipofika  hatua ya tatu kutaka kujua kuwa hiki kitu kimekaa wapi,  Mungu akanisemesha kwenye tumbo lake lakini nyoka alimuuma kwenye mguu.  Nilinnyunyiza Damu ya Yesu kwenye tumbo lake, lakini nilinyunyiza pia mahali alipopitia maana saa nyingine huwa panaacha alama.  
Nilikutana na mtu mmoja, aliumwa na nyoka kwenye ndoto na alipo amka akakuta alama na hazifutiki mpaka uziombee, maana ni mlango umefunguliwa. Niliponyunyiza Damu ya Yesu kwenye mguu pepo halikulipuka, ila niliponyunyiza kwenye tumbo, pepo likalipuka. Kwa hiyo unaweza ukaona nilienda moja kwa moja kwenye hatua ya tano, kukemea lile pepo kwa jina la Yesu. Si tu kukemea lile pepo bali mlango ulipofunguka,  na kuna pepo lilipita kama vile Elifazi anavyosema kuwa niliona pepo likipita mbele yangu na nywele zangu zikasisimuka, nilishindwa kulitambua. Ndivyo alivyosema Elifazi kwenye Ayubu 4.
Hatua ya nne *NG’OA KWA KUTUMIA DAMU  YA YESU*, Kwanini kwa kutumia Damu ya Yesu Biblia inasema katika Mathayo 26:28 , Damu ya Yesu ya agano imemwagika ili kuwa ondoleo la dhambi.  Kwa hiyo Damu inaweza kuondoa. 
*Mathayo 15:13*
_Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang’olewa._
Kwa hiyo huu mstari unakuruhusu kung’oa kila kitu ambacho shetani amepandikiza,  maana saa nyingine anapandikiza sumu, inategemea ni kitu gani kimekuuma, kama umeona aina ya mdudu inakusadia kuangalia aina ya sumu ambayo amepandikiza.  Ukienda  ndani ya Biblia itakueleza kila kitu.  Mbwa akikuuma itakueleza sababu zake, paka akikuuma itakueleza sababu zake, nyoka akikuuma na aina ya nyoka pia akikuuma ina sababu yake. Ukipigwa risasi kwenye  ndoto kuna sababu zake.
Mtu mmoja aliniambia kuwa alipigwa risasi kwenye ndoto na alipata kichomi,  nikamuuliza kwenye ndoto je risasi ikitoka, akasema hapana, kwa hiyo kwenye kutafsiri ndoto huwa nawaambia watu siku zote angalia ndoto ilivyoisha.  Ukiona umeamka kwenye ndoto na vita yake haina ushindi basi ujue vita yake ni mbaya.  Unahitaji kuanza kushughulika mara moja.
Wafanyakazi wa Farao, mwokaji wa mkate na myweshaji baada ya kuota ndoto tunaona mmoja ndoto yake iliisha vizuri  na mwingine iliisha vibaya yule mwokaji iliisha vibaya. Ndege wakala mikate yote.   Yusufu aliwaambia wewe ambaye ndoto yako umeliwa na ndege kichwa chako kutakatwa, na myweshaji atarejea kazini.  Ndoto zao zilitimia baada ya siku tatu tu. Nebukadreza alipewa miezi 12 alicheza nayo,na hawa walipewa siku tatu tu. Nafikiri hawa walijua ndoto tu. Lakini Mungu alikuwa anawasemesha kuwa kitu gani kitatokea, na  baada ya siku tatu  kilitokea vile vile.  Sasa angalia namna ndoto zako zinavyoisha,  kama haijaisha vizuri ingia kwenye maombi mara moja.  Kama ni sumu imepandikizwa hakikisha unaing’oa na kuifuta mara moja kwa Damu ya Yesu.
Kama ni pepo utajua ni aina gani, au limebebwa na picha ipi, sasa kama hujui aina ya pepo na limeigizwa kwa namna gani, basi sema jina la aina ya kitu kilichokuuma kwa hiyo unaweza ukasema,  pepo wewe uliyejificha  nyuma ya nyoka litajua na kama umesimama kwenye imani ya Damu ya Yesu  utashangaa kitu kitakachotokea.
Hatua ya sita: *NYUNYIZA DAMU YA YESU KWENYE LANGO LA NDOTO ILI LILINDWE* Maana damu ya Yesu  inaweza ikalinda maana ni Damu ya PASAKA kama ilivyoandikwa kwenye kitabu cha kutoka,  kama ilivyolinda hali ya kiroho ya wana wa Israeli ili uharibifu usiingie kwao na malaika wa  mauti aweze kupita.  Sasa kama damu ya wanyama, ilikuwa na nguvu kiasi kile, kwa sababu tu ya neno la Mungu si zaidi sana Damu ya Yesu iliyotamkwa zaidi kwenye agano jipya ambalo ni bora zaidi,   itakuwa na nguvu juu ya lango la kiroho lisipitishe kitu chochote ambacho ni kigeni.  Kwa hiyo unapolala funika lango la NDOTO usilale kienyeji kienyeji.
Zoezi la kuomba……..
*SIKILIZA YOUTUBE KWA LINK NILIYOWEKA PALE JUU…*
======BARIKIWA  NA KWA HERIII TUONANE SEMINA YA TANGA 5-10 JUNE 2018.===

Comments

Popular posts from this blog

UMUHIMU WA IBADA

IJUE IBADA-SEHEMU YA KWANZA