UFAHAMU JUU YA DHAMBI NA LAANA
Bwana YESU KRISTO asalifiwe sana...mpendwa ...
Karibu sana...tujifunze..pamoja..neno la Bwana
Wagalatia 3:7-10 "Fahamini basi, ya kuwa wale walio wa imani,hao ndio wana wa Ibarahimu...Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani,kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa....Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani....Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria,wako chini ya laana; maana imeandikwa,Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati,ayafanye...".
-Lengo la somo hili..ni.kukuongezea...na kuimarisha imani yako kwa Yesu Kristo..
-Pia kumwezesha mtu yeyote ambae hajamwamini Yesu Kristo aweze kumjua..na kumwamini..ili akapate kuishi milele..
-Dhambi...ni nini...?
-Laana ni nini?
DHAMBI
-Dhambi ni uasi...yaani kwenda kinyume na sheria au utaratibu ulioweka...ni kwenda kinyume na makubariano....
-Pia dhambi ni kitendo chochote..ambacho si cha haki au kinacho mnyima haki mtu anaye tenda/tendewa...au kinacho tendwa kinyume na misingi ya haki ya jamii nzima kwa ujumla....
1 yohana 3:4 *Kila atendaye dhambi,afanya uasi;kwa kuwa dhambi ni uasi..*
Kwahiyo dhambi...ni uasi..yaani kinyume na makunariano au mapatano...
Lakini..pia 1yohana 5:17 * Kila lisilo la haki ni dhambi..na dhambi iko isiyo ya mauti..*
LAANA NI NINI....?
-Laana ni adhabu...inayo tokelewa au inayo takea...kwa mtu yeyote...anaye tenda dhambi...
LAANA =MATOKEO YA DHAMBI.
~Pia laana..ni..matokeo...na matukio yanayo kuja na mifumo mbalimbali ya namna ya kuendesha maisha...baada ya dhambi kutendeka...
Mwanzo 3:1-19 ni habari za hawa na adamu..jinsi walivyo muasi Mungu..na kwa huo ndio mwanzo wa mtengano wa mtu na Mungu...ukisoma mstari wa 14...17..neno linasema *14 BWANA Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani walioko mwituni;kwa tumbo utakwenda,na mavumbi utakuka siku zote za maisha yako..17 Akamwambia Adamu,Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako,ukala matunda ya mtu ambao nalikuagiza,nikisema,Usiyale;aridhi imelaaniwa kwa ajili yako;kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako..*
~Kwa lugha rahisi naweza sema...laana..ni kukosa msaada wa karibu na uangalizi ...na Mungu...katika maisha..
Laana ni kuonfolewa katika mfumo..wa maisha ulio kuwepo mwanza...na kupewa au kuingia katika mfumo mwingine wa maisha ulio mgumu na ambao mafanikio yake hayaji kiurahisi....maana ndani yake..kunakuwa na mateso....
Laana ni adhabu.....
~Maana nyingine... Laana ni apizo alitoalo mtu kwa mtu mwingine ili afikwe na mabaya?
~mathayo 25:41
*Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto...Ondikeni kwangu, mliolaaniwa,mwende katika moto wamilele,aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake*
-Pamoja na kuwa laana ni adhabu...lakini pia laana bado inamfanya mtu aendelee kupata adhabu zingine..au watu waendelee kuoata adhabu..kwa sababu ya laana..iliyo letwa kwao...adhabu huwa nyingi zaidi...maana wanakuwa wamepoteza haki...ya msingi ya kutunzwa...kutetewa..ama kuhudumiwa au kupatiwa..kile wanachotaka...moja kati ya adhu nyingine..ni kuhukumiwe kwenda kwenye moto wa adhabu milele..
-Katika maisha ya kila siku..zipo njia..nyingi sana za mtu kupata laana...
~Laana kwa njia ya maneno ya watu....watu wanakutamkia maneno juu yako wewe..ili ukose msaada au upatwe na shida kiasi ambacho hali hiyo iwe ni adhabu kwako
~Laana kwa njia ya matendo...hapa wanakufanyia...vitendo vinavyo ashiria laana juu yako
~Laana kwa sababu ya hali ya chuki na kutokuelewana na watu wanao kuzunguka...jambo hii pia huleta laana hasa mtu akichukia akatamaka maneno..mabaya juu yako au juu ya aridhi hiyo..kwa sababu amekosa haki yake...
~Laana kwa sababu..ya kufunua au kufununiliwa uchi au utupu wa mzazi wako....uputu..wa mwanadamu..huachulia laana kubwa sana tu..maana huharibu akiri..za mtu kabisa...
Na ndiyo maana..ukimkorofisha mzazi...utasikia..nitakuvulia..nguo wewe...???
Lakini...njia kuu na ambayo laana zake huwa ni kubwa sana...ni kumwacha Mungu
~kumbukumbu ka torati 30:17-20
*Lakini moyo wako ukikengeuka,usipotaka kusikiza,lakini ukavutwa kando kwenda kuabudu miungu mingine,na kuitumikia....nawahubiri hivi leo hakika mtaangamia...hata matazifanya siku zenu kuwa nyingi jui ya...uivukiayo Yordani uingie kuimiliki....19..Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo...kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti....baraka na laana...basi chagua uzima..ili uwe hai wewe na uzao wako....kumpenda BWANA,Mungu wako,kuitii sauti yake...na KUSHIKAMANA naye;kwani hiyo ndiyo uzima wako,na wingi wa siku zako....upate kukaa katika nchi BWANA aliyo waapia baba zako...Ibrahimu...na Isaka...na Yakobo...kuwa atawapa...
~Laana haina dawa...wala laana haina mbadara...wake..ukilaaniwa umelaaniwa tu...mpaka aliye kulaani atamke msamaha..na baraka ili kuweza kukupa angalau furaha...juu ya hiyo adhabu...uliyo pata....
~DAWA YA LAANA NI MSAMAHA KUTOKA KWA YULE TU KWA YULE ULIYE MTENDA DHAMBI.
3:13-14 '' KRISTO alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti; ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika YESU KRISTO, tupate kupokea ahadi ya ROHO kwa njia ya imani."...
~Lakini pamoja na kwamba...watu wengine...wanaweza wakalaani..MUNGU yeye anaweza futa laana za mtu kwa mtu yeyote wakati wowote...kama tu..ukimpokea...na kumwamini... Yeye awe msaada na mwangalizi wa maisha yako..
~ Wagalatia 3:26-29 '' Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa MUNGU kwa njia ya imani katika KRISTO YESU . Maana ninyi nyote mliobatizwa katika KRISTO mmemvaa KRISTO. Hapana Myahudi wala Myunani.Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika KRISTO. Na kama ninyi ni wa KRISTO, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi...
~Kumb 28:20 '' BWANA atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo.''
~ Laana za wanadamu au majini au wakuu wa giza haziwezi kumfanya mtu asiende uzima wa milele kama huyu mtu ataamua kujikabidhi kwa Mungu na kutaka ulinzi wa Mungu...
~Lakini laana kwa sababu ya kujitenda na MUNGU inaweza kumfanya mtu asiende uzima wa milele.
NGUVU YA NENO
Yohana 1:1,14...
*1 Hapo mwanzo palikuwapo Neno...naye Neno alikuwako kwa kwa Mungu...naye Neno alikuwa Mungu.....14 Naye Neno alifanyika mwili,akakaa kwetu nasi tukauona utukufu wake,utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba;amejaa neema na kweli..."
~Neno...ni Yesu Kristo...na ndiyo maana toka mwanzo nimekuwa nakupa...mistari...unaona kazi ambayo...Yesu Kristo anaifanya....palipo na laana na dhambi...Yesu akiingia...anasafisha...anaweka baraka...amani..uzima...na mafanikio
~Haijarishi..laana ni yaaina gani...ila Yesu Kristo anao uwezo juu ya yote...yeye...anavunja...na kufuta...na..kutengeneza..na kusawazisha..kila jambo likawa sawasawa....
~Tumeona baada dhambi kuingia...laana ilitokea...na kwa ujumla...adhabu yote ikaleta mauti...kwa mwanadamu...ambaye alipoteza na amepoteza uhusiano na Mungu...wake...
~Kumbu 28:20... "BWANA atakuletea laana na mashaka,na kukemewa...katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya...hata uangamie na kuotea kwa upesi;kwa ule uovu wa matendo yako...uliyoniacha kwayo..."
~Ona...maisha ya laana yana dalili hizo hapo juu...
-kwanza kutakuwa na mikosi...tu..
-Pia..kutakuwa na mashaka...kila siku wewe utakuwa ni myu usiye pata..amani..moyoni mwako...uoga na wasiwasi vinatawala...
-Utajikuta...kila jambo unalofanya..unakosea...tu...na watu wanakukemea...tu...kama ndo unaajira utajikuta kika ajila unayo pata...unagukuzwa...tu..
-Kama ni..biashara..unajikuta..haziendi...na unafirisika...tu..
~Lakini...Neno akiingia kazini...ukimpokea..Neno...yaani huyu Yesu Kristo...anashughurikia...kila...kitu...we mwite..tu..na umwambie...Yesu..naona kuna..laana..kwehi..hii sehemu...naomba..uwe mwangalizi..wangu..maana mimi..siwezi..lakini..wewe BWANA wangu..na Mungu wangu unaweza..
~BAADHI YA MADHARA YA RAANA
Warumi 5:14 "walakini mauti ilitawala tangu adamu mpaka Musa..nayo ilitawala hata wao wasioifanywa dhambi ifananayo na kosa la Adamu..aliye mfano wake yeye atakayekuja..
>Dhambi na laana zilileta nauti na mauti ikatawala..na mbaya zaidi ikatawala hata ambao hawatendi dhambi...ifananayo na ile ya Adamu..
~Kumb 28:15-68
Hapo kuna madhara mengi..sana yameandikwa...
>Laana inakufanya aridhi ikukatae..kila unako enda iwe mjini au kijijini...ni shida na mikosi tu..
>Laana inafunga njia..za uchumi..wako..na huwezi fanikiwa..
>Laana inafatilia...kizazi baada ya kizazi...yaani utakuta matatizo ya kuridhi..ni..mengi sana..na yanakuwa hadi kelo kwa familia..na ukoo mzima..
>Laana inaweza fanya..haya mke wako/mume wako akaanza kuchepuka au kutoka nje ya ndoa...na kulala na watu wengine...(kumb28:30).
>Kumb 28:18 ''Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. ''
4. Kwa kosa la kumkosea MUNGU basi mtu huyo atakuwa mtu wa kuwa na mashaka mashaka, hukemewa, Kudhalilishwa na kutishwa bila kosa kwa sababu ya laana aliyonayo. Kumbu 28:19-20 '' Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo, BWANA atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo.''
5. Kwa Kumkosea MUNGU basi Laana yake inaweza kutengeneza magonjwa mabaya. Kumbu 28:22 ''BWANA atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie.'' \
6. Kufungwa kwa baraka kutoka kwa MUNGU. Kumb 28:23 ''Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma.''
7. Kwa kumkosea MUNGU basi Mazuri anayoyatarajia yatageuka kuwa mabaya Kumbu 28:24 '' BWANA atafanya mvua ya nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako kutoka mbinguni hata uangamie.''
8. Kwa Kumkosea MUNGU basi Adui kwenye ulimwengu wa roho watampiga. Kumbu 28:25 '' BWANA atakufanya upigwe mbele ya adui zako; utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini utakimbia mbele yao kwa njia saba; nawe utatupwa huko na huko katika falme zote za duniani.''
9. Atakuwa mtu wa kuonewa. Kumb 28:29 '' utakwenda kwa kupapasa-papasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.''
10. Kupata Hasara zisizoisha. Kumb 28:38-39 '' Mbegu nyingi utazichukua nje shambani, lakini utavuna haba, kwa kuwa nzige watazila. Utapanda mizabibu na kuitengeza, wala hutakunywa katika divai yake, wala kuichuma kwani italiwa na mabuu.''
11. Wageni au watu wapya wakija wanafanikiwa lakini yeye yuko pale pale, Pia atateswa na madeni Kumb 28:43-44 '' Mgeni aliye kati yako atazidi kupaa juu yako; nawe utazidi kushuka chini.Yeye atakukopesha, wala wewe usimkopeshe; yeye atakuwa ni kichwa, wewe utakuwa mkia. ''
12. Akipata mali au pesa wanatokea walaji ili asifanye chochote cha kimaendeleo. Kumb 28:50-51 ''taifa lenye uso mkali, ambalo haliangalii uso wa mzee, wala halipendelei kijana; naye atakula uzao wa ng'ombe wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako mpaka utakapokwisha kuangamizwa;''
Hizi ni alama chache tu za mtu anayesumbuliwa na laana.
~Ndugu yangu ni muhimu kujua kwamba damu ya YESU inaweza kufuta laana zote lakini ni mpaka uombe na sio kujifariji tu.
Kanuni ya laana ni kwamba mkubwa anamlaani mdogo hivyo na kuondoka laana kunahitajika nguvu kubwa kuliko mtoa laana wa kidunia ndipo laana hiyo itafutika.
~ Kama laana imetoka kwa MUNGU basi dawa ni kutubu tu kwa MUNGU na kutengeneza njia zako kwa kuanza kutenda yale ayatayo MUNGU.
YESU KRISTO ana uwezo wa kukuweka huru kweli kweli mbali na laana, lakini hadi uamue wewe kuwekwa huru.
Yohana 8:36 '' Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.''
Yakobo 3:9-10 ''Kwa huo(Ulimi) twamhimidi MUNGU Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa MUNGU. Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo"
Ndugu..yangu yapo mambo mengi sana ambayo...tutaangalia...Siku nyingine...lakini...zingatia..sana jambo hili ya kuwa Yesu anaweza mambo yote...
-Usiishie kufadhaika tu...na kuhangaishwa na dhambi...na laana...
Hiyo haita saidia...kabisa...bali..fanya maamuzi leo...na dumu katika maamuzi hayo....
MPOKEE YESU KRISTO AWE BWANA NA MWOKOZI WAKO...MKABIDHI YESU MAISHA YAKO NA JIKABIDHI KWAKE...YEYE AWE MWANGAKIZI...MSIMALIMIZI..NA MUNGU WAKO....
HAKIKA LAANA NA DHAMBI WALA MAUTI HAVITA KUTISHA TENA NA KUKUANDAMA...BALI UTAKUWA HURU DAIMA..
MUNGU AKUBARIKI SANA
Kwa msaada zaidi..na mawasiliano...
Naitwa Elisha Ndumizi
0654501879
ALL MIGHT GOD bless you with this wisdom shared to us
ReplyDelete