WOKOVU NI NEEMA TUPATAYO KWA NJIA YA IMANI

Warumi 3:21-26
"Lakini sasa,haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria;inashuhudiwa na torati na manabii; ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya  imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio.Maana hakuna tofauti;kwa sababu wote wamefanya dhambi,na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haji bure kwa neema yake,kwa njia ya ukimbozi ulio katika Kristo Yesu; ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake,ili aonyeshe haki...yake kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zotd zilizotangulia kufanywa; apate kuonyesha haki yake wakati huu...ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabu haki yeye amwaminiye Yesu..."

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana...karibu sana...tujifunze pamoja..

Lengo la somo hili...ni..kukujengea..imani zaidi juu ya maisha yako..na kukupa uhakika..juu ya wokovu na Imani uliyo nayo
Kuwasaidia..ambao bado hawajaokoka..wapate..kuokoka na kupokea wokovu..
Kumekuwa na mafundisho mengi..ambayo yanaeleze habari za wokovu..na kuokoka...na imani ya kumwamini Yesu Kristo...
Hivyo ninavyo fundisha..ninaimani habari hizi kwa watu wengi..hazika  kuwa ngeni sana masikioni..mwao..lakini haimaanishi hazikuhusu....
Mafundisho mengi jui ya wokovu kwa njia ya Imani..hayajafanikiwa kujibu maswali nahoja..za watu wengi...na jamii imebaki katika..upungufu huu na hata kushindwa kabisa kutambua...utofauti..wa wokovu kwa njia..ya neema..iliyo letwa na Bwana Yesu Kristo...na pia habari za sheria..katika neema..na kwa maisha ya leo...na wengine..hawajafahamu kuwa inawapasa nao pia kumwamini Mungu na kupata wokovu..

-Nini maana ya kuokoka sasa..na maana ya wokovu...?
-Ninapo sema kuokoka..napenda ufamu fundisho hili kwa maana hii ifuatayo;-
"Kuokoka ni hatua ya kufahamu na kujua kwa usahihi na kuamini ya kuwa yupo MUNGU,ambae ameumba mbingu na nchi..na vitu vyote vinavyo onekana na visivyo onekana...na ukisha amini uwepo wa Mungu..pia laxima uamini na kufahamu kuwa mwanadamu hawezi kuishi pasipo Mungu...hivyo anahitaji msaada wa Mungu katika kila jambo...na akikosa mahusiano na Mungu..hawezi kufanikiwa..mwisho..atakufa" 
Waruni 10:9-10 "Kwa sababu..ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana,na kuamini moyoni mwako ya kuwa  Mungu alimfufua katika wafu,utaokoka...Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki,na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu"
-Hapo nataka uone...namna ambavyo paulo mwandishi wa kitabu hicho anavyo wafundisha namna kuokoka kunatokea...na mwisho wokovu una tokea...kwa mtu awaye yeyote...

Warumi 1:16 *Kwa maana siionei haya Injili;kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu..kwa kala aaminiye,kwa Myahudi kwanza,na kwa Myunani pia*

-WOKOVU-kutokana na vifungu..hivyo hapo juu..tunaweza sema...Ni hatua au msaada wa Mungu unao mpatia mtu awaye yote..mahusiano mazuri na Mungu...nimsaaada wa Mungu unao mtoa mwanadamu katika dhambi..na kumweka huru..na kuishi maisha mazuri ambayo hayana hukumu na dhambi...wala mauti.

Najua..unafahamu...juu ya dhambi..na uasi..kuwepo hapa..duniani...na namna ambavyo uasi huu ulikuja hapa duniani...
Na baada ya miaka mingi sana kupita..na mwanadamu akazidi kutenda dhambi...na kuzidi..kuwa mbali na Mungu..maana dhambi ilimfanya..mtu awe mbali na Mungu...yaani muumba wa mbingu..na nchi na aliye tuumba sisi wanadamu..na ambaye..yeye ndiye mwenye jukumu la kulinda uhai wetu..na ndiye..awezae kutusaidia kila kitu..na uhitaji..wetu..na ndiye..anaye weza kuweka..mifumo ya maisha na mafanikio...yetu..ya kila siku..
Pamoja na dhambi kututenga na Mungu..lakini pia iliharibu..mfumo mzima wa maisha ya mwanadamu...maana..hapo mwanzo kabla ya dhambi mwanadamu alikuwa amewekewa mfumo rahisi..na ambao ulikuwa ni mwepesi sana..kuuishi..na kumfanikisha..mwanadamu..mfumo ambao haukuwa na masharti mengi..na ni.mfumo ambao haukuhitaji mtu atoe jasho..au ahangaike ndipo apate..chakula..na ridhiki..alizo kuwa anahitaji...
Kitendo cha mfumo kubadilika Mungu alikiita laana..na maisha ya mifumo hiyo hata leo..tunasema ni maisha..ya laana..au maisha ya dhambi..au maisha ya utumwa wa dhambi..au maisha ya giza...(ufalme wa giza).

ukisoma mwanzo 1:28-31..utaona Mungu anawakabidhi dunia..adamu na hawa..
na mstari 29 biblia inasema *Mungu akasema,Tazama,nimewapa kila mche utoao mbegu,ulio juu ya uso wa nchi yote pia,na kila mti,ambao matunda yake yana mbegu;vitakuwa ndivyo chakula chenu.*

Lakini maisha baada ya hawa wanadamu kuto kutambua gharama za kwenda kinyume na kile Mu.gu anasema..wakaamua..kuasi kwa kumsikiliza nyoka..
Mwanzo 3:1-19..lakini tuoni huu kwa haraka 17 *Akamwambia Adamu,Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako,ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza,nikisema,Usiyale,ardhi imelaaniwa kwa ajili yako;kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako*  angalia huo mfumo wa maisha katika kipengele cha kupata chakula...mwanzo walipewa tu..wakawa wanakula pasipo uchungu...na mara hii wanapewa kula kwa uchungu..ili wale lazima kwanza wapate uchungu...

Maisha haya ya dhambi yalizidi kuwa mabaya siku hadi siku...na hata ikafika kipindi cha Nuhu..Mungu akawaangamiza watu wote..lakini bado aridhi..ilikuwa imebeba ile laana ya tangu adamu..tena uchungu wa maisha ukaendelea tena..na hii biblia ikasema..dhambi bado inawatawala wanadamu...Mungu akatengeneza..mpango maalumu wa kumwokoa..mwanadamu..
Mpango wa Mungu..aliazimia kutengeneza mbingu mpya zingini na dunia nyingine...ambayo katika hiyo..watu wataishi pasipo shida..na pasipo uchungu...na huko kutakuwa na furaha...daima..hiko hakutakuwa na njaa...wala taabu...na hii ndiyo...Yesrusalemu mpya...au Uzima wa milele..amabao..ndio kanisa..linautangaza..na Yesu Kristo alikuja kuutangaza..na kutengeneza njia..ili tuweze kupata neema na kibali cha kwenda kuishi..na Mungu..na tukaishi..na Mungu sikuzote..daima..
Mungu..akatengeneza kizazi cha mfano..kwa kumchagua..Ibrahimu...na akamfundisha...Ibrahimu...kumwani...Mungu..ibarahimu..akamwamini Mungu..na alipo fanikiwa..na kuhesabu iwe imani ya ibrahimu..kuwa yatosha..sana..kama kila mwanadamu atakuwa nayo hiyo..basi..itakuwa ni haki ya mwanadamu huyo kuhesabika kuwa anafaa sana katika ufalme..huo mpya..na katika nchi hiyo mpya..ambayo anaiandaa kwa ajili ya watakatifu...yaani watu walio stahiri..kuingia...na kuishi..kwa sababu ya kipimo cha imani...yao watakayo weka kwa Mungu wao...yeye aliye..mwandaaji wa hayo makao mapya..na mifumo mipya ya maisha..ya mwanadamu...
Hatua..iliyo fuata baada ya adamu kuwa tayari amefanika na kuhesabiwa haki na Mungu..ya kuwa ni mtu wa Imani..ikaja sasa mwanadamu alikuwa bado hajatambua dhambi ni nini..na ubaya..ni nini...japoaliishi katika uchungu..wa dhambi na laana ya dhambi..na mauti..

Sheria..ikawekwa..na Mungu..kuwa kama kiyoo cha kumonesha mwanadamu..kuwa
Dhambi ni mbaya
Mungu ni mtakatifu..na hachangamani na dhambi..
Na mwanadamu pasipo Mungu hawezi jambo lolote...hata kama ataoneshwa na njia..zote..na kila kitu..lakini..bado hana uwezo..wa kuishi pasipo Mungu...
Na hii utaiona..kwa kuisoma sheria..na kuona hakuna aliye weza kuitimiza siku zote..sheria..hiyo..zaidi sana walijikuta..sheria..anageuka..siku zote kuwahukumu wao..tu..
Jambo ambalo hata Yesu alipo kuja..akalieleza..lakini kuna watu hawakuelewa..wakazani..kuwa wanaweza kuyashika..na kuishi katika sheria..na kuishi kwa sheria..waokwama wao..jambo ambalo..limekuwa mzigo kwao..na kila siku wamekuwa watu..wa kujihukumu..na hata wanaposema wana-Yesu ndani yao lakini bado tu..wanajihukumu..kila siku..na mioyo yao..inawahukumu kwa sababu ya sheria..na mifumo waliyojiwekea..ya kuishika sheria..aliyo itoa Mungu..iwe kiyoo..wao wanaitegemea..kwa kuzani...wataweza..
Wengi jambo hili..wamelipokea..hivyo ni mapekeo..lakini wengine..ni kwasababu..hawajapata mafundisho ya kutosha..kuelezea..juu ya wokovu..na namna maisha ya wokovu..yanavyo..enda...hivyo...haitupasi kuwalaumu..wala haitupasi kujilaumu..na kujihukumu..au kunyosheana..vidole..juu ya swala hili..bali kwa upendo..yatupasa kkukaana kuturia..na kujifunza..kwa undani..hakika ya mambo haya..na kuanza..kuishi katika kweli..
Bwana Yesu Kristo..alisema hivi...mtaifahamu kweli..na hiyo kweli..itawaweka..huru..haikumaainisha..kuwekwa huru..na magonjwa..tu..
Bali..pia..alimaanisha..kuwekwa huru..mbali na dhambi...na kuwekwa huru..yaani hatutaendelea..tena kubaki..kuishi..kwa kufungwa na sheria...au kuhukumiwa..na sheria...zaidi sana..tutaishi..kwa uhuru..amani...furaha...pasipo mashaka ya kuogopa kufanya..jambo lolote..kwa maana..tayari tunafahamu..yatupasayo...yaani..kuishi..kwa kumtegemea yeye tu

Sasa..unaweza sema..mbona..unaongea..tu..kwa maneno yako.sisi..tutaaminije..?

Tuangalie..biblia...namna ambavyo inatueleza... Yohana..3:16 *Kwamaana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata kila amwaminiye asipotee bali awe na uzema wa milele..*.
Biblia..inasema kila AMWAMINIYE...shika hilo..ili likusaidie..huko mbele tunako elekea....

Yohana 17:1-3 *Maneno hayo aliyasema Yesu;akainua macho yake kuelekea mbinguni,akasema,Baba,saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao,ili Mwana wako naye akutukuze wewe..kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili..ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele...NA UZIMA WA MILELE NDIO HUU..WAKUJUE WEWE MUNGU WA PEKEE WA KWELI,NA YESU KRISTO ULIYEMTUMA*..
Lengo la Yesu Kristo..ni sisi kumjua..Mungu...na pia kumjua.. Yesu Kristo mwenyewe..yaani kwanini Yesu Kristo amekuja...na tukimjua...tutajua..nini cha kufanya...au cha kufuaata..au cha kutaka kutoka kwake.....

Efeso..4:11-15 *Naye alitoa wengine kuwa mitume,na wengine kuwa manabii..na wengine kuwa wainjikisti na wengine kuwa wachungaji na walimu...kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu,hata kazi ya huduma itendeke..hata mwili wa Kristo ujengwe....HATA NA SISI TUTAKAPOUFIKIA UMOJA WA IMANI NA KUMFAHAMU SANA MWANA WA MUNGU..HATA KUWA MTU KAMILIFU HATA KUFIKA KWENYE CHEO CHA KIMO CHA UTIMILIFU WA KRISTO..ili tusiwe tena watoto wachanga,tukitupwa huku na huku..na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu..kwa hila ya watu..kwa ujanja..tukizifuata njia za udanganyifu.*....
sasa naamini taratibu unaelewa japo kuwa sjafika sehemu..nijibu swali lako..ila naamini hata hapo..kuna kitu Mungu anakijenga katika ufahamu wako...
-Sasa..mtumishi..ubatizo wa maji unakazi gani..kama wokovu..ni kumjua..Mungu..tu...na kumjua..Yesu..Kristo...?
Jibu langu ni hili...ubatizo..wa maji ni dalili ya nje..tu ambayo inatoa ushahidi au ushuhuda ya kuwa kweli mtu huyu ameamua..na unatumiwa makanisani kulingana na taratibu za kanisa...ila mi sipo kuzungumzia hilo...naongela...kuokoka na kupata wokovu moyoni..mwako kwanza....

Kama unabisha...kasome habali za yule mtu..aliyeteswa pamoja na Yesu Kristo..ndo utaelewa...kilicho mwokoa yule..jamaa ni kumtambua Yesu Kristo kuwa..yeye hana dhambi..na pia..hakustahili..kuwa pale..msalabani..lakini pia..jamaa akatambua..kuwa Yesu Kristo anaufalime..na alikuwa pale..msalabani..kutengeneza njia ya kuingia katika ufalme..wako...na ukimwamini..na kumwomba..anaweza kukupa..nafasi..maana yeye..ndo anatoa tiketi..au haki..au naweza sema..yeye..ndo mlango wa kuingilia..kwenye huo ufalme...
Sasa nahisi utaelewa..kwanini jamaa...alifika mahali baada ya majibizano..akasema..Bwana nikumbuke..basi kwenye..huo ufalme..wako..na Yesu pasipo kuchelewa..wala kusita akasema hakika leo hii utakuwa na mimi peponi...
Sijui..sasa kama unaelewa..nini ambacho nakisema..hapa..ok..
Sawa...unaweza sema..sasa mtumishi..hiyo imani ya kuzalau hadi ubatizo..jambo ambalo hata Yesu Mwenyewe..alipitia..na sisis lazima..tupitie...hiyo haikwepeki...kuokoka..ni kubatizwa kwa maji..na ukisha batizwa kwa maji..basi..ndo..umeokoka..

Sikia..mtu wa Mungu..ukubali ukatae..sawa tu..ila na kesho.mi nitaendelea..kufundisha..na watakao amini...wataokoka..ila ukigoma mimi..nimesha nawa...
KAMA HAUJAMJUA YESU KRISTO  NA KUMUAMINI KUWA NI BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO MOYONI MWAKO HATA TUKIKUBATIZA HAUNA UZIMA WA MILELE...LABDA TUKUBATIZE..KAMA ISHAYA YA NJE HALAFU TUKUFUNDISHE..ILI UJUE NA KUFAHAMU..YESU NI NANI..
HIVYO MBINGUNI HATUENDI KWA KUFANYA ISHARA ZA NJE...YAANI UBATIZO .NA KUHUDHURIA KANISANI NA KUFUATA MATENDO YA SHERIA...
MBINGUNI TUNAENDA KWA KUIFAHAMU KWELI...NA KUMJUA MUNGU..NA MIPANGI YAKE MUNGU JUJ YETU...NA KWA KUMJUA YESU KRISTO YA KUWA YEYE NDO NJIA PEKEE YA KUTUINGIZA KATIKA UZIMA HUO WA MILELE WA MBINGUNI..NA KWA KUTAMBUA YEYE NDIYE ANAWEZA KUTUFANYA TUKAFANANA NA APENDAVYO...KWA JUHUDI ZETU PEKE YETU HATUWEZI...
Luka 3:16 *Yohana akawajibu akawambia wote..mimi kweli nawabatiza kwa maji...lakini yuaja mtu mwenye nguvu..kuliko mimi ambaye..mimi sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake..YEYE ATAWABATIZA KWA ROHO MTAKATIFU..NA KWA MOTO...*
Pia..soma na hapa
Yohana 15:26 *Lakini ajapo huyo Msaidizi..nitakayewapelekea kutoka kwa Baba..huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba..yeye atanishuhudia.*...
Sasa..kama..unataka kujua..hicho unacho amini..angalia
Je..Roho mtakatifu..amekupa...Amani..juu ya wokovu wako....?
Je!haujihukumu tena...?
Je!unauhakika..wa kuingia mbinguni...Yesu akija leo...?.
Kama hauna huo ukika..angalia...sana imani...iliujaza..moyo wako..na hayo mashaka yanatoka wapi...?.
Sina maana..mafundisho uliyo nayo ni yauongo..bali...hujayaelewa sawasawa...lakini pia..huenda..hayajakamilika..kiasi cha kuweza kukupa..ufahamu..huu ambao..nimekupa..wewe leo..ya kuwa...wokovu..ni ndani..ya moyo...na ni hakika..kabisa..moyoni..juu ya Yesu Kristo..
Warumi...
10:8-11 *Lakini.yanenaje? Lile neno li karibu nawe,katika kinywa chako..na katika moyo wako..yaani lile neno la imani..tulihubirilo..9 kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa cahako ya kuwa ni Bwana,na kuamini moyoni mwako ya kuwa  ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu..utaokoka. 10 KWA MAANA KWA MOYO MTU HUAMINI HATA KUPATA HAKI..NA KWA KINYWA HUKIRI HATA KUPATA WOKOVU...11 kwa maana andiko lanena.Kila amwaminiye hata tahayarika.*..
Sasa..angalia huo mstari wa katika kitabu cha warumi...na kile..alicho kifanya..yule..mnyang'anyi...aliye teswa pamoja..na Yesu pale..msalabani...hivyo..utagundua..jambo ambalo...nimekwambia..ya kuwa wokovu..siyo kwa matendo ya sheria..bali..ni NEEMA TU..kwa njia..ya KUAMINI...UKWELI JUU YA MUNGU NA JUU YA YESU KRISTO...

-Lakini..pia naomba ufahamu...hivi..sisi ndani ya Yesu tunaokolewa kwa NEEMA tu siyo kwa sababu ya matendo yetu...na kama ulikuwa unaogopa..kwa sababu..ya matendo..au unajiona hauwezi kuokoka kwa sababu haujui na haujaweza kutenda matendo mema...sikia hii itakusaidia...wewe mwamini Yesu...yeye ndo atakufundisha...kutenda mema..na kuacha dhambi ukiwa tayari...umekwisha kumwamini...
-Kwa sababu ukimwamini huyu Yesu Kristo unapokea NEEMA ya wokovu na kuokoka...na hii neema..ndiyo itakusaidia..na kukufundisha vizuri hatua kwa hatua..kuweza kuishi...na kushinda dhambi.....

Tito 2:11-13 "Maana neema ya Mungu iwaokowayo wanadamu wote imefunuliwa..nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi,na haki,na utauwa,katika ulimwengu huu wa sasa; tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu,Mungu mkuu na Mwokozi wetu.."

-Hakuna mwanadamu yeyote..anaye weza kuishinda dhambi...wote hatuwezi...bali Yesu Kristo alikuja ili atushindie dhambi..na kutufanya sisi washindi..na watakatifu wa Mungu...

Wagalatia 4:3-7 *Kadhalika na sisi,tulipokuwa watoto,tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia...Hata  ulipowadia utimilifu wa wakati,Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke,amezaliwa chini ya sheria...kusudi awakomboe hai waliokuwa chini ya sheria..ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana...Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana,Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu,aliye,Aba,yaani,Baba....Kama ni hivyo..wewe si mtumwa tena..bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu..."

UNASUBIRI NINI NDIPO UAMUE KUOKOKA..!!!?
AMUA KUOKOKA LEO NA UWE NA UZIMA WA MILELE TANGU LEO..

KUOKOKA NI HAKI YA KILA MTU NA NINJIA PEKEE YA KUKUWEZESHA KUISHI NA BWANA..NA KUWEKABMAISHA YAKO SALAMA..

YESU KRISTO ATAKUJA WAKATI WOWOTE TUSIOUJUA WALA KUUDHANIA

USIANGALIE NDUGU WATAKUONAJE...
AU DINI YAKO NA DHEHEBU LAKO WATAKUONAJE...MAANA HAO HAWATA KUSAIDIA CHOCHOTE MBELE ZA MUNGU SIKU ILE YA HUKUMU....

Kwa  msaada zaidi..wasiliana nami,
Naitwa Elisha Ndumizi
0654501879.

Comments

Popular posts from this blog

UWEZA WA MUNGU JUU YA MAGONJWA NA VYANZO VYAKE

UMUHIMU WA IBADA

IJUE IBADA-SEHEMU YA KWANZA