NDOA NA MAHUSIANO

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana...
Namshukuru sana Mungu kwa ajili na neema hii ambayo ametupa..na kutupa kibari hiki cha kuiona siku hii ya leo...

karibuni sana wote katika somo letu...la MAHUSIANO NA NDOA...leo tutaendelea..katika ile sehemu tulipo ishia wiki iliyo pita...
~ Sehemu iliyo pita..tuliangalia mambo kaadhaa ya msingi kuangalia..ili kuweza kutunza mahusiano hako...au kabla hujaingia katika mahusiano...

-Tulisema Jua history ya mweza wako..
-Tulisema pia Jua Mahusiano yenu na Mungu...maana ndoa imara ni ndoa iriyo jengwa katika Kristo...
-Tukaona pia jitahidi kujua utamaduni wa mwenza wako...
-Tukaona pia jambo muhimu.. lingine...kuwa lazima UJUE HAIBA YA MWENZA WAKO.....
-Haiba ni tabia  au sifa ambayo inamtambulisha mtu...yaweza kuwa uchngamfu...hasira...upole..nk..
-Na kwa watalamu wa saikolojia ya mahusiano na tabia...wameziweka tabia na haiba za watu katika makundi manne....
+Sangwini
+Melankoli
+Flagmatik
+Kolerik
Na tuliangalia hayo makundi..kwa sehemu..
Sasa tunaendelea...

~ Kwa sasa jamii yetu imekuwa na migogoro mingi sana ya ndoa...na mahusiano...na hata kanisani...matatizo ya ndoa pia yamekuwa ni matatizo sugu sana...
~Shetani anatesa..watu...na anatumia mahusiano ya ndoa...kuwafanya watu wengi kujeruhika sana mioyoni mwao kwa sababu ya mahusiano..

Lakini...pia hata kwa vijana ambao bado hawajaoa...swala la ..mahusiano linasumbua sana..
.na hasa ni pindi wanapo taka kufanya maamuzi ya kuoa...hawajui...ni nani anafaa na nini wafanye ili wasikosee machaguo yao ya kuona 
~ Somo hili..linalenga tu kukupa taarifa ya mambo jinsi yalivyo..na kama utafanikiwa kupata taarifa...hizi ukiwa katika ndoa tayari au bado haujaingia katika ndoa..zitakusaidia...kufanya maamuzi sahihi...pia kuweza kushughulikia migogoro kwemye mahusiano yako
~ Napenda nikupe swali hili...
Tendo la ndoa..linachukua muda mdogo sana..tu may be masaa 2..Je masaa 22 ya siku yaliyobaki ili siku iishe yanatumikaje...?...au unayatumiaje...?

~Swali hili litakupa jibu..na jibu utakalo pata litakufanya utambue kuwa kumbe ili ndoa idumu siyo tendo la ndoa..tu.na tunaingia kwenye ndoa si kwa sababu ya tendo tu..

Watu wanasema mapenzi ni upofu....wengine wanasema mapenzi ni kama bahari..ukizama ndo umepotea...
~ Lakini mapenzi kwako haitakuwa upofu tangu leo...wala haitakuwa bahari tangu leo...kwa jina la Bwana;Yesu Kristo aliye hai

       Fahamu yafuatayo..
Ndoa siyo kitu cha dharura..ni mpango rasmi..na Mungu ndo ameweka na kuamua..
-sasa hii inamaana hii iwe uliingia kwa kuingizwa na Mungu...au uliingia tu...hata hukujua kwamba Mungu anahusika...ila kwa sababu..upo kwenye ndoa...Mungu anahitajika..na Mungu ndo aliweka huo utaratibu wa kuoana...hivyo anajua namna ya kuweza kukuongoza na kukutunza...mruhusu..yeye atakusaidia..

Unapo ingia katika ndoa ingia ukiwa unafahamu kuwa vipo vitu vingi sana mnatofautiana na huyo mwenzako...kama vile kifikra...kimtazamo na kimira na mifumo mbalimbali za makuzi na malezi zilizo mlea...

Ingia ukijua kuwa vipo vitu vingi ambavyo huvijui na huvifahamu juu ya huyo unae taka kuoana nae(ambae umeoana nae)

Ungia ukijua ni mwanzo wa safari ndefu sana inayoku unganisha na familia mbili tofauti na pia ni mwanzo wa kizazi cha watoto ambao hujawahi kuwaona

Ingia huku ukiwa unajua kabisa kuwa kuna ndoto za maisha yako zitasonga mbele lakini zipo zitakazo kufa...kabisa..na pia zipo ndoto mpya ambazo unatakiwa kuzipata na kuzianzisha...hivyo jiandae

Pia tambua huyo unae mchagua leo..au uliyo mchagua tayari upo nae..ni mwanadamu anaeishi katika dunia ya anguko-alizaliwa akiwa mwenye dhambi hivyo ni mwanadamu wa kawaida tu...ingia ukijua siku atafanya kama uonavyo dunia inafanya

     Pia tambua na kufahamu...
Huyo mtu anatabia za kijinsia hivyo kuna namna mko tofauti...
Mfano...katika kuwaza...mwanamke anawaza tofauti na mwanaume..pia mwanaume anawaza kama wanaume wengine..ile eti mmewaza kuoana na mawazo yenu yakakubaliana haina maana kila kitu mnawaza sawa...ingia ukijua..kuwa kila wkati utahitaji kujielezea kwa mwenzako hadi ueleweke..maana hata kuelewa maramoja tu...

-pia katika utoaji wa taarifa...mwanaume sisi tuna toa taarifa kwa maelezo mafupi tu..lakini mwanamke anapenda taarifa kwa maelezo marefu..na pia anataka apewe nafasi ya kutoa taarifa ndefu..
-pia utendaji kazi...na uwajibikaji

pamoja na tabia za kijinsia anamalezi na makuzi tofauti na ya kwako...
-mwanamke unaolewa na mwanaume ambaye yeye tangu yupo kwao...yeye ni mtoto mwanaume peke yake kwao..na dada zake walikuwa wakipika ili ale lazima wambembeleze..ndo anakuwa...sasa akikuoa na akawa haoni zile tabia za kike alizo ziona kwa dadazake kuwa wanawake..wanajua kubembeleza..
-sasa wewe mwanamke umetoka familia ambayo hakuna tofauti kati ya mtoto wa kiume na wakike..wote kazi tu...na wote kama ni kupika mnapeana zamu...
Lazima ujue sasa namna ya kuweza kuendana na makuzi na malezi

Pia kumbuka hili...SIKU ZOTE MNAPO TAKA  KUOANA KUNA MVUTANO WA KIHISIA..TU... sasa siku ikifika hisia zikawa zimeondaka..na ile hamu ya kufanya tendo la ndoa imekuwa siyo kitu kwenu...maisha yanakuwa tofauti...

Kitaalamu hapo kwenye tabia za kijinsia...mwanamke kila wiki anakuwa na tabia tafauti...kwa sababu ya mzunguko wa homoni zake..zinazohusika na mfumo wa uzazi...hivyo usishangae..wiki hili amechangamka...na wiki hili anajikuta anahasira nk....

Ebu tuangalie biblia inasemaje Wimbo ulio bora 2:1-4 *Mimi ni ua la uwandani,ni nyinyoro ya mabondeni...kama nyinyoro kati ya miiba..kadhalika mpenzi wangu kati ya binti..kama mpera kati ya miti ya msituni...kadhalika mpendwa wangu kati ya vijana...niliketi kivulini mwake kwa furaha..na matunda yake naliyainja kuwa matamu....akanileta mpaka nyumba ya karamu...na pendera yake juu yangu ni mapenzi...

~Mistari hii inatupeleka katika kipengele muhimu sana...ambacho nataka tukiangalie..kwa sehemu kidogo...nacho ni nawezaje kumjua...mtu anaye nifaa na sahihi kwangu....? Au nawezaje kudumu na mke wangu huyu ?

~Mwandishi ameonyesha namna ambavyo alikuwa anamwonyeshi huyu mhusika ambaye anajaribu kutuhadithia..habari zake yeye na mpenzi wake

~ Kwanza amejionesha kuwa yeye ni mzuri sana kama ua la uwandani..kuna sehemu akajitofautisha kuwa yeye ni mpera katikati ya miti ya msituni...hii inaobyesha kuwa ni wapekee kabisa..na sehemi aliyopo hafananishi na vyote vilivyopo..na vinavyo mzunguka...maana hata kama na yeye ni mti mstituni..lakini yeye ni mpera...sifa hizo za uzuri zmemfanya aweze kuwekwa katika nyumba ya karamu...lakini kawekwa hapo...kwa sababu ya mapenzi..siyo kwa sababu ya uzuri...ila sifa zile zmpeleka katika ndoa.. Sasa kabla hatujaenda mbali nataka nikupe mambo yafuatayo...

Maamuzi unayi yafanya ukiwa na taarifa zote sahihi ni maamuzi ambayo hautajuta

Unapo kuwa katika ndoa au ndo unataka kuingia..tambua kunavitu havita badirika kwa huyo mtu..mchukue mtu jinsi alivyo leo...na hakikisha unasema niko tayari hivi alivyo kamahauna ujasiri wa hilo...usifanya maamizi

Kuna vitu huwa vinachukua mda kubadirika..hivyo usikate tamaa vijapo chelewa kubadirika kwa mkeo au mmeo au huyo unae ingia nae kwenye mahusiano

Pia napenda utambua..kuna vitu vinataka wewe nbadirike...na siyo mwenzako

Elewa vitu vyote ili ujue namna ya kuishi na hugo mtu,pia kujua nani afanye nini na nani afanye nini...

Jitambue wewe na mtambue huyo unae mtaka au ambaye tayari upo nae katika ndoa

Mwangalie kama mke/mume pia kama mama/baba wa watoto wako pia ni ndugu wa ndugu zako..
Pia anafaa kwenda nae kwenye maona yako

Kijana ni marufuku kuchumbia wakati hujui unako kwenda...(haujui maono yako na maisha yako ya mbeleni)

Wasichana msiangalie fedha,gari,nyumba, bali fikiria na kuwa na msimamo wa kuolewa na mtu mwenye maono

Kila mtu anataka mke /mume mzuri na bora...hivyo sasa jiandae kuwa wewe ndo huyo mzuri na bora anayehitajika...
Zaburi 18:25

~Niishie hapa kwa sasa...tutaendelea hapa baadae...

Kwa mawasiliano....zaidi
Naitwa Elisha Ndumizi
0654501879

Comments

Popular posts from this blog

UWEZA WA MUNGU JUU YA MAGONJWA NA VYANZO VYAKE

UMUHIMU WA IBADA

IJUE IBADA-SEHEMU YA KWANZA