NDOA NA MAHUSIANO
Bwana Yesu Kristo asifiwe sana....
Mpendwa karibu sana katika mwenfelezo wa somo letu....
Nataka tuendelee na somo..letu la leo..kumbuka tunajifunza..MAHUSIANO NA NDOA...na baade nataka tuje kuona namna ya kutambua chaguo lako sahihi...lakini pia namna ya kuweza kudumu na huyo mke/mume uliye naye...endelea kuomba..Mungu azidi kutupa hekima...na maarifa zaidi kiweza kukupa kitu kitakacho kusaidia na kukuwezesha kufanikiwa na kuwa na Mahusiano mazuri na ndoa nzuri
~Niukweli usio pingika kila mtu anahitaji mke mwema...au mume mwema...na biblia..inasema mke/mume mwema atoka kwa Bwana...lakini kuna namna...ya kuweza pia kugundua kuwa huyu...ni special kweli kutoka kwa Bwana
Sasa kwa wale ambao bado hamjaoa au kuolewa...nataka nikupe sifa kadhaa hapa ambazo ztakusaidia...
MUME MWEMA KWAKO EWE BINTI
~Awe mcha Mungu
~Anaonyesha kukujali na kukuheshimu
~Anaonyesha kuwa wewe ndiyo chaguo lake na anautulivu na huo upendo anakujali
~Anamipango ya maendeleo ya baadae kuhusu maisha
~Anaonyesha uwajibikaji...?
Je!anaweza kuwa baba na anaweza kukuwajibisha? Na kuwa na misimamo kama mume...?
~Anaweza kuomba msamaha...?
UKIONA BAADHI YA YAFUATAYO JUA NI KIMEO A.K.A BOMU
~Anaomba tendo la ndoa kabla ya ndoa
~Hataki kufanya kazi
~Hajishughulishi na mambo ya Mungu
~Anategemea wazazi kwa kila kitu kupita kiasi..(hawez hata jisimamia mwenyewe)
~Awe anapenda wazazi wake..na pia awapende na wazazi wako
MKE MWEMA KWAKO MKAKA
~Mcha Mungu
~Anatabia za umama..?? ~Anaonyesha kweli.anaweza kuwa mama wa watoto..?
~Anaonyesha kukukubali kuwa wewe ndo mume..?
~Ujue nini vipaumbele vyake..nae lazima ajue vipaumbele vyako...
~Msafi..? (heshima...adabu na ustaha wa nguo na ni mkarimu?..)
~Anajishughutisha kuingiza kipato...?
~Je!anafaa kwa ajili ya maono yako...uliyo nayo...?au ndo anakuja kuyamaliza kabisa na kuyazika...?
UKIONA YAFUATAYO JUA NI KIMEO AU BOMU HUYU
~Ukiona hajishughurishi na Mungu huyo mkimbie..Anataka au anatoa..tendo la ndoa kabla ya ndoa
~Ana lugha ngumu...?hakujari...? ~Hakuheshimu...?
~Mzembe...?
~Hawezi kuomba msamaha...
~Anakufananisha na wanaume wengine...?
~Hajishughulishi na kuingiza kipato...?
Methali..31: 1-31...lakini.mimi nitakupa sehemu tu...kuanzia mstari wa 10 *Mke mwema ni nani awezaye kumwona...?maana kima chake chapita kima cha marijani
MOYO WA MUMEWE HUMWAMINI...wala hatakosa kupata mapato....Humtendea mema wala si mabaya..siku zote za maisha yake...Hutafuta sufu na kitani...Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo...Tena huamka kabla haujaisha usiku..huwapa watu wa nyumbani mwake chakula..na wajakazi wake sehemu
Ebu tuangalie biblia inasemaje Wimbo ulio bora 2:1-4 *Mimi ni ua la uwandani,ni nyinyoro ya mabondeni...kama nyinyoro kati ya miiba..kadhalika mpenzi wangu kati ya binti..kama mpera kati ya miti ya msituni...kadhalika mpendwa wangu kati ya vijana...niliketi kivulini mwake kwa furaha..na matunda yake naliyainja kuwa matamu....akanileta mpaka nyumba ya karamu...na pendera yake juu yangu ni mapenzi...
Natumaini sasa baada y mistari hiyo na point nilizo tangulia kukupa..tunaweza endelea
Sasa mtumishi...ni wakatigani sahihi.. wa kuoa..au kuolewa...?
Wakati sahihi ni wakati ambao unakuwa na uhitaji kabisa na kuthamilia kuwa sasa ni nahitaji kuwa namke au mume..?
Kisheria ni kuanzia miaka 18
Ki umila...ni pale ambapo mtoto anaweza kuwa na uwezo wa kujitegemea..na kufanya maamuzi..
Ukisoma biblia..Mungu aliwaumba mwanamke na mwanaume siku moja...lakini.alimdhihirisha mwanaume kwanza na baadae ndipo mwanamke...tena hakumdhihirisha mwanamke kwa kuwa alitaka...kumdhihirisha...ila hadi alipo ona sasa adamu anahitaji mwanamke ndipo alimletea mke...
Yusufu...alipo kuwa utumwani...alipo pewa kazi ya kufanya kazi ambayo ilikuwa ndo imebeba maono...yake...ndo alipatiwa mke...Musa..alipo pata kazi...kuwa sasa atakuwa anachunga ndo alipewa mke akamwoa...
Asa hiyo inatupa kuona kuwa kwanza tambua kazi...au tambua..kuwa sasa unaishi katikamaono yako...au upo katika uhitaji kabisa wa kuoa au kuolewa...usikulupuke..tu kisa wenzako wameolewa au wameoa..nawewe ukasema..sasa namimi..bora niolewe......
Mtumishi...sasa nitamjuaje..kuwa huyu ndo ananifaa...na.ndo sahihi.kwangu...wa kuolewa...nae au wa kumwoa...?
Zipo njia nyingi tu za kumpata...mke au mume ambae ni.mwema au mzuri na sahihi kwako...
samahani.kwa...wale ambao mpo kwenye ndoa..tayari..nitakuja na nyie upande wenu...
Njia sahihi...inategemeana na mfumo.wa malezi na maisha jinsi unavyo yaendesha...
Pia inategemeana...muda wa kutaka kukamilisha hatua zote hadi..kuofunda ndoa...
Biblia inasema...mke mwema anatoka kwa BWANA..sasa njia zote tutakazo angalia...na kwa kuwa tunaongelea mke/mume mwema..ambae atatengeneza ndoa..bora..siyo ilimradi ndoa..tu..bari ndoa bora na nzuri na yenye afya...NJIA MOJA WAPO NI.KUWATUMIA WAZAZI...
~Wazazi au walezi...au wachungaji.na walimu wako.wa kiroho wanaweza kuwa msaada sana wa wewe kuweza kumpata mwanamke sahihi..au..mume sahihi..
~Njia hii ilikuwa inatumika toka zamani...lakini kwa sasa watu wengi hawaitumii njia hii lakini..bado inafaa na ni nzuri...kama wewe mwenyewe utaamua kuwashirikisha wazazi au walezi au mchungaji wako..ukasema.mimi nahivi nataka kupata ndoa..naomba mnichagulie anae nifaa...
~Sasa watamjuaje...kama wanakujua..wewe na wanajua tabia zako sawasawa...watakuwapatia..mtu sahihi na ambae utaendana nae....
~Ibrahimu...alitamfutia mwanawe..Isaka...mke..na bahati nzuri zaidi yule mfanyakazi ndo alienda kutafuta mke kwa ajili ya isaka kwa ruhusa ya Ibrahimu...lakini..nyuma yake Mungu alitangulia na Mungu ndo alisimamia zoezi zima...hadi isaka anapata mke
~Njia nyingine..ni kupitia...maono au kuambiwa na Mungu moja kwa moja..
~Njia nyingine..ni kutafuta wewe mwenyewe...lakini njia hii itapimwa na Amani...ya Mungu ndani yako...
~Njia nyingine ni kutumia washenga..
~Sasa..namna ya kupata..mke nahisi unazijua..na zipo nyingisana... Sana..lakini lazima matokeo yake na usahihi wake upimwe na neno la Mungu...na Ukisha pima Amani...ya Mungu itaamua ndani yako...hautakuwa na shaka..na huyo mtu...
~Maana moyo waweza mpenda mtu..lakini akawa siyo sahihi kwako..kabisa...na ukimpiama huyo mtu na kumwingiza kwenye mizani na viwango vyo biblia...biblia...itakuonesha kuwa huyo siyo sahihi...kwako..
Na ukisha jua kweli..gafla utashangaa moyo hata kama ulikuwa unampenda kiasi gani...ule upendo unapotea..kabisa...
~ Hivyo ndo maana ni muhimu sana kumsikiriza Mungu..na kujifunza Mungu anasemaje..juu ya kuoa na kuolewa...na ukijua..utakuwa..na hali nzuri na nafasi nzuri sana ya kufanya maamuzi sahihi..sana na pia..ambayo yatakupa kuishi maisha ya ndoa kwa furaha na amani kubwa kiasi hujawahi kuona...
~ Asante..sana...kwa wale wote ambao mnatuma maswali inbox...naomba mengine niyajibu hapa..ili.wengi wapate kupokea sawasawa na uhitaji wao...
~Mtumishi asante kwa somo..ubarikiwe sana...najifunza mengi..na somo linanisaidia sana...
Samahani..naomba uneelezee dalili ambazo naweza zitumia..au ziona ili kudhibitisha kuwa sasa huyu mchumba niliye naye anafaa...
Asante kwa swali...zuri sana...
~Zipo dalili za nje na dalili za ndani...
~Dalili za nje..ni pamoja na tabia..au haiba ya mtu..huyo inaendana na wewe au inakufaidia..sana na kukupendeza... Pia zile sifa ambazo nilizitaja hapo juu...
~Dalili za ndani...ni
KULIDHIKA NA UPENDO KWA HUYO MUTU...AU YEYE KULIDHIKA NA UPENDO WAKO...
+Methali..31: 11 *moyo wa mumewe humwamini sana...*
Methali 5:19 *Ni ayala apendaye napaa apendezaye..Maziwa yake yakutoshe sikuzote..na kwa upendo wake ushangilie daima*
ATAKUWA NI WATOFAUTI SANA NA WATU WENGINE..YAANI NJIA ZAKE NA JINSI UNAVYO MWONA MOYONI.MWAKO..HUWEZI MFANANISHA NA WANAUME WENGINE AU WANAWAKE WENGINE..UTAMWONA NA ROHONI UTAKUWA NA AMANI KWA KUSEMA HAKIKA HUYU NDIYE...
wimbo ulio bora 2:3 *kama mpera kati miti ya msituni..kadhalika mpendwa wangu kati ya vijana...Niliketi kivulini mwake kwa furaha..na matunda yake naliyaonja kiwa matamu*
Amani ya BWANA itakuwa inatawala ndani..yako...
Neno lina sema hivi... *na Amani ya Bwana ipitayo fahamu zote..iwalindi na kuhifadhi nia zenu na hiyo mioyo yenu...* pia linasema... *na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu*
~[Pia atakuwa tayari kuachana na watu wengine wote..alio kuwa nao..na kukudhibitishia...kuwa sasa wewe ndo chaguo sahihi.....~kama ni wewe..utakuwa na Amani.ya kuamua kuachana na watu wengine wote...na kubaki na huyo mmoja tu...pasipo shaka..na maumivu moyoni....
[Mtumishi...swali langu...ni...hivi mimi ninamtu ananipenda.ila sasa anamwanamke mwingine..ambae ameanza nae mapenzi siku nyingi...sasa kila nikimwambia..vipi atanioa...? Anasema nisubiri kwanza..kama ikitokea..akaachana na yule wa kwanza..ndo tutaoana..kwani kwa sasa hawezi mwambia...hampendi..maana anadai anaogopa kumuumiza...
Jibu...ni...hili huyo mtu..si sahihi kwako...maana tayari yupo na mtu mwingine..
kumbuka biblia inasema ukizini na mtu..nafsi yako inaambatana na huyo mtu..pia..mnapo oana..nafsi huungana na kuwa mwili mmoja...sasa kama ikitokea...nafsi tatu zikaungana...ni shida..na..ndoa haiwezi kusimama... Kama anataka.ajitoe kwanza kwenye agano na huyo wa kwanza na aweke agano.na wewe...
Pia..hadi hapo...japokuwa unampenda upendo wako haujafika sehemu akuone kuwa ni wewe ndo chaguo sahihi..na moyo wake upo kwa mtu mwingine...hakufai huyo..
Na je sasa ikitokea hawajaachana..wewe utakuwa fungu gani...hivyo..achana nae mapema..
Achana nae..na mwombe Mungu.akusaidie..kuweza kuchukua hatua hiyo..maana inaweza ikawa nk ngumu..kwako..lakini..kwa ufupi..si sehemu sahihi kwako..Tumia Damu ya Yesu kuisafisha na kuitenga nafsi yako na huyo mtu..kumbuka damu ya Yesu inafuta maagano dhaifu..na pia inatengeneza agano...imara...
[But sometime kuacha njia ile uliyopo huwa nivigumu sana even if u try to play... Inahitaji kujitoa na maamuzi magumu sana
[ Mtumishi..mimi...nashukuru kwa somo hili..nabarikiwa na kutiwa fataja sana..
Naomba ushauri..Mume wangu..nilikuwa nampenda sana...na tulipendana..lakini..kwa sasa hanipendi...na anafanya biashara..wala hanishirikishi...anaishia..tu kununua unga na mboga basi..lakini.hanipi hela za matumizi..na wala maelewano ndani ya nyumba hayapo...kabisa nifanyaje...? ]
~Hakuna kitu kibaya sana kama...kujua kitu furahini ni kibaya na ukawa unashindwa...kukiacha ..njia nzuri ya kukiacha ni kujifunza...zaidi..lakino Mungu ndo njia tosha na ya pekee kukuwezesha...
Fikilia..kwa habari ya dhambi...mtua kwa nguvu zake hawezi acha dhambi...ila kwa msaada wa Mungu katika Kristo Yesu...tunaweza kuacha dhambi...hivyo amini Mungu anaweza kukusaidia...na anaweza kukuokoa...lakini pia..amua kubadirika na kumwambia huyo mtu..kuwa humuhitaji tena kwa sababu..siyo sahihi kwako...ukimwambia hivyo...ukweli huo...atakuwa hana uwezo wa kukusumbua tena..
Kubari..kuishi bila mwanaume..ili utengeneze nafasi ya kupata mtu sahihi...wa maisha yako..
[21:49, 24/02/2018] Elisha Ndumizi: Ndugu..asate..kwa ajili ya kuendelea kufatilia somo hili..lakini pole kwa ajili ya hilo tatizo...
Naamini Yesu Kristo..anaweza mambo yote..na atakusaidia na wewe pia...
~Shetani ametumia njia ya mawasiliano...kuharibu hiyo ndoa yenu...lakini pia yawezekana yapo mambo mengine...lakini hilo la mawasiliano...ni kubwa sana..
Katika kitabu cha mwanzo ukisoma habati za mji wa babeli...utaona..wale watu walio taka kujenga mnala hadi mbinguni...nguvu yao ilikuwa katika lugha...na usemi mmoja...na hii ilileta ushirikiano...japo kuwa halikuwa wazo zuri .lakini walikuwa na nguvu...na ili kukwamisha..Mungu alishuka akaichafua..lugha...akachafua..mawasiliano..yao..na mwisho wakashinda kuelewana...
Nitafundisha zaidi..namna ya kurudisha uhusiano..na kudumisha mahusiano ya ndoa...kipindi kijacho..lakini..kwa sasa..naomba..tuliweke katika maombi swala lako..na hadi kipindi kijacho..naamini Yesu Kristo mtenda miujiza atakuwa amesha fanya..miujiza katika ndoa yako....
~ Karibuni kwa maswali..na ushauri...lakini.asanteni sana..kwa ushirikiano..wenu..na kwa kutuma hata ujumbe inbox..hii inaonyesha kuwa..tupo pamoja..na kuwa tunayo fundisha..yanawafikiwa..na yanamanufaa..
~ Endilea..kuombea sana huduma hii ili tuweze..kutoa mafundisho yatakayo kuokoa..na kukisaidia..pia kubadirisha maisha ya watu wengi zaidi...na endelea kusambaza masomo haya..kama sehemu ya uinjilist...
....Mungu akubariki sana....
Kwa mawasiliano zaidi...
Naitwa Elisha Ndumizi
0654501879.
Mtumishi kuna mtu umemjibu hapo juu nakusema ukidhini na mtu nafsi zenu zianaambatana...??
ReplyDeleteSasa tukirudi kibiblia yakobo alipewa kijakazi na racheli mkewe ili ampatie mtoto.
Na yule kijakazi sio mke halali wa yakobo..
Swali ni jee..?? Pale jakobo amedhini au...?? Na kama ajadhini inakuwaje kulala na kijakazi wako na isiwe kosa..
Vivyo hivyo kwa babu yake ambaye ni Ibrahim...
Mume wangu amerudi!!! Baada ya miaka 1 ya ndoa iliyovunjika, mume wangu aliniacha na watoto wawili na maisha yangu yalivunjika. Nilitaka kuyamaliza, nusura nijiue maana alituacha bila chochote. Nimekuwa nimevunjika kihisia wakati huu wote na maisha yanaonekana kutokuwa na maana. Siku moja mwaminifu, nilipokuwa nikivinjari mtandao, nilikutana na baadhi ya shuhuda kuhusu Dk DAWN. Baadhi ya watu walishuhudia kwamba alimrudisha mpenzi wao wa zamani, wengine walishuhudia kwamba anarejesha tumbo na kuponya magonjwa kwa mimea. Nilipendezwa zaidi na upatanisho na mume wangu, ambao Dk. DAWN aliwezesha kumrudisha mume wangu ndani ya siku 3. Sasa mume wangu amerudi na tumekuwa tukiishi kwa furaha tangu wakati huo. Shukrani zote kwa Dk DAWN. Hapa, ninaacha mawasiliano yake kwa kila mtu. Maana kuna changamoto za aina yoyote,
ReplyDeleteBarua pepe ( dawnacuna314@gmail.com )
Whatsapp: +2349046229159