IJUE IBADA-SEHEMU YA KWANZA
SOMO LETU LA SASA..NI IBADA..
JE! IBADA NI NINI....?
~Lengo la somo ni kuimarisha uhusiano wetu na Mungu...
~Kujifunza na kumjua Mungu,ili kuweza kumwabudu kwa uhakika na kwa Imani...
Mathayo 4:10 *Ndipo Yesu alipo mwambia,Nenda zako,Shetani;kwa maana imeandikwa,Msujudie Bwana Mungu wako,umwabudu yeye peke yake.*
pia..ukisoma
Kumbukumbu la torati 6:10-14 lakini 12&13 inasema... *Ndipo ujitunze,usije ilukamsahau BWANA aliyekutoa nchi ya misri,nyumba ya utumwa.Mche BWANA,Mungu wako;ndiye utakaye mtumikia,na kuapa kwa jina lake.*
~ Kuna maswali mengi sana..ambayo yanahitaji ufafanuzi wa kina..juu ya ibada....
Maana lazima tujue..IBADA NI NINI...?? KWA NINI TUNATAKIWA TUFANYE IBADA??..NI WAKATI GANI...YATUPASA KUFANYA IBADA...?..JE! NINI KANAFANYIKA AU KINATAKIWA KUFANYIKA ILI NDO IBADA IKAMILIKE...?...
~ Somo hili si kwa wale..ambao wameokoka tu au kwa watu wa kanisa na dini fulani..ila ni kwa watu wote...maana majibu ya maswali hayo hapo juu..yanawza kutusaidia kujua..kuwa Ibada ni kwa ajili ya watu gani....
Tuanze hivi....
~ Ukisoma kwenye kamusi ya kiswahili... *Ibada ni tendo la heshima ya hali ya juu linalotolewa kwa kitu,miungu au Mungu.*
Ibada inaweza fanya na mtu binafsi ai kundi la watu..
~ Kwa maana nyingene..Ibada ina maana ya Utiifu na unyenyekevu,unao oneshwa na mtu au watu kwa kitu,miungu au Mungu..(kwa hisia za dhati kabisa toka ndani ya moyo ).kuonesha uhusiano uliopo..kati ya hao watu na hicho kinacho abudiwa/anae abudiwa.
~ Kwa wakrito Ibada ni jumla ya mabo yote yanayo mpasa mtu kufanya..katika maisha yanayo himiza na kuonesha uhusiano wa maisha ya mtu na Mungu..kwa msaada na usimamizi(kuongozwa) na Roho Mtakatifu..kupitia kweli yote na kutumia neno la kweli..lililofunuliwa na Yesu Kristo
Hivyo ibada..ni jumla ya mambo yote..yanayo takiwa kufanywa..ua yanayo fanywa..na ndiyo yanayo onesha utiifu..na unyenyekevu...na heshima ya hali ya juu..na utukufu wa Mungu(anaye abudiwa).
Hiyo ni maana ya ibada...lakini..kwanini tunafanya ibada..?? Na ibada tumfanyie nani...? Na wakati gani...? Na ni mambo gani..tufanye...ili yakamilishe n kulet maana ya ibada...?
~ YATUPASA KUFANYA IBADA KWA BWANA MUNGU,MUNGU MKUU..WA PEKEE ALIYE ZIUMBA MBINGU NA NCHI NA ALIYE ANZISHA UHAI WETU KWA KUMUUMBA ADAMU NA HAWA....
Kwanini tumwabudu yeye.....??
Ibada inapofanyika hicho kitendo kinaitwa..kuabudu..KUABUDU-Ni kunyenyekea..na kuonesha heshima ya hali ya juu..na kuonesha mapenzi ya dhati..yanayo ashiria utegemezi wa mtu kwa Nguvu itokanayo na kitu ambacho kinaabudiwa..au nguvu za anaye abudiwa....
~ Kuna aina nyingi za ibada..tutaona mbele kidogo....
Mfano biblia..inaposema usiabudu miungu...hii inaonesha kuwa tusiitegemee miungu..au kuinyenyekea miungu..au kuonesha heshima ya hali ya juu kwa miungu katika maisha yetu.....
miungu ni nini....miungu ni watu..wenye nguvu za kiungu ndani yao....
Mungu alipokiwa akiumba vitu..na wanadamu na malaika..ndani ya kila kitu aliweka uweza wa huyo mtu au hicho kitu kufanikisha jambo fulani..katika maisha....
Hiyo nguvu..yaweza elezeka au iseelezeke vyema...
Sasa...baada ya dhambi kuingia..ulimwenguni..na chanzo alikuwa ni malaika mmoja aliasi huko mbinguni...ambaye tunamwita shetani hii leo..na alipo asi alipewa hukumu ya kuangamizwa milele..lakini kabla ya wakati wakuangamizwa kwake haujafika...alianza kutumia nguvu alizo kuwa ameumbwa nazo na Mungu..na uweza alio kuwa nao...ili kuvuruga uhusiano kati ya wanadamu na Mungu....alianza kutoa ushawishi..kuwa sasa..watu na ulimwengu usimtegemee Mungu bali utegemee nguvu za kuingu zilizopo ndani yao..na hasa kwa kushirikiana na yeye..
Nguvu ya kiungu iliyopo ndani ya mtu au malaika..au kituchochote..haijitoshelezi kiukamilifu..inahitaji ushirika wa karibu na chanzo cha nguvu hiyo..ambapo chanzo ni Mungu mwenyewe....
Zaburi ya 82:1-8
Nataka uone..hii maana ya miungu ninayo kupa inatoka wapi....
Soma hiyo mistari yote..lakin mstari wa 1,5&6 inasema *Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu, katikati ya miungu anahukumu.....5..Hawajui wala hawafahamu,hutembea gizani;Misingi yote ya nchi imeharibika...na 6..Mimi nimesema, Ndinyi miungu,na Wana wa Aliye juu,nyote pia.*
~ Kulingana na hiyo hapo mistari napenda ifahamike kuwa kila mtu ndani yake ananguvu ya kiungu...ambayo ikipata connection na Mungu anaweza kukamilisha au kufanya jambo au muujiza...
Na shetani alitumia weeknes yetu..hiyo kuwa anatengeneza muunganiko au connection na mtu yeyote..kwa kumwongezea mtu malaika zake waasi(mapepo/mizimu/mashetani) na kuwapa watu uwezo wa kufanya mambo kwa uwezo usio wa kawaida....na anaanza kushawishi watu kumwabudi yeye..au kutegemea..hizo nguvu zake...kupitia kwa huyo mtu aloongezewa...roho za kishetani ili kutimiza malengo fulani...anayo kusudia shetani...ili kumsaidi shetani kuwashawishi watu..kumsahau Mungu..na kujikuta watu wawampi Mungu heshima anayo stahiri...na utiifu na unyenyekevu...sawasawa..na inavyotakiwa
~ Lakini nguvu hizo anazo kuwa nazo mtu kwa kupatiwa na mizimu..au mashetani...zina mipaka.yake..kuna mambo kweli zinaweza tekeleza lakini..zinamipaka..yake....pia mara nyingi hizi nguvu huleta uharibifu..kwa maisha ya watu...ndo maana utaona kuwa kuna waganga wanatoa utajiri..lakini..ukichukua dawa kwao kuna kuteketeza watoto..au ndugu...na masharti..mengi tu yanayo mfanya mtu kuwa mtumwa na kukosa uhuru..moyoni..wa kuishi..na kufaidi kwa uzuri..kile hizo nguvu zinampatia..maana lengo la hizo nguvu..ni kumtenga mtu mbali na Mungu..pia kuharibu maisha ya watu wengi....tofauti na nguvu za Mungu mkuu...Mungu mkuu yeye nguvu zake hazina mipaka..na zinauwezo juu ya kili kitu..hakuna jambo ambalo haziwezi kulitekeleza....na lengo la Nguvu za Mungu ni kufanikisha watu kuishi kwa amani..kulida amani..na kuleta maisha mazuri yasiyo na uharibifu....na hata tunapo zitumia hatuharibu..maisha na uhai wa watu wengine..au sisi wenyewe bali..Nguvu za Mungu zinatupa uzima wa Milele..kuishi daima pasipo kikomo...mara baada ya maisha haya ya sasa...lakini kutupa amani na ushindi tuwapo hapa katika ulimwengu huu wa sasa....
~Nguvu ya kiungu iliyopo ndani yetu..pia hufanya kazi kwa ufasahaa na uzuri..sawasawa na mapenzi ya Mungu pale tunapo kuwa katika Muunganiko na Mungu, Mungu huachilia Roho Mtakatifu ndani yetu..na tunaanza kufanikisha mambo na kufanya mambo kwa viwango vya juu...kuliko...vya binadamu wa kawaida..(viwango vilivyo juu visivyo vya kawaida
~Kumbuka..nilikupa hii maana ya ibada... *Kwa wakrito Ibada ni jumla ya mabo yote yanayo mpasa mtu kufanya..katika maisha yanayo himiza na kuonesha uhusiano wa maisha ya mtu na Mungu..kwa msaada na usimamizi(kuongozwa) na Roho Mtakatifu..kupitia kweli yote na kutumia neno la kweli..lililofunuliwa na Yesu Kristo*
Tuone neno linasemaje...
Marko 16:16-18 *Aaminiye na kubatizwa ataokoka;asiye amini,atahukumiwa.NAISHARA HIZI ZITAFUATANA NA HAO WAAMINIO; kwa jina langu watatoa pepo;watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka;hata watakinywa kitu cha kufisha,hakitawasha hakitawadhuru kabisa;wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya...*
Haya ni maneno ya Yesu Kristo...anajaribu..kuzungumza..namna ambavyo wale watakao amini..neno lake na Injili yake..juu ya WOKOVU...na watakapo amini..anawaambia wanafunzi kuwa wawabatize..na ubatizo huu anao ongea hapa..ni ule ubatizo alio sema yohna...kuwa yeye anabatiza kwa maji..lakini ajaye yaani Kristo atabatiza kwa moto na Roho Mtakatifu...
Kubatizwa..ni kutambulishwa..rasmi..hivyo kwa yule ambae ataamni..na kutambulishwa na Roho Mtakatifu mbele za Mungu kuwa ameamini..na kupokea Injili ya wokovu...ndani yake..atapewa uwezo usio wa kawaida..hata ataweza kuponya..kutoa pepo...kuongea lugha mpya..na mengine mengi...kama alivyo sema Kristo..
~ Nimejaribu kuelezea kwa undani kidogo kwa habari za nguvu na mamlaka..na ambayo ndani yake..yanatupa sababu..kuwa kwanini tumwabudu Mungu...?
Mungu alipo kuwa ananifunulia..haya mambo niliona kabisa kuwa kuna umuhimu mkubwa..kuwa hii kweli..inatakiwa ihubiriwe kwa watu..ili wakigu..dua na kuifahamu..itawasaidia..kupenda ibada..na kufanya mahusiano yao na Mungu kuwa mazuri zaidi....
Hivyo...basi..niseme tu kuwa..Mungu pekee ndiye anaye stahiri kupewa heshima ya hali ya juu..sana..na utiifu..na unyenyekevu..kwa moyo wa dhati kabisa..kwani uweza wake..na mamlaka yake..ni makuu sana...ila hii ni lazima kwanza tujifunze tujue..siri hizi za ukuu wa Mungu....ila kama usipo jua unaweza ukaanza kusema..mbona..sjaona ona kuu alililifanya....??.. Au utaanza kulinganisha nguvu za Mungu na waganga..maana umewahi kusikia kuwa wanauchawi hata wakumbadirisha mtu kuwa kuku..na ukazani huu ni ukui wa hali ya juu..sana...
Ukisoma.vizuri..habari za Mungu,mkuu ambaye..Kristo Yesu alikuja kufunua..ukweli..na uhalisia wake..utagundua..miungu yote ni haimfikiii..vijana wanasema..(miungu yote..hiyo utaiona chamtoto tu...)
Jitahidi..sana..upitie..vizuri..marambilimbili..hicho nilichokituma...maana..ni chakula..kizuri sana..na msingi mzuri sana...na ni siri nzito sana...maana utakapo kuwa unasoma..kuna mambo mengine..Roho wa Mungu atakufundisha zaidi ya nilicho kiandika...
Mungu atakubariki sana...na kukujaza nguvu na Roho Mtakatifu..
Mungu akuponye..akuinue..nakukutendea wema..na rehema..kwa kadiri ya uhitaji ulio nao..hapo ulipo kwa jina la Yesu Kristo...
~Kuna sababu..nyingi tu ambazo zinaweza kutufanya tukafanya ibada....kwa Mungu..au zinazo tupa umuhimu wa kufanya Ibada...
Tunafanya ibada ili kuleta Muunganiko wa kimungu..ili kupata kibari..na upendeleo wa kupata kile tunakihitaji alicho nacho Mungu (au anaye abudiwa)
mfano..Shetani alimtaka Yesu (amwabudu kwa lugha rahisi anyenyekee na kutoa heshima ya hali ya juu sana..kwa shetani ili shetani ampe mali na utajiri wote
~ Tunaweza fanya ibada ili kuonesha ukuu wa Mungu na upendo wa Mungu alio nao kwetu kwa watu wanao tuzunguka...
-hapa katika sababu hii na aina hii ya ibada...tunakuwa tunawasimuliwa watu..habari na sifa na heshima za Mungu..au (anaye abudiwa kwa kuonesha au kusimuloa uweza na nguvu alizo nazo)
~ Tunaweza fanya ibada au kumwabudu Mungu wetu...kwa kujitoa miili yetu..na maisha yetu yote..yatumike na Mungu ayatumie kwa ajili ya kufanikisha mapenzi yake..(au anaye abudiwa aweze kuitumia miili yetu na maisha yetu kufanikisha kile anataka kifanyike)
Kusudi sifa zake/au mamlaka yake ipate kutawala..na kuwafikia watu au kufika sehemu anataka ifike...
Warumi 12:1-2 *Basi ndugu zangu,nawasihi kwa huruma zake Mungu,itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai,takatifu, ya kumpendeza Mungu,NDIYO IBADA YENU YENYE MAANA....wala msiifuatishe namna ya dunia hii;bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu,mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema,ya kumpendeza na ukamilifu.*
~ Nikupe mfano huu...chukulia kuna sehemu matatizo au majanga yametokea..sasa watu wote mliopo pale..mnataka kuokowa watu walio patwa na majanga..na kwa sababu ya nia yenu mnayo taka kuionesha..mnajitosa iwe ni kwenye moto..au kwenye maji ya mafuriko..kutaka kuwasaidia watu..ili kuonesha upendo wenu..kwa hao watu...
~ Sasa kwa namna hiyo hiyo hapa paulo anajalibu kueleza kuwa...Kumwabudu Mungu au kufanya Ibada nzuri kwa huyu Mungu..ni kujitosa kabisa..miili yetu na nia zetu kuhakikisha kabisa..tunaonesha mapenzi ya Mungu..na ukamilifu anao tupatia Mungu...lakini pia sisi wenyewe tupate kumfahamu Mungu alivyo mzuri...baada ya kujiachilia kwake...
~ Namna nyingine ya ibada ni hii...kuachilia au kuruhusu nguvu za Mungu (au anaye abudiwa zifanye kazi) kwa watu au kundi la watu..au sehemu..ili kufikia kile tunataka kiwe..na kifanyike....na kitokee...
Mfano..najua usha wahi kusikia..kuhusu ibada za matambiko..unakuta familia wanatambika ili wawe salama..kwa mwaka mzima...au unakuta mtu anafanya ibada ya kumloga mtu..iliawe kichaa au apatwe na wazimu....(kumsomea dua)...hii pia kusudi ni kuonesha utendaji wa kazi na nguvu za huyo tunaye mtegemea...na kumpa utii na heshima ya hali ya juu...
~ Hiyo ni kwa miungu...lakini..kwa Mungu mkuu pia kuna maelekezo na sisi tunaluhusiwa kufanya ibada ya namna hii...
1timotheo 2:1-3 *Basi kabla ya mambo yote nataka dua na sala na maombezi na shukurani zifanyike kwa ajili ya watu wote...kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka tuishi maisha ya utulivu na amani..katika utauwa(uungu) wote na ustahivu...Hili ni zuri nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu.*
~ Kumbuka huko juu tuliona..na nikajaribu kuonesha..namna Nguvu za Mungu au nguvu za shetani zinafanya kazi....
~ Nilikuambia sisi binadamu tuliumbwa ndani yetu tukawekewa nguvu za kiungu...ambazo hizo nguvu zikipata connectiona na malaika au roho zinazo weza fanya kazi katika ulimwengu wa roho...tunajikuta tunaweza kutenda vitu vya ajabu..na miujiza na kufanya mambo mengi kutendeka..isivyo kawaida ya kibinadamu.....
~ Mganga wa kienyeji ni mgangwa kwa sababu kunamizimu na muunganiko wa roho yake..unaoleta nguvu na uweza ndani yake kufanya uganga....
Na nikasema kuwa sisi kwa tunao mfuata Mungu aliye Mkuu na Mwenye uwezo wote...tunapo ipokea kweli yake iliyo letwa Yesu Kristo..tunapata kuunganishwa na yeye..maana anamtuma Roho Mtakatifu(Roho wa Mungu) huya akija ndani yetu...nasi tunaanza kutumia nguvu ya uungu iliyopo ndani yetu kufanya mambo kwa namna isiyo kawaidaya kibinadamu
~ Lakini matumizi ya nguvu hiyo ya Mungu ndani yetu....inakuwa ibalenga kutimiza kile Mungu anataka..na zaidi sana kuendelea kutufanya kumpenda Mungu na kuwa na mahusiano na Mungu siku zote pasipo kupatwa na madhara pia pasipo kusababisha madhara kwa watu wanao tuzunguka...
Bado kuna mambo..mengi sana..natamani nipate kuyaeleza.....
~Wakati mwingine..unaweza sema..sasa mtumishi unafundisha mambo ya ibada..mbona..tunajua..tu hayo...?
Mbona kila siku..tunaenda na kanisani..na wachungaji wapo...na tunaabudu vizuri...tu...na mbona hata kanisani..kwetu kuna vitabu vya Mwongozo vya ibada...?..
~ Ni kweli..hayo yote yapo...lakini...moja kati ya siraha kubwa..na sehemu ambayo kanisa hatujapata ufahamu...ni swala...la ibada...
Maana kama tutafahamu..zaidi maana ya ibada..na tukajua...yote yahusuyo ibada...kanisa litakuwa na nguvu kubwa sana..lakini pia binafsi kila mtu atakuwa na nguvu kubwa sana...ya kuweza kusimama..imara katika imani..na kuishi maisha ya mafanikio...zaidi..
Pia tutaweza kuleta raha..na ile furaha ya wokovu ambayo imepotea..kwa watu wengi....sana...
~ Ni kuulize swali....mara ngapi umeenda kanisani...na kufanya ibada....na ukaona matokeo ya ibada hiyo..na ukafurahia..???
Je! Ni mara ngapi...umezifurahia ibada zinazo fanyika kanisani kwenu..kiasi cha kuzipenda..na kuona zinaumuhimu..na hata leo hii hautamani..kukosa..kuhudhulia...?
Je! Ushawahi jiuloza umuhimu wa ibada kwenye maisha yetu..na kwa jamiii kwa ujumla...?
~ Labda..nikuelezee kwa namna hii utanielewa...nini..ninaongelea...
Kwa wale..ambao wanaenda kwa waganga wa kienyeji kutafuta..dawa na uganga..kinacho wafanya kuweka imani yao kwa waganga hata kama sisi leo tunajua..kuwa nguvu yao..ni hasala..sana..na pia inamipaka....lakini...mara nyingi...matokeo wanayo yaona..mara baada ya kufanya hizo ibada kwa hao wanganga..ndiyo yanawapa..kuheshimu na kuamini..ibada..za kiganga na kishirikina...
~ Sasa..mi sifundishi uchawi..au sifundishi watu kwenda kwa waganga..ila ninacho fu.disha..ni IBADA...maana tukiweza kufahamu na kuelewa..matokeo ya kufanya ibada sahihi..kwa Mungu,Mkuu hii itatuongezea imani..na itatufanya tuwe imara sana..na kuona umuhimu wa kufanya ibada..sahihi katika maisha yetu....maana ni hatari sana kwa kanisa..kama tutakuwa tunafanya ibada..na hatujui...ninamna gani...yatupasa kufanya...na nini kinatokea tunapo fanya ibada...na pia zaidi..tusipo ona matokeo halisia..kwa kile tunataka tupate..au tuone..kikitokea..sawasawa..na lengo au kusudi lililo tufanya tufanye ibada...
~ Kumbuka ibada nimesema ni kitendo cha kutoa heshima ya hali ya juu..utiifu..na unyenyekevu..kwa miungu..au Mungu(kulingana..na ukuu ,heshima na nguvu zinazotokana na kitu kinacho abudiwa...)
~ Tukishindwa kutambua heshima...na unyenyekevu...na utiifu...ambao inatupasa kumpa Bwana Mungu wetu...uwe na uhakika au tarajia kuwa itafika sehemu..tutampa hiya heshima mtu asiye stahiri..na hii itakuwa tunajifungia baraka zetu na kujitakia laana..mbele za Mungu wetu......
Sikia...najua unafahamu kwa sehemu habari za wana wa Israeli...wale watu..ukisoma..habari zao kwa mtazamo wa kuchunguza heshima yao na utiifu kwa Mungu wao..utajua..nini.nina kisema...
Hawa jamaa..walimwamini Mungu..na wakamjua...kwa sehemu..lakini..walishindwa kutambua ukuu wa Mungu...wao..na matokeo yake...walijikuta..wakiangukia..kuabudu miungu mingine..na kujitengenezea miungu mingine...hasa pale..ambapo walishindwa kutambua..na kuona..matokeo ya ibada zao kwa Mungu wao...au walipo kosa mtu wakuwaelekeza...habari za ibada sahihi kwa Mungu wao...na kila walipo abudu miungu mingine..na kuipa heshima...walijikuta ndo wanajiongezea shida na matatizo..maana kumbuka nilikuambia...nguvu za miungu..hazipo ili kuleta amani..na suruhisho la matatizo...ila zinatumia matatizo kuongeza matatizo...na ndo maana mtu hana mali..anaambiwa aue mtoto..kwanza..ili apate mali....na akisha ua..mtoto..anapata mali..kweli..lakini..hakuna raha anayo ipata kwa zile mali...na akipata raha yeye..anasababisha..madhara makubwa sana..kwa watu wanao mzunguka..na hasa ndugu zake....na anakuwa mtumwa...wa mali...na siyo mtawala wa mali...
[22:18, 22/05/2018] Elisha Ndumizi: Najua..ni vigumu sana kuelewa hili jambo kwa siku moja..ila...inawezekana...kabisa tukajifunza..na tukaelewa..na kufahamu..yatupasa...
Mwanzo 2:1-3 *Basi mbingu na nchi zikamalizika,na jeshi lote..Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya;akastarehe siku ya saba,akaacha kufanya kazi yote aliyoifanya.Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe,akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.*
Tumeona sababu..kadhaa na namna kama nne za kufanya ibada...na sasa tuone..hii ya tano..inayo itwa SABATO...Namna nyingine ya ibada..ambayo Mungu..ameisisitiza sana kwenye biblia...
~ SABATO...inafahamika sana..na watu wengi..sana..kuwa ni..siku ya Bwana..na ndo siku ya ibada...kama ambavyo torati imeelezea...na hata agano jipya linavyo elezea...japo kwa sura tofauti...kidogo
SABATO...kulingana na kama inavyo elezewa katika kitabu cha mwanzo...ni siku ambayo Mungu alimaliza kufanya kazi ya uumbaji...lakini pia...ni siku..ambayo Mungu alizipima...kazi zake..na kuona zilikuwa katika viwango vya juu sana..kiasi ambacho havikuhitaji urekebishwaji...na akaamua..kuachilia..nguvu ya kiungu..juu ya kila alicho kiumba..sawasawa...na alivyo penda..(akavibarikia..)
na akaifanya siku hii kuwa ni siku yenye hadha..na heshima...na akapumzika...(akaridhika)
~ Hivyo...hata..baada ya kutoa sheria...kabra hajatoa siri ya siku ya saba...alisisitiza sana..kuishika siku hiyo ya saba...kuwa iwe ni siku ya kupumzika...
Comments
Post a Comment